permanides
JF-Expert Member
- May 18, 2013
- 10,018
- 11,210
Kwenye Baraza la Usalama USA ni mwanachama wa kudumu na anaweza kublock maamuzi kwa kura yake ya veto. Kuna usawa flan unapaswa kuwepo kati ya mataifa, ila siamini kama mataifa yote yana hadhi sawa.Ni kama ilivyo kwa watu, ukiwa na fedha ni mtu ndio lakini unakuwa na hadhi tofauti, ndivyo ilivyo baina ya mataifa.Sudan na China pia sio wanachama. Baraza la usalama la kimataifa hapo ndilo litakalopendekeza kesi kwa mwendesha mashtaka au mwendesha mashtaka mwenyewe aamue kuchunguza. Kuhusu kutokuwa na nchi ya kumkamata sio swala la kushangilia sababu matokeo yake ndio haya tunayaona Congo, Ethiopia, Iran n.k. Dunia inahitaji usawa kwenye hivi vyombo vya kimataifa. Hatua ya kwanza kufikia usawa hapa ni kuona hati ya kumkamata inatoka baadae sasa tuangalie nani atamfunga paka kengele
Wa kumfunga kengele US hayupo, wala haitatokea kwenye kizazi hiki. Badala ya kuanzia kwa taifa kubwa kama US wangekomaa hata na kataifa kama Israeli, ili wakifanikiwa wapate pa kuanzia. Kwa sasa US is an "indomitable " force.