Iran: Watu 81 wapoteza maisha kutokana na homa ya mafua

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Watu 81 wamekufa kwa sababu ya janga la homa ya mafua
Mafua yasababisha vifo Iran


Watu 81 wamekufa kwa sababu ya janga la homa ya mafua nchini Iran.
Naibu Waziri wa Afya wa Iran Ali Riza Reisi, ameliambia shirika rasmi la habari la Iran wiki iliyopita, kuwa watu elfu 8 333 wamefika mahospitalini wakilalamika kandamwa na mafua makali.

Karibu nusu ya watu hawa walilazwa hospitalini kwa zaidi ya siku 2 kwa sababu ya shida ya kupumua.
Hali hiyo ilipelekea wagonjwa wengine watibiwa wakiwa wamesimama.

Idadi ya waliopoteza maisha wiki iliyopita ni 25,jumla ni watu 81 wamepoteza maisha kutokana na homa ya mafua nchini humo.

Waziri amewataka wananchi kuzingatia maazimio ya Wizara ya Afya ili kudhibiti kuendelea kwa homa hiyo.
 
Sina shaka Iran ilitumia baadhi ya kemikali za sumu kuzima yale maandamano ndo maana wakazima na intaneti ili Dunia isione unyama waliokua wakitenda.
 
Naanza kuamini Maneno ya Trump kuwa Iran iliua raia zaidi ya 1000 so wanazuga kuwa raia wamekufa kwa Mafua dah!
 
Back
Top Bottom