Iran yashika nafasi ya pili katika kutibu Corona duniani

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,990
17,869
Iran yashika nafasi ya pili katika kutibu Corona duniani

Takwimu rasmi zilizotolewa na mashirika ya kimataifa zinaonyesha kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeshika nafasi ya pili duniani katika uga wa kutibu na kuwezesha kupata afweni waathirika wa virusi vya Corona.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO), Iran inashika nafasi ya pili baada ya China katika mwenendo wa kuwa na idadi kubwa ya watu waliopona ugonjwa wa Covid-19 ambapo karibu asilimia 80 ya watu waliobainika kuathirika virusi vya Corona nchini hapa, wamepona. Kwa kuzingatia kwamba Iran ni kati ya nchi 10 duniani zenye idadi kubwa ya waathirika wa virusi vya Corona, kiwango cha watu waliopona, ugonjwa huo, ni kubwa kikilinganishwa na cha nchi nyingine.

China inashikilia nafasi ya kwanza ambapo asilimia 94 ya waathirika wa virusi vya Corona, wamepona. Katika uwanja huo Alireza Wahabzadeh, Mshauri wa Waziri wa Afya, Tiba na Mafunzo ya Udaktari nchini Iran amezungumzia takwimu za watu waliopona nchini hapa ikilinganishwa na nchi nyingine za dunia na kusema kuwa, mwenendo bora wa kuwafuatilia wagonjwa wa Corona na takwimu za watu waliopona zinaonyesha kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepiga hatua kubwa katika elimu ya tiba na katika uga wa matibabu duniani.


My take: Waajemi pamoja na vikwazo vya marekani kwamba hawawezi kuagiza hata paracetamol moja nje lakini bado wameweza kufikia kiwango hiki cha juu kabisa Wakati mwingine hujiuliza wairan ni binadamu wa aina gani?kwasababu japokua kuna vikwazo lakini wanazidi kushangaza ulimwengu

4bv812574cbf971n6m9_800C450.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom