Irene Uwoya anafanya kazi gani?

Wakuu kwa kipindi kirefu nimekuwa nikimfuatilia huyu Mrs Janjaro ili nijue chanzo chake cha mapato ni nini haswaa maana nimemfuatilia weeee nimeambulia patupu nimeona nije kuwashirikisha humu wanajamvi huenda nikapata muangaza kidogo kuhusu wapi anapopata pesa zake.

Kwa kipindi cha hivi karibuni Uwoya mara kwa mara tunamuona akizunguka nchi mbalimbali huku akifanya kufuru kubwa ya pesa na pia wiki hii jumapili iliyopita kwenye Biko Jibebe Challenge tulimshuhudia Uwoya akimwaga mijipesa kwa mashabiki kama hana akili nzuri vile , na kama hiyo haitoshi Irene pesa zinamuwasha sana siku hizi , mara atume vocha za elfu kumi kumi za kila mtandao kuanzia Tigo, Voda, Halotel, TTCL, Airtel nk .

Pia juzi katoa ofa ya kuwauliza watu wanataka nini kutoka kwake ambapo kundi kubwa la watu walijitokeza na kumuomba mitaji ya biashara ba Uwoya bila hiyana akawapatia , na hatujakaa vizuri akatoa post IG akitaka watu wataje vitu saba wanavyovijua kutoka kwake ambapo mamia ya watu walijitokeza kutaja hivyo vitu na Irene akachagua washindi watatu ambao ataenda nao kula bata katika hotel zenye nyota tano kwa muda wa wiki moja na zoezi hilo kasema litakuwa endelevu kila mwisho wa mwezi, Sasa swali linabaki
Irene Uwoya anafanya kazi gani inayomuingia mijipesa yote hiyo au ni kweli anamegwa kisela na Diamond Platnumz??


View attachment 864523
Muda si mrefu utawasikia wakitembeza bakuli na kuomba kusaidiwa eti wameitangaza Tanzania
 
Ana mtaji wa mbunye used km 250,000.

Sent from my SM-J700H using Tapatalk
 
Back
Top Bottom