Iran yabadili mawazo ya kuzituma black box Ukraine, ikisema bado inajaribu kuchukua data zilizomo ndani

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Maafisa wa Iran wanaoongoza Uchunguzi wa ajali ya Ndege ya Abiria ya Ukraine iliyotungiliwa na Iran wamebadili mawazo ya kutuma 'Black Box' Nchi za nje kwa Uchunguzi

Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Mkuu wa Uchunguzi wa Ajali katika Mamlaka ya Anga ya Iran, Hassan Rezaeifer kusema vifaa hivyo haviwezi kusomwa Iran na watavipeleka Kyiv, Ukraine

Akinukuliwa na Shirika la Habari linaloongozwa na Serikali, Tasnim, Hassan amesema, "Black Box hizo kutoka kwenye ndege ya Ukraine zipo mikononi mwa Iran na hatuna mpango wa kutuma popote."

Amesema, Iran inafanya kazi kuzipata Data zilizo ndani ya 'Black Box' hizo na kwa wanaweza kuvituma vifaa hivyo Ufaransa au Ukraine ile kwa sasa wajafanya maamuzi

Iran awali lisema itapeleka Ukraine vifaa hivyo vya ndege iliyoua watu wote 176, ili maafisa wa Marekani, Canada na Ufaransa wakavichunguze
*******

The official leading the investigation into the Ukrainian plane shot down by Iran has appeared to backtrack on plans to send the black boxes abroad for analysis, a day after saying they would be sent to Kyiv.

Hassan Rezaeifer, the head of accident investigations for the civil aviation department, had said on Saturday the flight recorders could not be read in Iran, so they would be sent to Kyiv, where French, American and Canadian experts could analyse them.

However in an apparent u-turn, he was quoted by the state-run Tasnim news agency as saying: “The flight recorders from the Ukrainian Boeing are in Iranian hands and we have no plans to send them out."

He said Iran was working to recover the data and cabin recordings, and that it may send the flight recorders – commonly known as black boxes – to Ukraine or France. “But as of yet, we have made no decision.”

Iranian officials previously said the black boxes were damaged but usable.
 
IRAN Hua Namkubali Maana Hua Anafanya Jambo Anavyopenda Sio Kulazimishwa.....

Safi Sanaaa Wakimaliza Kuharibu Ushahidi Watawapelekea Wenyewe

Lile tukio lakuangushwa ndege linaonekana halikua labahati mbaya kiukwel

Sent using Jamii Forums mobile app
kama utakumbuka niliwahi sema humu kuhusu mauaji ya General kwishnei sasa ni ndege>mkataba wa nyuklia then mabomu Iran.
 
Sahihi ila inasemekana Kuna mkono wa US, yaani maelezo fulani yalikuwa yanatembea WhatsApp eti kwamba US wali intercept mawasiliano ya pilot wakajifanya kama Jeshi la Iran wakiionya ndege hiyo irudi Teheran au itashambulia. Pilot pasipo hila akageuza kurudi Teheran, waajemi wakaona ndege isiyo na taarifa wakajua ni hostile flight wakaidungua faster maana haikuwemo kwenye ratiba zao. Happy US akawa amefanikiwa kuwachonganisha waajemi na ulimwengu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaambiwa missiles mbili zilipiga ile ndege. Ya kwanza ilivyopiga ndege wakaona haitoshi,wakatuma na ya pili. Sasa hapa utasema vipi bahati mbaya ? GAZETI LA NEWYORK TIMES.
Wanaona wakitoa blackboxes kuna vitu ambavyo hawataki vijulikane vitajulikana.
Iran waunyute hivyo hivyo. Mbona Russia waliunyuti pale Ukraine Separists ambao ni pro Russia walipoitungua MH 17?
 
