Iran yaipa tanzania dola milioni 1.2 kusaidia kilimo kwanza

mdau wetu

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
548
58
IRANI YATOA DOLA MILIONI 1.2 KUSAIDIA KILIMO KWANZA NCHINI TANZANIA

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu (Kulia),akizungumza na Naibu Balozi wa Irani hapa nchini Bw Bahman Ahmadi(Kushoto) alipomtembelea Ofisini kwake leo. Mwingine ni Mshauri wa kibiashara katika Ubalozi wa Iran hapa nchini Bw Mobasher.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu (Kushoto),katika picha ya pamoja na wageni wake Naibu Balozi wa Irani hapa nchini Bw Bahman Ahmadi(Katikati) na Mshauri wa kibiashara katika Ubalozi wa Iran hapa nchini Bw Mobasher (Kulia).

Katika kusaidia kutekeleza kwa vitendo kampeni ya Kilimo Kwanza, Serikali ya Irani itaisadia Tanzania Dola za kimarekani Milioni moja pointi mbili ($ 1.2Mil) kwa ajili ya kampeni hiyo.

Taarifa hiyo njema imetolewa Jijini Dar es salaam leo, wakati Balozi Msaidizi wa Iran hapa nchini Bw Bahman Ahmadi alipotembelea Wizara ya Viwanda na Biashara na kukutana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh Lazaro Nyalandu.

Katika mazungumzo hayo yaliyojikita katika kuimarisha Uhusiano mwema bana ya nchi hizi mbili hasa kibiashara, Mh Nyalandu kwa niaba ya serikali ya Tanzania, ameishukuru serikali ya Iran kwa msaada huo na kuahidi kuwa utatumika kama ulivyokusudiwa.

Aidha, Mheshimiwa Nyalandu amewakaribisha wawekezaji kutoka Iran kuja nchini na kushirikiana na wazalendo katika kutumia vyema fursa mbalimbali zilizopo hasa katika sekta ya Kilimo.
 
Mambo ya aibu hayo! Serikali ingemuomba mzee wa Visenti tu

Hivyo mapato ya madini Tanzania ni kiasi gani kwa mwaka, utalii na uwindaji unaingiza kiasi gani kwa mwaka mpaka tuanze kutembeza bakuli hii ni aibu. Kuna mtu aliwahi sema uchumi tunao lakini tunaukalia, hakukosea kabisa.
 
jiulize na wao watapewa nini???unajua hizo hela ni za walipa kodi wa iran tena ni laana kubwa ndio maana kagame amekataa huu upuuzi
 
Hii serikali kweli iko ki-matonya matonya hata hela kidogo namna hiyo wanapokea? RA ana-make over 280 mil. $ per year kwa nini wasingemuomba hako kadola mil 1.2?
 
IRANI YATOA DOLA MILIONI 1.2 KUSAIDIA KILIMO KWANZA NCHINI TANZANIA

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu (Kulia),akizungumza na Naibu Balozi wa Irani hapa nchini Bw Bahman Ahmadi(Kushoto) alipomtembelea Ofisini kwake leo. Mwingine ni Mshauri wa kibiashara katika Ubalozi wa Iran hapa nchini Bw Mobasher.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu (Kushoto),katika picha ya pamoja na wageni wake Naibu Balozi wa Irani hapa nchini Bw Bahman Ahmadi(Katikati) na Mshauri wa kibiashara katika Ubalozi wa Iran hapa nchini Bw Mobasher (Kulia).

Iran wanatuchora nilifikiri umesema $1.2 Bil. kumbe ni hela ambayo hata akina EL na RA au Manji au Mengi wangeweza tu kutoa kama zawadi au wakachangishana.

nyalandu angalia na wewe mh. huu msaada alitakiwa akapokee katibu muhtasi wako na siyo wewe mkuu.

Is there any good thing from IRAN ANYWAY?

Katika kusaidia kutekeleza kwa vitendo kampeni ya Kilimo Kwanza, Serikali ya Irani itaisadia Tanzania Dola za kimarekani Milioni moja pointi mbili ($ 1.2Mil) kwa ajili ya kampeni hiyo.

Taarifa hiyo njema imetolewa Jijini Dar es salaam leo, wakati Balozi Msaidizi wa Iran hapa nchini Bw Bahman Ahmadi alipotembelea Wizara ya Viwanda na Biashara na kukutana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh Lazaro Nyalandu.

Katika mazungumzo hayo yaliyojikita katika kuimarisha Uhusiano mwema bana ya nchi hizi mbili hasa kibiashara, Mh Nyalandu kwa niaba ya serikali ya Tanzania, ameishukuru serikali ya Iran kwa msaada huo na kuahidi kuwa utatumika kama ulivyokusudiwa.

Aidha, Mheshimiwa Nyalandu amewakaribisha wawekezaji kutoka Iran kuja nchini na kushirikiana na wazalendo katika kutumia vyema fursa mbalimbali zilizopo hasa katika sekta ya Kilimo.

Iran wanatuchora nilifikiri umesema $1.2 Bil. kumbe ni hela ambayo hata akina EL na RA au Manji au Mengi wangeweza tu kutoa kama zawadi au wakachangishana.

nyalandu angalia na wewe mh. huu msaada alitakiwa akapokee katibu muhtasi wako na siyo wewe mkuu.

Is there any good thing from IRAN ANYWAY?
 
mbona hao uliowataja hawatoi basi, kazi yao kusaidia vikundi vya taarabu na timu za mpira tu, eboo
 
Back
Top Bottom