Iran yaufanyia majaribio na kuuboresha mfumo wa Bavar 373 sisi tupo bize kuua upinzani

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Iran yaufanyia majaribio mfumo wa makombora wa Bavar 373 kwa mafanikio makubwa
Naibu Waziri wa Ulinzi wa Iran, Ghasem Taghizadeh amesema kuwa jeshi la Iran limeufanyia majaribio mfumo wa ulinzi wa anga wa makombora wa Bavar 373 kwa mafanikio makubwa.
Kamanda Taghizadeh amesema kuwa miongoni mwa mafanikio ya Wizara ya Ulinzi ya Iran ni mfumo wa kurushia makombora wa Bavar 373. Ameendelea kubainisha kwamba, umbali wa masafa wa mfumo huo ni kilometa 200 na kwenda angani ni kilometa 27 na kwamba unahesabika kuwa wenye teknolojia ya kisasa kabisa na ulioundwa nchini hapa.
Kadhalika amezungumzia uundwaji wa ndege ya kivita ya Kauthar na kuongeza kuwa, ndege hiyo imejumuishwa katika kikosi cha Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwamba vifaa vyake vyote vimeundwa na wataalamu wa nchi hii kuanzia nyenzo na mfumo wake, kinyume na ilivyotangazwa na vyombo vya habari vya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Ameenda mbali na kusisitiza kwamba, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei alisema vyema pale alipoweka wazi kwamba, Marekani kamwe haitoingia vitani na Iran kwa sababu inajua vyema uwezo wa silaha na makombora ya nchi hii, na kwamba, hadi sasa jeshi la Iran halijaweka wazi baadhi ya teknolojia za kiulinzi inzozimiliki ambazo zipo tayari kutumiwa katika kujibu chokochoko za adui. Naibu Waziri wa Ulinzi wa Iran, Ghasem Taghizadeh ameongeza kwamba kipindi cha 'kupiga na kukimbia' kimepita na kwamba leo Iran inamiliki nyenzo za kisasa zikiwemo pia za makombora.

My take:Itachukua miaka 500 kuifikia iran
 
Tuna fanya manunuzi mkuu yni Ana daka nyuki watatu anaweka ndani akitegemea watatengeneza asali!
 
Hyo amtishi maana mossad ndo wanashiriki kulitengeneza na tiba yake ipo kwahyo hamtishi marekani hata chembe
 
Hahahahahaha sisi vipaumbele kupiga campaign wenyewe wa mlengwa wa kulia wakifanya wa kushoto ni uhaini huku raia tukifuatilia na mbabe kati ya TRA na mtoa laana
 
Back
Top Bottom