Iran: Tupo tayari kuwasaidia wapiganaji wa Kipalestina kwa kila hali

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
5,698
2,000
Jenerali Qassem Soleimani: Iran iko tayari kuvisaidia vikosi vya Muqawama vya Palestina kwa kila hali
Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) ametangaza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kutoa msukumo na kuvisaidia kwa kila hali vikosi vya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina.
Meja Jenerali Qassem Soleimani ameyasema hayo katika mazungumzo aliyofanya kwa njia ya simu na makamanda wa brigedi za Izzuddin al- Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS na wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina pia.
Katika mazungumzo hayo Jenerali Qassem Soleimani amesisitiza pia kwamba makundi mengine ya Muqawama katika eneo la Mashariki ya Kati yako tayari kuuhami msikiti mtukufu wa Al Aqsa.
Jumatano ya tarehe 6 ya mwezi huu wa Desemba, Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza uamuzi ambao kwa mujibu wa jumuiya za kimataifa na nchi mbalimbali duniani unagongana na kukinzana na maazimio ya kimataifa. Trump aliitangaza Baitul Muqaddas kuwa mji mkuu wa Israel na kutoa amri ya kufanywa maandalizi ya kuuhamishia katika mji huo ubalozi wa Marekani ulioko Tel Aviv.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilikuwa miongoni mwa nchi za mwanzo ambazo zililaani hatua hiyo ya Trump. Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ilitoa taarifa siku hiyo hiyo ya Jumatano usiku na kusisitiza kwamba hatua ya Rais wa Marekani ya kuitambua Quds kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni ni ukiukaji wa wazi wa maazimio ya kimataifa.
Nchi nyingi duniani pamoja na jumuiya za kimataifa, nazo pia zimelaani hatua hiyo ya Trump...

Chanzo; Radio tehran
 

Jackal

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
6,108
2,000
Iran ilishaanza kuwasaidia wapalestina miaka nenda rudi.Mpaka leo juhudi zao zimegonga mwamba!
 

Liwagu

JF-Expert Member
Jan 25, 2017
2,127
2,000
Iran wanajuwa hawawezi kujaribu kutia miguuyao waziwazi huko Israel, wanajaribu tu kutoa kauli za kuhamasishatuu ilikupima upepo kwa mataifamengine ya kiarabu.
 

ivunya

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
1,642
2,000
Amani imeshatoweka ilo eneo, silah zitaanza kutapakaa ilo eneo, rocket za masafa marefu yatatafutwa na kurushwa
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
13,003
2,000
Ha ha ha! Mwajemi ni pumbafu kweli. Hadi His Excellency D. Trump anatia signature ile declaration; recognition of Jerusalan as the sole, indivisible capital of Israel all options had been considered.

Ilifahamika wazi hao mbwa wangebweka na solution was very clear; what next if that happens. Mayahudi wenyewe wamekuwa vitani tangu nyakati za mtoto daudi akilichinja lile jitu lisilojua tohara ndio itakuwa leo. Waache kucheza na moto; watamalizwa kwa makundi. Shauri yao.
 

Mangachini

Senior Member
Mar 24, 2014
138
225
Halafu ushangae Israel kuna waziri wa Vita!! Yaani mbali na waziri wa Ulinzi, kuna Waziri wa Vita, ndipo ujue kwamba hawa jamaa, maisha yao ni vita!!
 

Kingsharon92

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
6,730
2,000
Ha ha ha! Mwajemi ni pumbafu kweli. Hadi His Excellency D. Trump anatia signature ile declaration; recognition of Jerusalan as the sole, indivisible capital of Israel all options had been considered.

Ilifahamika wazi hao mbwa wangebweka na solution was very clear; what next if that happens. Mayahudi wenyewe wamekuwa vitani tangu nyakati za mtoto daudi akilichinja lile jitu lisilojua tohara ndio itakuwa leo. Waache kucheza na moto; watamalizwa kwa makundi. Shauri yao.
Mimi nasubiri utekelezaji siyo maneno ikiwezekana watupe ratiba yao
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom