Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,402
Tangu Oktoba 01, 2019 Wananchi wa Iraq walianza maandamano ya dhidi ya Wanasiasa wanaoongoza nchi hiyo wakiwashutumu kwa mfumo uliokithiri rushwa na utawala usiokidhi katika kuongoza nchi
Taarifa zinadai kuwa siku za hivi karibuni, Polisi wanaopambana na Waandamanaji hao waliwatishia Waandamanaji kwa Mbwa waliofunzwa. Katika kujibu mapigo mmoja wa Waandamanaji aliandamana na Simba akishishia kumuachia Simba huyo kuwashambulia Mbwa wa Polisi na Polisi wenyewe
Takribani watu 319 wakiwemo Waandamanaji na Polisi wamefariki tangu kuzuka kwa maandamano hayo Kamati ya Bunge ya Haki za Binadamu imebainisha hayo
Waandamani wanaofunga mitaa, hususani Vijana wameigawanya nchi hiyo katika vipande viwili kipande cha mji mkuu Baghdad na Kipande chenye utajiri wa Mafuta Kusini mwa nchi hiyo
Makundi kadhaa ya Haki za Binadamu hivi karibuni wamelalamikia Polisi kwa kutumia nguvu zaidi katika kutuliza Waandamanaji hao
Amnesty International imezitaka Mamlaka za nchi hiyo kuvitaka vikosi vya kutuliza ghasi akutotumia nguvu, ikisema waandamanaji sita walifariki Jumamosi katikati ya Baghdad