Iran yazindua mfumo wa kisasa wa makombora wa Khordad 15...unapiga mpaka kilometa 150

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,985
17,850
Iran imezindua mfumo wa kujilinda kwa makombora uliotengenezwa kikamilifu hapa nchini unaoweza kulenga shabaha sita za adui kwa wakati mmoja.

Mfumo huo wa makombora uliopewa jina la Khordad 15 umezinduliwa mbele ya Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Amir Hatami.

Akizungumza katika uzinduzi huo hii leo, Brigedia Jenerali Hatami amesema kuwa, mfumo wa makombora wa Khordad 15 una uwezo wa kugundua ndege za kivita na droni kutoka umbali wa kilomita 150 na kuzifuatilia katika umbali wa kilomita 120. Ameongeza kuwa mfumo huo wa makombora aidha una uwezo wa kugundua maeneo ya siri na kuyasambaratisha katika umbali wa kilomita 45.

Waziri wa Ulinzi wa Iran ameeleza pia kwamba mfumo wa ulinzi wa Khordad 15 unatumia makombora ya Sayyad 3; na una uwezo wa kugundua, kusambaratisha na kutungua shabaha sita kwa wakati mmoja.

Amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaunda mifumo mbalimbali ya kukabiliana na makombora na vitisho vingine vya anga kwa kuzingatia kuwepo vikosi vya kikanda katika kambi za nchi zinazoziunguka Iran.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeeleza kuwa uwezo wake wa kijeshi ni kwa ajili ya kujilinda na si tishio kwa nyingine nyingine.

Tujikumbushe pia iran ana mfumo wa Bavar-373 ambao unapiga kazi kama mfumo wa s300 wa urusiView attachment 1122840
4bsi0eea0b57231fpsk_800C450.jpeg
 
Iran yazindua mfumo wa kisasa wa makombora wa Khordad 15

Jun 09, 2019 13:56 UTC
Iran imezindua mfumo wa kujilinda kwa makombora uliotengenezwa kikamilifu hapa nchini unaoweza kulenga shabaha sita za adui kwa wakati mmoja.
Mfumo huo wa makombora uliopewa jina la Khordad 15 umezinduliwa mbele ya Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Amir Hatami. Akizungumza katika uzinduzi huo hii leo, Brigedia Jenerali Hatami amesema kuwa, mfumo wa makombora wa Khordad 15 una uwezo wa kugundua ndege za kivita na droni kutoka umbali wa kilomita 150 na kuzifuatilia katika umbali wa kilomita 120. Ameongeza kuwa mfumo huo wa makombora aidha una uwezo wa kugundua maeneo ya siri na kuyasambaratisha katika umbali wa kilomita 45.
Waziri wa Ulinzi wa Iran ameeleza pia kwamba mfumo wa ulinzi wa Khordad 15 unatumia makombora ya Sayyad 3; na una uwezo wa kugundua, kusambaratisha na kutungua shabaha sita kwa wakati mmoja.
Amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaunda mifumo mbalimbali ya kukabiliana na makombora na vitisho vingine vya anga kwa kuzingatia kuwepo vikosi vya kikanda katika kambi za nchi zinazoziunguka Iran.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeeleza kuwa uwezo wake wa kijeshi ni kwa ajili ya kujilinda na si tishio kwa nyingine nyingine.

Tujikumbushe pia iran ana mfumo wa Bavar-373 ambao unapiga kazi kama mfumo wa s300 wa urusiView attachment 1122840View attachment 1122841
Zimejaribiwa wapi?
Au watajaribia 'kuvita'
 
Mbona kile kikosi kipo ufukweni mwa iran (mijimeli iliosheheni madege vita, makombora kibao) tuone kijimeli kinaenda kuuziwa wese iran gaaademeti!!
Ipo ufukweni mwa iran???subutu yako meli za marekani zipo kwenye maji ya kimataifa na iran alishasema mmarekani akivuka mstari mwekundu tu akiingia pwani ya iran tu iran anazilipua hizo meli...

Acha bwabwaja
 
Mbona kile kikosi kipo ufukweni mwa iran (mijimeli iliosheheni madege vita, makombora kibao) tuone kijimeli kinaenda kuuziwa wese iran gaaademeti!!
Wee huelewi lengo la USA kupeleka vifaa vya kivita pale middle East.
Lengo halikua kuzuia Iran kuuza mafuta bali lengo ni deterrence against any possible attack of US interest from Iran or Iranian proxies.

Pia hiyo US aircraft carrier hiajaingia pwani ya Iran Bali ipo ktk international water hivyo haiwezi kushambuliwa na Iran
 
Zimejaribiwa wapi?
Au watajaribia 'kuvita'
Kujaribu wanazijaribu wenyewe kwenye war games au drills! Ukisikia war game au drill wenzetu hua hawaendi kupasua mawe kwa vichwa Bali ni kutest mitambo yao mbalimbali apo wanarusha drone ili zidakwe zikifanikiwa ndo wanazalisha kwa wingi pia wanarusha cruise missile au Ballistic missile then zikiwa intercepted then Test inakua OK hivo kupewa OK na wizara husika kwa ajiri ya kutengenezwa kwa wingi
 
Back
Top Bottom