Ireland na European Countries, Je umaskini umeingia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ireland na European Countries, Je umaskini umeingia?

Discussion in 'International Forum' started by niweze, Dec 1, 2010.

 1. n

  niweze JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wanajamii Tujadili Kuanguka Kwa Uchumi Inchi za Ulaya. Leo Hii Tunasikia Ireland Inatupiwa Mkono wa Msaada Tena Baada ya Hali ya Uchumi Kuwa Mbaya. Kinachoendelea ni Kwamba Mabanki ya Ireland Hayana Pesa Tena na Uchumi Mzima Umekufa. Hii Imekuja Tu Baada ya Greece Kupewa Marundo ya Pesa ya Mikopo. Sasa Hivi Kuna Tetezi na Hizi ni za Uhakika Portugal na Italy are Next. Ujerumani Wamewaka Moto Hawataki Kuzisadia Majirani Zao Wakati Bidhaa Zao Nyingi Zinauzwa Huko. Tunaona Misaada Hii Katika Inchi za Ulaya Zinatoka IMF na EU Bank. Vitu Vingi Kama Waafrika Tunaweza Kujifunza ni Kwamba Umoja wa Ulaya Umesaidia Sana Inchi Zao na Tunaona Leo Hii Hawana Matatizo ya Kupata Mikopo Kama Inchi za Afrika Ilivyo.

  Vitu vya Kuuliza ni Kwamba IMF Inajali Inchi za Ulaya Sana na Kuwapa Deals Nzuri Kuliko Huko Africa? Kwanini Africa Haibadiliki kwa Hii Mikopo ya IMF? Kuna Vitu vya Kuangalia Jinsi Gani IMF na World Bank Zinafanya Huko Africa. Viongozi wa Africa Wanadhihirisha Hawana Majibu na Kila Mara Wanataka Kukimbilia IMF Bila Kufanya Thoughtful Review ya Resources Zao Kabla ya Kuomba Misaada. Wengi Tunaona Inchi Zetu Zina Weakness in Leadership na Tukipata Viongozi Hawa Wazuri na Wanaopenda Inchi Zao, Africa Itaanza Kubadilika. Angalia Egypt, Libya, Rwanda, Uganda, S. Africa, Tanzania, Zimbabwe Demokrasia Inaendelea Kuvunjwa...

  "A True Democratic Platform is Only Way Forward to Build Strong Africa"
   
Loading...