Iran yajiimarisha kwa drone na makombora ya kisasa

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,887
Kamanda: IRGC imejizatiti kwa makombora na drone za kisasa
Nov 12, 2019 02:59 UTC

Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) ameashiria kuhusu kuendelea kuimarika uwezo wa kujihami wa Iran na kusema kuwa, taifa hili limejizatiti kwa makombora yenye uwezo wa kulenga shabaha kwa ustadi mkubwa na ndege zisizo na rubani (drones) za kisasa.

Brigedia Jenerali Mohammad Pakpour alisema hayo jana Jumatatu katika hotuba yake katika mkoa wa Esfahan wa katikati mwa Iran na kuongeza kuwa, "Kikosi cha Nchi Kavu cha IRGC kimejihami barabara kwa silaha mpya na za kisasa."

Amesema zana za kijeshi zinazotumiwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hii leo hazifanani na zile ilizozitumia katika enzi za Vita vya Kujihami Kutakatifu vilivyoanzishwa na aliyekuwa dikteta wa Iraq, Saddam Hussein dhidi ya taifa hili katika miaka 1980.

Amesema iwapo Iran ingelikuwa na zana ilizonazo hivi sasa, isingepata changamoto zozote katika vita hivyo vya kulazimishwa na kwamba wakati huu, uwezo wake wa kijeshi umeimarika kuliko wakati mwingine wowote ule.
Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, taifa hili linaona fakhari kuwa na ujuzi wa hali ya juu na wataalamu wenye uelewa wa kuzalisha na kutumia zana za kijeshi za kisasa, kwa shabaha ya kulihami taifa hili.

Brigedia Jenerali Mohammad Pakpour ameeleza bayana kuwa, "Maadui wa nchi hii wanafanya kila wawezalo kutoa pigo kwa makundi ya muqawama sambamba na kuzusha hofu na vitisho kwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ili uachane na malengo yake; hata hivyo vitisho hivyo havijakuwa na matokeo yoyote ghairi ya kushindwa maadui."

4bsmeb7744334a1iuvv_800C450.jpeg
 
Sawa muajem mweusi ngoja tusubiri wamarekani wa Tandale nao waje wajibu mapigo
 
View attachment 1261132
Mvaa pedo mwenzako kagongwa Gaza kaomboleze huko
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom