Iran wazindua meli mpya ya kivita ya kisasa

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Iran yazindua manowari mpya ya kisasa katika Ghuba ya Uajemi
Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limezindua manowari mpya ya kisasa yenye uwezo mkubwa wa kuvurumisha makombora.
Uzinduzi huo umefanyika mapema leo Jumamosi katika maji ya Ghuba ya Uajemi, na kuhudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Iran, wakiongozwa na Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi.
Meli hiyo ya kijeshi iliyoundwa kwa teknolojia na wataalamu wa hapa nchini, imesheheni mifumo ya kisasa yenye uwezo wa kuvurumisha makombora ya chini ya maji (torpedo).
Manowari hiyo iliyopewa jina la Sahand ina uwezo wa kufanya operesheni za masafa marefu katika maji makuu, na kwa zaidi ya miezi miwili.
Meli hiyo ya kijeshi ya Sahand ni katika mfululizo wa Miradi ya Mowj (Wimbi) inayofanywa na Jeshi la Majini la Iran, ambayo tayari imezalisha pia manowari za Jamaran na Damavand.
Jeshi la Majini la Iran mbali na kulinda maji ya taifa hili, lakini pia limezima mara kadhaa mashambulizi ya maharamia dhidi ya meli za mizigo na mafuta za nchi hii na nchi nyingine katika maji ya kimataifa.
 
kongole zao waache hao kina saudia kukumbatia ununuzi badala ya kuunda vyao
 
Back
Top Bottom