Iran yamtia mbaroni jasusi wa Shirika la Kijasusi la Marekani CIA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Iran yamtia mbaroni jasusi wa Shirika la Kijasusi la Marekani CIA

Discussion in 'International Forum' started by Imany John, Dec 18, 2011.

 1. Imany John

  Imany John Verified User

  #1
  Dec 18, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,777
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  Wizara ya Usalama wa Taifa
  Iran imemkamata jasusi wa
  Shirika la Kijasusi la Marekani
  CIA .
  Kukamatwa jasusi huyo
  mwenye asili ya Kiirani kumezima njama kubwa ya
  Marekani dhidi ya Jamhuri ya
  Kislamu ya Iran.
  Kwa mujibu wa taarifa ya
  Wizara ya Usalama wa Taifa,
  jasusi huyo wa Marekani anafanya kazi kama
  mchambuzi wa CIA na ana
  uzoefu wa kikazi katika
  Kitengo cha Usalama cha Jeshi
  la Marekani ambapo
  amehudumu Iraq na Afghanistan. Alikuwa
  amepewa jukumu la kazi nyeti
  za kijasusi ikiwa ni pamoja na
  kujipenyeza katika Wizara ya
  Usalama wa Taifa Iran. Taarifa
  hiyo inasema jasusi huyo alipata mafunzo ya kiwango
  cha juu kabla ya kuanza kazi
  yake. Alitambuliwa na maafisa
  wa usalama wa Iran mara tu
  alipowasili katika uwanja wa
  ndege wa jeshi la Marekani huko Bagram nchini
  Afghanistan. Alipoingia Iran,
  jasusi huyo wa Marekani
  alinaswa kabala hajaanza kazi
  zake. Hii si mara ya kwanza
  majasusi wa CIA kukamatwa Iran. Mwezi Mei mwaka huu
  mtandao wa majasusi 30 wa
  CIA walikamatwa hapa nchini.
  Aidha Novemba 24 Iran
  ilitangaza kuwatia nguvuni
  majasusi kadhaa wa Marekani waliokuwa na jukumu la
  kuharibu vituo vya nyuklia vya
  Iran na maeneo mengine
  muhimu.

  Source:radio tehran swahili.
   
 2. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,268
  Likes Received: 8,334
  Trophy Points: 280
  aise,aah saaafi.
   
 3. Imany John

  Imany John Verified User

  #3
  Dec 18, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,777
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  Jamaa wanatisha kama njaa.
   
 4. k

  kimini Member

  #4
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Du usalama wa iran ni noma kweli yani cjui kama wa kwetu wana skilz kama hizo za watu wa iran,
   
 5. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  propaganda za iran zinaniacha hoi!
   
 6. Imany John

  Imany John Verified User

  #6
  Dec 18, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,777
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  Hahaha umbea ndo ngao ya jeshi letu.ila yule dogo wa dar ambaye ali hack akaunti za riz one na mamaye nimesikia amekamatwa dar.
   
 7. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,929
  Trophy Points: 280
  Watakuwa wana wapelelezi wao Afghanistan endapo waligunduwa kuwa wamarekani wanapitisha majasusi huko, dunia ya sasa ni pesa inaongea, mamulah wanajuana kwa vilemba.
   
 8. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,824
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Mnyongeni hafharani mpuuzi huyo...japokua hata nyie iran ni wanafiki ila mko juu sana hawa mbwa wa US ni kuwaua tu,,,
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hongera ahmednejad
   
 10. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #10
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Safi sana IRAN. Uzi huo huo, piga kitanzi huyo mamluki.
   
 11. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #11
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Jamaa namkubali
   
 12. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #12
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Sie huku tunawakamata akina kibanda,ndo intelijensia ilipo
   
 13. g

  goodlucksanga Senior Member

  #13
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbwembwe tuuuuu hizo unachezea marekani veveeeee.....!!
   
 14. N

  Nonda JF-Expert Member

  #14
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. MpigaKura

  MpigaKura JF-Expert Member

  #15
  Dec 20, 2011
  Joined: Jan 25, 2007
  Messages: 385
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Safi sana...

  Vipi kwetu TZ..

  Kuna hata siku moja tumesikia jamaa wa usalama wamedaka jasusi la nchi nyingine likiwa katika spying mission?
   
 16. MpigaKura

  MpigaKura JF-Expert Member

  #16
  Dec 20, 2011
  Joined: Jan 25, 2007
  Messages: 385
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  US demands release of CIA spy by Iran

  The United States has demanded that Iran release "without delay" a CIA spy who was recently detained in the country and who confessed to being commissioned by the US to infiltrate Iran's intelligence circles.

  On December 17, Iran's Intelligence Ministry announced the capture of an American CIA agent of Iranian decent, foiling an intricate US plot to carry out further espionage activities in the Islamic Republic following the capture of an American spy drone in northeastern Iran.

  US State Department spokeswoman Victoria Nuland announced on Monday that the US had requested access to Hekmati through the embassy of Switzerland, which maintains a US interest section in Tehran in the absence of diplomatic relations between the two countries.

  Nuland told reporters "We call on the Iranian government to grant the Swiss protecting power immediate access to him and release him without delay."

  She claimed that the family of the detained US spy first reported his detention in September and that the State Department has offered the relatives consular assistance.

  This is not the first time Iran arrests CIA spies. On May 30, members of a CIA espionage and sabotage network were arrested by the Iranian Intelligence Ministry.

  SOURCE: US demands release of CIA spy by Iran
   
Loading...