jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,989
- 22,521
Madai ya US na Israel kwamba Iran inatengeneza mabomu hayana "substantive evidence", kwa sababu Iran imesaini mkataba wa Nuclear Non-Proliferation Treaty na nuclear facilities zake ziko monitored na International Atomic Energy Agency (IAEA).
Wao IAEA wamekwishasema kwamba Iran inatengeneza nyuklia kwa ajili ya uzalishaji umeme tu na si vinginevyo kama ambavyo Uingereza na nchi zingine zilizoendelea zinavyotumia nyuklia kuzakisha umeme.
Kiini cha mgogoro huu ni "military supremacy" ambapo Israel inajaribu kuitawala Middle East na kuhakikisha hakuna kipingamizi hasa kutoka Iran.
Ni sababu tu za KWENDA VITANI KAMA ILIVYOKUWA KWA IRAKI KWANI NO WMD WAS FOUND!
Ila naona kweli kuna vita vinaweza kutokea kwasababu ya kauli mbili hadi sasa...
1)Wamarekani wametoa taarifa za YELLOW CAKE kuwa waliisafirisha kutoka Iraki..Na yellow cake ni ya kutengeneza Nyuklia...!
Hivyo ni kama njia nyingine ya ku justify vita ya IRAKI kwa mlango wa nyuma kwamba ni kweli walikuwa wakitengeneza Silaha za Maangamizi!
2)Obama alitoa kauli ya tofauti kuwa itabidi awasiklilize makamanda wa jeshi kabla hajayaondoa majeshi ya marekani kutoka Iraqi kwani naona sasa keshagundua kunaweza kuwa na vita nyingine dhidi ya IRAN na hataweza kuyaondoa majeshi mara moja kama mpango wake wa awali ulivyokuwa.
Na pia kauli zake sasa zinaendana na za Amiri jeshi mkuu wa Marekani na si kama ilivyokuwa kabla ambapo kauli za Amiri jeshi mkuu ziliendana na za Bush.
Na ndio maana Bush anataka kuwatumia waisraeli waivamie Iran baada ya mpango wake wa kulitumia jeshi la USA kuelekea kukwama kutokana na ushauri wa Makamanda wa jeshi kuwa haina haja ya vita kabla ya mazungumzo..Na Israel ni OPTION YAKE YA MWISHO kwani baada ya hapo watakuwa na haki ya kuingia vitani kumsaidia ALLY wao namba moja.
Kazi IPO!