Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Mataifa kadha yakiwemo hasimu mkubwa wa Iran, Saudi Arabia, wiki iliyopita yalikata uhusiano na Qatar baada ya kuishtumu kwa kufadhili ugaidi.
Mpaka na Saudi Arabia ambapo asilimia 40 ya chakula cha Qatar hupitia umefungwa.
Raia wa Qatar wameamrishwa kuondoka kutoka mataifa hayo lakini Qatar imesema kuwa haitafanya hivyo.
Haijulikani ikiwa chakula hicho ni msaada au ni cha kuuzwa.
Shirika la Ndege la Iran liliandika katika mtandao wa Twitter, wakati chakula hicho kikijazwa kwenye ndege ya nchini Iran.
Wadadisi wanasema kuwa uhusiano mzuri kati ya Qatar na Iran ni moja ya sababu zilizochangia mzozo huo.
Qatar kwa upande wake inasema haijajibu baada ya Saudi Arabia, Bahrain na UAE wiki iliyopita, kuamrisha raia wote wa Qatar waondoke ndani ya siku 14.
Karibu watu 11,000 kutoka nchi tatu wanaaminika kuishi nchini Qatar.
Chanzo: BBC