Ndege na mawasiliano ya ndege hayaingiliki vinginevyo watu wasingehangaika ziteka na kujiua wangekuwa wanazishusha tu kwa data

Japo ndege ya Rais wa Marekani iliwahi ingiliwa na wakaambiwa kuna Bomu, wakahesabiwa hadi 0 ila hakuna kilichotokea,

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hao wa Iran wameishangaza Dunia jamaaa wana shabaha iliyopitiliza!
Pia technology wapo mbali Sana Sana iyo ndege waliangusha kwa sababu wanazo juwa wao!
Hizi ndege za abiri hutumika kwa masuala ya upelelezi pia! Ndio maana zikibainika Dawa ni moja tu kuangushwa!
Ukiona wamesema hawakitowi juwa ni Salam izo!
 
Sahihi ila inasemekana Kuna mkono wa US, yaani maelezo fulani yalikuwa yanatembea WhatsApp eti kwamba US wali intercept mawasiliano ya pilot wakajifanya kama Jeshi la Iran wakiionya ndege hiyo irudi Teheran au itashambulia. Pilot pasipo hila akageuza kurudi Teheran, waajemi wakaona ndege isiyo na taarifa wakajua ni hostile flight wakaidungua faster maana haikuwemo kwenye ratiba zao. Happy US akawa amefanikiwa kuwachonganisha waajemi na ulimwengu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nalendwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa ndivyo unavyodhihirisha ushetani wako, unafurahia hata Wairani wenzio walivyouawa?

IRAN Hua Namkubali Maana Hua Anafanya Jambo Anavyopenda Sio Kulazimishwa.....

Safi Sanaaa Wakimaliza Kuharibu Ushahidi Watawapelekea Wenyewe

Lile tukio lakuangushwa ndege linaonekana halikua labahati mbaya kiukwel

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaambiwa missiles mbili zilipiga ile ndege. Ya kwanza ilivyopiga ndege wakaona haitoshi,wakatuma na ya pili. Sasa hapa utasema vipi bahati mbaya ? GAZETI LA NEWYORK TIMES.
Wanaona wakitoa blackboxes kuna vitu ambavyo hawataki vijulikane vitajulikana.
Iran waunyute hivyo hivyo. Mbona Russia waliunyuti pale Ukraine Separists ambao ni pro Russia walipoitungua MH 17?
Kosa kubwa ni kutolifunga anga lao ili kutoruhusu safari za ndege wakijua fika kuwa kuna hatari ya mashambulizi kufanyika.

Huo ni ukurupukaji na uzembe wa hali ya juu unaopaswa kukemewa kwa nguvu zote ili usijirudie tena.
 
Kitendo cha kutuma missiles mbili ni volley strike ambayo inatumika sana hasa na Russia kuhakikisha target inapigwa. Kwa hiyo point ya bahati mbaya haifutiki kisa wametuma mara mbili. Then Russia hakupiga kimya kwenye ndege ya Malaysia kama unavyodai, alitoa ushahidi kuwa hakuhusika, hata hizi missile walizonazo Iran zilitengenezwa Russia mbona hapa hawajasema anahusika. Waasi ni pro-Russian lakini nchi inakana sasa tutafanya nini. Mwisho gazeti lako ni NEW YORK TIMES, kwamba kuna siku Musiba ataisifia Chadema hapo sijui.
 
Ndege na mawasiliano ya ndege hayaingiliki vinginevyo watu wasingehangaika ziteka na kujiua wangekuwa wanazishusha tu kwa data

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndege hawawezi kuhack? Yaani wanaiba data kwenye ofisi za Lockheed Martin washindwe hack ndege ambayo haina ulinzi wa kijeshi. Russia walihack meli ya U.S ya kivita ikazima umeme sembuse ndege ya abiria. Teknolojia inaweza mengi sana.
 
Kosa kubwa ni kutolifunga anga lao ili kutoruhusu safari za ndege wakijua fika kuwa kuna hatari ya mashambulizi kufanyika.

Huo ni ukurupukaji na uzembe wa hali ya juu unaopaswa kukemewa kwa nguvu zote ili usijirudie tena.
Kabisa. Hapa walikosea sana. Ingawa wanasema hata wao wanaregreat. Sasa sijui kweli wanaregreat au ni siasa tu. Maana ile haikuwa bahati mbaya ile.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom