Iran yazima jaribio la kushambuliwa shirika lake la nishati ya atomiki na hakuna chochote kilichotokea

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,840
17,438
Iran yazima jaribio la kushambuliwa shirika lake la nishati ya atomiki na hakuna chochote kilichotokea

Jun 24, 2021 03:06 UTC

[https://media]

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetibua njama za kuhujumiwa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya nchi hii mjini Karaj, nje kidogo ya mji mkuu Tehran.

Taarifa ya Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran (AEOI) imesema jaribio hilo la mapema jana Jumatano la kukishambulia kituo cha shirika hilo mjini Karaj limezimwa, na wala hakuna uharibifu wowote ulioripotiwa.

Imeongeza kuwa, hatua madhubuti za kiusalama katika taasisi hiyo ya nishati ya nyuklia ya Jamhuri ya Kiislamu zimepelekea kugonga ukuta njama hizo za maadui wa taifa la Iran.

Taarifa ya Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran imebainisha kuwa, uchunguzi wa kubaini wahusika wa njama hizo umeanzishwa.

Ikumbukwe kuwa, Aprili mwaka huu, sehemu moja ya umeme ya taasisi ya urutubishaji urani ya Shahid Ahmadi Roushan katika kituo cha nyuklia cha Natanz hapa nchini Iran ilihujumiwa.

[https://media]Kituo cha nishati ya nyuklia cha Natanz

Utawala wa Kizayuni wa Israel ulijigamba kuwa ndio uliofanya uharibifu huo huku vyombo vya habari vya Magharibi vikilivalia njuga mno suala hilo mpaka kufikia kudai kuwa eti urutubishaji urani nchini Iran utasimama kwa miezi kadhaa kutokana na uharibifu huo.

Hata hivyo Dk Ali Akbar Salehi, Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran alisisitiza kuwa, uharibifu huo haukuathiri zoezi hilo na urani iliyorutubishwa kwa asilimia 60 tayari imeanza kuzalishwa.
 
Drone ya Kamikaze huwa ikitumwa haikosi shabaha yake... Sehemu ya mitambo imeharibiwa na ililazimu wazime mitambo haraka la sivyo mlipuko ungejitengeneza wenyewe na mkubwa sana na ingekuwa ndio the end ya tamaa ya Nguvu za atomic huko iran.. kiufupi Iran ingeachana tu na mipango ya kishetani waliyojiapiza kuitenda dhidi ya israel maana hizi taabu hazitaisha.. Iran hawataki kuishi kama nchi zingine like Tanzania hatuzitishi nchi zingine
 
Na hiyo drone imerushwa toka humo humo Iran.
 
Alafu nadhan kwa namna Iran inavyoendesha mambo yake ktk mazingira tete ya uhasama na wamagharib na bado wanasimamia misimamo kulingana na maslah ya kinchi na bado nchi inaenda sisi watanzania tuna lakujifunza hapa ifikie kipind Tanzania yetu isimame kidete kwenye kusimamia maslah yake haijulish nan atasimama mbele yetu.
 
Drone ya Kamikaze huwa ikitumwa haikosi shabaha yake... Sehemu ya mitambo imeharibiwa na ililazimu wazime mitambo haraka la sivyo mlipuko ungejitengeneza wenyewe na mkubwa sana na ingekuwa ndio the end ya tamaa ya Nguvu za atomic huko iran.. kiufupi Iran ingeachana tu na mipango ya kishetani waliyojiapiza kuitenda dhidi ya israel maana hizi taabu hazitaisha.. Iran hawataki kuishi kama nchi zingine like Tanzania hatuzitishi nchi zingine
Ww ni mgonjwa wa akili uliekata tamaa, sasa unasema waache mpango wao ww kama nani, kwanza unaongea hivyo nchi yako uliwahi kunisaidia nini mpuuzi ww
 
Hivi kimsboy una maslahi gani na Iran? Kwa nia njema kabisa
Sio mpaka awe na maslahi. Kuna watu hobi yao ni kupenda haki na kutokupenda kuonewa au kutokupenda ubaguzi.

Wewe huoni wanaotaka kumzuia Iran asiwe na nyukilia ndio wenye nazo huku wakiwa wanaziboresha kila uchao?
Hata sisi Tanzania siku tukitaka kujitegemea na tukataka kulinda maslahi yetu tutaanza kuandamwa.

Asiyeelewa haya mambo ni mjinga wa mwisho!
Hata China imeweza kufika ilipo kutokana na kuwekeza kwenye jeshi la kisasa ambalo lazima liweze kuwa na silaha hatari kama walizo nazo maadui.

Dunia ya sasa kama huna silaha hatari kama nyuklia, silaha za kimtandao na silaha za kibaiolojia huwezi kulinda maslahi yako.

Ifike mahali tuamke... Mzungu hawezi kukuheshimu au hawezi kukaa meza moja na wewe kama huna vitu vya hatari kama alivyo navyo yeye
 
Sio mpaka awe na maslahi. Kuna watu hobi yao ni kupenda haki na kutokupenda kuonewa au kutokupenda ubaguzi.

Wewe huoni wanaotaka kumzuia Iran asiwe na nyukilia ndio wenye nazo huku wakiwa wanaziboresha kila uchao?
Hata sisi Tanzania siku tukitaka kujitegemea na tukataka kulinda maslahi yetu tutaanza kuandamwa?

Asiyeelewa haya mambo ni mjinga wa mwisho!
Hata China imeweza kufika ilipo kutokana na kuwekeza kwenye jeshi la kisasa ambalo lazima liweze kuwa na silaha hatari kama walizo nazo maadui.

Dunia ya sasa kama huna silaha hatari kama nyuklia, silaha za kimtandao na silaha za kibaiolojia huwezi kulinda maslahi yako.

Ifike mahali tuamke... Mzungu hawezi kukuheshimu au hawezi kukaa meza moja na wewe kama huna vitu vya hatari kama alivyo navyo yeye
Hawawezi kuzuia Bahari kujaa maji wanajisumbua tu
 
Ni Mwanapropaganda wa Muqawamma wa Shia kwa upande wa Afrika mashariki, kwenye misikiti ya Shia huwa wanafundishwa kuwneza propaganda za Iran.
Kama ww unavyofundishwa huko makanisani kuwapenda wayahudi na kuwachukia Waislam wakati huyo unaemuabudia alichezea kichapo na wayahudi na wala hakuna andiko alilosema kuwa yeye ni Mungu, wametokea wazungu akina paulo huku wakiwapotosha
 
Hivi kimsboy una maslahi gani na Iran? Kwa nia njema kabisa
Extremists km kimsboy ni watu htr sana, akiwa jirani jitahidi sana uhame, mimi nimeshuhudia jamaa mmoja ameacha kazi ya udaktari huko kagera kaenda kujiunga na kundi la waasi hapo msumbiji eti anaitimiza sunna! Extremists must not be allowed to live
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom