Iranian commander: We could ‘destroy all US bases in region & create hell for Zionist regime’

Sasa nyie Iran,kama mmeshambuliwa,na Israel,mbona hamjajibu kwa kiwango kilekile,haya matamko wala hayana mashiko,
Maneno matupu hayavunji mfupa,mnasema ndogo iliyotunguliwa sio yenu,thibitisheni tuone uongo wa Israel,
Mpaka sasa HV,mmeshambulia vituo vingapi vya Israel au USA?,nyie waajemi/shia vipi?
Nyie dawa yenu ndogo tu,tunawapambsnisha na Saudia(suni) tu,mtafyata wenyewe mikia
Achana na hao Ayatollahs kazi kupenda misifa bila kuwa na chochote.
 
Sasa unadhani Israel watabakia hivyohivyo bila kufanyia marekebisho hizo kasoro zilizojitokeza.Mbona ndege ya Urusi imedunguliwa na ISIS juzi Syria hamuongelei hiyo mnaongelea tu tukio la Israel?
Rudia kusoma ulichoandika ni pumba yani yaonekana unamaumivu yaliyopitiliza hadi hueleweki uandikacho
 
hahahaha ngoja tusubiri mkuu ilo onyo la Iran halijakaa vizuri wamesema neno baya sana jehanam dah !!! Bila shaka mjomba wao Russia kawatuma!! Iran sio wa mchezo mchezo ulinzi wao wa anga ni sawa na wa north korea dah wana nusu mapipa ya north sio watu wa kudharau kabisa !!
Hiyo kauli "Jehanamu" hata mimi imenishtua mkuu. Hakika Russia na China wako nyuma ya Iran. Donald Trump ataleta maafa makubwa huko mashariki ya kati akifumbiwa macho.
 
"Kwani hayo mnayoyaita makombora USA hawana?", SirChief.

Marekani anaweza akawa nayo, ila na wasiwasi kwa kiasi flani kama watakuwa na hizo Intercontinental Ballistic Missile.

Kwa kuzingatia mtazamo huu.

Mwaka Jana Rais wa Marekani(Trump) aliruhusu kujipanga kikamikifu dhidi ya Korea Kaskazini kwa kuamuru USA aircraft carriers zikifahamika kama USS Ronald Reagan, USS Nimitz na USS Theodore Roosevelt. US carriers zote kwa pamoja zilifanya shughuli za kujiweka sawa kwa mambo makuu yafuatayo :-

1:Air defense drills
2:Sea surveillance
3:Defense air combat


Na hiyo haikutosha carriers hizo ziliambatana na takribani Aegis Ships 11(For tracking and guiding weapons to destroy enemies targets) na zikaongezeka meli vita zingine za Korea Kusini zisizo pungua 7.

Kwa waliobahatika kufuatilia mtanange huu wanasema ilikuwa ni mara ya kwanza kwa US aircraft carriers tatu kufanya mafunzo/mazoezi ya pamoja tangu mwaka 2007, Je ni kweli Kim Jong Un kawarudisha darasani Marekani na washirika wake?

Mara ya mwisho kwa US Aircraft Carriers tatu kuchana mawimbi kwa pamoja kwenye Peninsula ya Korea ni 1969 baada ya Korea Kaskazini kuifanyia mafanyo(Kuitungua) ndege ya Kimarekani(USA spy plane) na kusababisha vifo vya Wamarekani takribani 31(according to Naval history and Heritage command).

Swali.

1:Kwa nini Mr. Trump atumie nguvu nyingi kifedha na kuhatarisha assets zake zilizopo Japan, Korea Kusini na Guam, kama angekuwa na ICBM kwa ubora huo si angeyarusha toka Marekani mpaka karibu na Korea Kaskazini kama anavyofanya Kim Jong Un kwa Japan na Seoul?

2:Kuna habari Mr. Trump anaboresha budget kwa ajiri ya harakati tukutu zitakazo simamiwa na Pentagon kuhusu Nuclear Arsenal, hii inaashiria nini?
You are so smart mkuu kwenye haya mambo
 
Iran is talking, Syria is talking...

Israel is acting and destroying their bases inside Syria..!!
 
Jamani tusishangilie mambo ya kipumbavu yanayfanyika huko Middle East...watu wanakufa kama dagaa...Mungu arudi tu!
 
Iran katika propaganda hawa jamaa n wazur sana kwnye propaganda
Kama utakuwa unaelewa ama kumbukumbu ....basis utajuwa Hezbollah's waliwafanya nini Zionist in 2006 shubahamiti.... Ukweli si fagilii kabisa kwa mnyongee kuonewa ama kuuwa watu pasipo sababu ati kisa wewe una powers ..... What happened to Palestine similar to south Africa during apartheid times...inashangaza mnoo kwa mtanzania ama my African kum cherish criminal like nut yahoo.,....or Zionist fake Jews.... Real Jews are so good peoples...
 
Usemayo ni kweli siwez bisha hilo, uwezo wa marekan ni mkubwa ila unachangamoto zake
Hakuna taifa litakalo anzisha vita ya nuclear au litakalo jiingiza ktk vita ya Nuclear.
Kitendo cha DRPR walipo sema wao awataanzisha vita ila wakichokozwa watajibu vita kamili tena ya Nuclear nafikir unakumbuka hilo na alisema angelipua na kuzamisha meli vita za US na walizitoa mapema.

Nin nataka kisema, ni kwamba kwangu mim namuona NK (Kim) ndio shujaa wa mambo yake maana kila alilolipanga na analo lipanga anafanikiwa lisha ya kuwa na vikwazo vya dunia na Marekan.

Hakuna anacho kifanya kwa kulazimishwa bali anafanya kwa mipango yake na kwenda kinyume na Marekan kwa kila jambo.

Marekan akutaka ushirikiano wao hata wa Olympic na alionesha waz kupitia VP Mr Prince ambae akutaka hata kushirik chakula cha pamoja na alikaa china ya dakika 10 jukwaa waliloandaliwa na SK ktk mashindano. Na akesama wao na US Japan na ROK kuwa wataendelea kuitenga DRPK kwa kila kitu na kuongeza presha zaid had atakapo Denuclearize kitu ambacho NK awez kukifanya hata. Saiz US alipinga invitation ya Kim kwa Sk lakin SK wamekubali na wameanza maandalizi.

Ninacho kiona sio kwamba urafik wa marekan na sk utakwisha hapana ila terms nying za NK sitafanyiwa kaz kianina ila ndugu hawa wafurahi pamoja. Na Marekan atakaa Meza moja na NK kuzungumza juu usalama bila NK kuharibu Nuclear zake. Na atatambulika kama mataifa mengine yenye Nuclear siku za mbele

Huu ni mtazamo wangu kutokana na matokeo mbalimbali juu ya mgogoro wao had sasa
Daaah una akili sana wee kiumbe ubalikiwe kwa kweli ....waelevu kama were wako wachache mnoo ktk hii tz yetu..big up brother
 
hahahaha ngoja tusubiri mkuu ilo onyo la Iran halijakaa vizuri wamesema neno baya sana jehanam dah !!! Bila shaka mjomba wao Russia kawatuma!! Iran sio wa mchezo mchezo ulinzi wao wa anga ni sawa na wa north korea dah wana nusu mapipa ya north sio watu wa kudharau kabisa !!
 
Zipi ni propaganda sasa?.Kwani hayo unayoyaita makombora USA hawana?.Kwa akili yako unafikiri NK ana uwezo wa kuanzisha vita ya Nuclear na USA?.Hahaha,you must be crazy Man.Nimeshasema NK anajivunia geographical advantage na backup ya Urusi na China.Kama US angamua kuivamia NK,kuna uwezekano mkubwa China n Urusi wakaingia moja kwa moja kwenye hiyo vita kulinda maslahi yao,kama ilivykuwa 1950s.Sasa hapo ni calculated risks,either kuivamia NK na kuanzasha vota ya 3 au kuacha na kutafuta the other way ya ku deal nao?.Kingine kwenye hiyo vita US hawezi pata madhara makubwa kiasi hicho unachowaza wewe.SK ndo watakaoumia kwa 100%,sababu ndipo itakuwa battle ground.
Kuhusu ushuriki wa NK kwenye Olympic hilo siyo jamboa la ajabu,labda tu hujui kawa NK na SK ni ndugu wa damu.Walichotaka kufanya ni kutumia Olympic games kama njia ya kuzikutanisha familia zao sababu baada ya kugawanyika famlia zilitengana na huwa hawaruhusu kukutana kwa aina yyte ile.Wala usifikiri kuna siku SK watakujakuwaacha wamarekani na kujiunga na NK.Labda hujui geopolitics za pale peninsula ya korea.Kuna ma Players wakubwa sana pale wana influence ule mgogoro.BTW,hawa ma players wanajua kuliko mimi na wewe,tunachofnaya hapa ni kama ku guess tu.
Huna akili
 
220a015ab511985dcd29681484e2e3a1.jpg


Tehran(Irani) wamesema malalamiko ya Tel Aviv(Israeli) kuhusu Unmanned Aerial Vehicle(UAV)/Drone ya Irani kuangushwa na ndege ya Taifa la Israeli ni jambo ambalo ni upuuzi(illogical). Kamanda wa Irani emeonya kwamba watairuhusu/kuifungulia JEHANAMU kwenye ngome ya Kizayuni na kuharibu vituo vyote vya kijeshi vya Marekani vilivyopo nchini Israeli.

"Tuhuma kuhusu ndege/Drone ya Irani na kuhusika kwa Irani kuitungua ndege vita ya Kizayuni ni upuuzi", Bahran Qassemi(Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje wa Irani).

Bahran Qassemi amesema maofisa wa Irani nchini Siria wanafanya kazi za kishauri na wanafanya shughuli zao kwa ombi la serikali halali ya Siria na ya kisheria.

"Vitendo korofi vingine vikifanywa na Tel Aviv(Israeli) vitasababisha serious response. Na hiyo ndiyo itakayo kuwa sababu ya Irani kutengeza JEHANAMU ndani ya Taifa hilo la Kizayuni(Israeli)", Brigadier General Hosseini Salami(Mkuu msaidizi wa Iran's Elite Revolutionary Guards Corps).

Qassemi akaendelea kutema cheche kwa kusema Siria ni Taifa, na Serikali yake na Majeshi yake yanahaki ya kuiilinda mipaka ya nchi na kupambana na aina yoyote ya vitendo tukutu/korofi vya kigeni. Mapema siku ya Jumamosi Jeshi la Ulinzi la Israeli(IDF) limesema limeidhibiti UAV/Drone ya Irani ambayo iliruka mpaka wa Siria na kuingia Israeli. Kwa kujibu mapigo Israeli ilifanya mashambulizi ya anga kwenye maeneo yenye shughuli za Irani nchini Siria.

Jeshi la Israeli badae likasema kwamba ndege vita moja F-16 ilianguka kutokana na mashambulizi makubwa yaliofanywa na Siria. Marubani walifanikiwa kutoka ndani ya ndege na wapo salama. Kwa kujibu mashambulizi ya Siria, Israeli Defense Force (IDF) ikafanaya mashambulizi ya kutosha kwenye maeneo 12 yenye shughuli za Irani nchini Siria, Damascus hawajasita kusema vitendo vya Israeli ni UKOROFI.

Kugusia Sera za Marekani nchini Irani na vikwazo walivyowekewa Jamhuri ya Kiislamu(Irani), Salami amesema Irani inaweza kuharibu vituo vyote vya kijeshi vya Marekani vilivyopo nchini Israeli kwa kufanya mashambulizi kutoka nchini Irani.

Wasiwasi umepamba moto kati ya Israeli na Irani kutokana na tukio la Jumamosi. Jeshi la Israeli limemuonya Siria na Irani kwa kuruga uhuru wake kama Taifa kwa kusema kwamba nchi zote (Irani na Siria ) watalipa ghalama kubwa wakikiuka onyo hili. Israeli Defense Force (IDF) likaweka mkazo kwa kusema Tehran na Damascus wanacheza na MOTO.

We could ‘destroy all US bases in region & create hell for Zionist regime’ – Iranian commander
Hisia zako haziwezi elezea vitendo! Hujui wewe kaa utulie marekani na Israel hawafanyi kazi kwa maneno..!
 
Israel ni moto GOD is with them wale Iran atagongwa Kama mtoto
Israel ipi mkuu hii ya sasa iliojaa waashkenazi ama israel ambayo wengi wao walishatoweka mshariki ya kati???

Waisrael hao waliotajwa kwenye biblia ambao ndio taifa teule walitokana na abraham mwana wa shem ila Ashkenazi jews wametokana na gomer mwana wa japhet sasa mnaposema Mungu yupo nao mnachanganya sababu wale wa kale walitoweka na mpaka sasa hatujui wakwapi ila hawa waliopo ni waashkenazi ila sio wayahudi wale halisi waliotokana na uzao wa shem!!!
 
Back
Top Bottom