Iran ni nchi ya kwanza duniani kwa kusambaza gesi maeneo mengi nchini

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Iran ni nchi ya kwanza duniani kwa kusambaza gesi maeneo mengi nchini

Jun 24, 2021 13:15 UTC

[https://media]

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran ni ya kwanza duniani kwa mafanikio ya kusambaza gesi katika kila kona ya nchi kwa ajili ya matumizi ya watu wake.

Rais Hassan Rouhani amesema hayo leo kwenye sherehe za kuzindua miradi ya taifa ya mafuta humu nchini zilizofanyika kwa njia ya video na kuongeza kuwa, kasi ya usambazaji gesi katika vijiji na miji ya Iran kwenye kipindi cha miaka minane iliyopita imeongezeka mara tano na sasa hivi Iran inahesabiwa ni nchi ya kwanza duniani katika jambo hilo.

Rais wa Rouhani amegusia pia juhudi za wataalamu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran za kufikisha na kudhamini gesi katika kila kona ya miji na vijiji humu nchini na kusisitiza tena kwa kusema, kiutaalamu na katika upande wa usambazaji gesi, mashirika ya kimataifa yanaitambua Iran kuwa ndiyo nchi ya kwanza duniani kwa kuwafikishia gesi ya matumizi wananchi wake walioko hata maeneo ya mbali ya miji na vijiji.

[https://media]Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepiga hatua kubwa katika utafutaji, uchimbaji na usambazaji wa gesi asilia



Miongoni mwa miradi ya taifa iliyozinduliwa leo na Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ni kukamilika zoezi la kufikishwa gesi kwenye miji 21, vijiji elfu mbili na 809 na maeneo 664 ya viwandani katika kona mbalimbali za Iran.

Miradi yote hiyo imefunguliwa rasmi na Rais Rouhani kwa njia ya video, leo Alkhamisi na imeanza kufanya kazi.
 
Back
Top Bottom