Iran kutotekeleza ahadi za mkataba wa nyuklia

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,402
Wizara ya mambo ya nje ya Iran imesema Jamhuri hiyo ya Kiislamu imeamua kusimamisha utekelezaji wa baadhi ya ahadi ilizotoa katika mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 iliyotia saini na mataifa yenye nguvu zaidi duniani.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Javad Zarif amesema hatua ambazo Marekani imechukua katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita baada ya kujiondoa kutoka kwenye mkataba huo na hata kabla kujiondoa, ni ishara ya wazi ya kuzuia kuendelea kuwepo kwa mkataba huo.

"Vifungu vya 26 na 36 vya mkataba wa nyuklia vimeipa Iran pamoja na nchi nyengine zilizotia saini uwezo wa kusimamisha utekelezaji wa ahadi zao kwa sehemu fulani au kikamilifu. Hii ni iwapo mojawapo ya nchi zitakataa kutekeleza ahadi zake. Kwa hiyo Iran haijakiuka chochote kwa kuchukua hatua hii," alisema Zarif.

Chini ya mkataba huo wa mwaka 2015 Iran iliondolewa baadhi ya vikwazo kwa masharti ya kusitisha uendelezaji wa mpango wake wa nyuklia. Baada ya Marekani kujiondoa kutoka kwenye mkataba huo ilivirejesha vikwazo kwa Iran, jambo lililochochea mzozo wa kiuchumi nchini humo kuwa mbaya zaidi.

Iran imetuma barua kuhusiana na uamuzi wake kwa viongozi wa Uingereza, China, Umoja wa Ulaya, Ufaransa na Ujerumani. Nchi zote hizo zilikuwa miongoni mwa nchi zilizotia saini mkataba huo na bado zinaendelea kuunga mkono. Barua moja pia itatumwa kwa Urusi.

Hakujakuwa na jawabu kutoka kwa Marekani ingawa Jumapili ilisema kwamba itatuma meli yenye uwezo wa kubeba ndege na silaha yenye uwezo wa kurusha makombora umbali mrefu katika ghuba ya Uajemi kutokana na kile ilichokielezea kama kitisho kipya kutoka kwa Iran.

China imesema mkataba huo wa nyuklia ni sharti uungwe mkono kikamilifu. Israel nayo kupitia kwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu imesema haitokubali kamwe Iran kuendelea na utengenezaji wa silaha za nyuklia.

Rais wa Iran Hassan Rouhani alisema Jumatano hawataziuzia tena nchi za nje, urani na maji ya kutengeneza silaha za nyuklia, kama ilivyoainishwa kwenye mkataba huo wa mwaka 2015. Rouhani ametoa muda wa mwisho wa siku sitini ili kupatikana kwa maelewano mapya katika mkataba huo.

Matamshi haya ya Rouhani yamekuja wakati umetimia mwaka mmoja kamili tangu Rais Donald Trump wa Marekani alipotangaza uamuzi wa kuiondoa Marekani kutoka kwenye mkataba huo.
 
SAFI SANA IRAN, MSIKUBALI, HAO NGURUE PORI MAREKANI WAACHENI WASUMBUKE, USIUZE TENA URANIUM YAKO NJE, ENDELEA KUTENGENEZA SABUNI YA ROHO UWACHIE MBWA WABWEKEBWEKE
 
Uchumi wa Iran umeanza kuyumba Kwa kasi ya ajabu.Tatixo Iran alianza kuichokonoa Israel ndio tatixo lilipoanzia
 
Ahhh, we nawe, kwani umeanza Leo?? Hio kutokuuza URANIUM ni ahadi tokea 2015 ndio wanaitekeleza leo, au umesahau
 
Kuna wakati baada ya US kujiondoa, wengine waliokuwa wamesign hiyo JCPOA walisema wangetengeneza mechanism ya kuilinda Iran, na makampuni Yao dhidi ya US na vikwazo. Kama hilo lingewezekana, nadhani ndo ungeanza kuwa no mwishoni wa ushawishi wa US na nguvu ya dollar kwenye biashara za dunia. Kilichotokea no tofauti, mpaka sasa hakuna mechanism yoyote, uchumi wa Iran unaripotiwa kushuka na hata zile harakati za washirika kujikita katika kuisaidia Iran dhidi ya vikwazo zimepoa Sana. Swali langu ni kuwa, je kama Iran akijitoa kwenye mkataba, ni madhara gani atayapeleka Kwa US? Na ni faida gani ataipata? Na ni Kwa nini Russia, Japan, EU & Co, zote Kwa pamoja wanaonekana kupoteza msimamo Kwa hili suala la Iran? Siku 60 siyo nyingi, huenda lolote likatukia
 
Wewe ndio umeongea point,,,kwanza hawa JCPOA wangesimamia mpango wao wangefaulu, lakini sasa shida ilikuja kwamba ' choose either to do business with Iran or with Us'woote wakala kona, nakwambia xku 60 zitaisha, iran itaendelea na vikwazo, na hata supply chochote, zaidi labda kama anataka kisingizio cha change regim...naona watu wengi wanajidanganya oooh iran ni strong sijui nini, hizo ni ngonjera kwa US,,,nakeambia zaidi ya Russia hamna mwingine anaweza mvimbia US hata china na ukubwa wake hawez thubutu
Kuna wakati baada ya US kujiondoa, wengine waliokuwa wamesign hiyo JCPOA walisema wangetengeneza mechanism ya kuilinda Iran, na makampuni Yao dhidi ya US na vikwazo. Kama hilo lingewezekana, nadhani ndo ungeanza kuwa no mwishoni wa ushawishi wa US na nguvu ya dollar kwenye biashara za dunia. Kilichotokea no tofauti, mpaka sasa hakuna mechanism yoyote, uchumi wa Iran unaripotiwa kushuka na hata zile harakati za washirika kujikita katika kuisaidia Iran dhidi ya vikwazo zimepoa Sana. Swali langu ni kuwa, je kama Iran akijitoa kwenye mkataba, ni madhara gani atayapeleka Kwa US? Na ni faida gani ataipata? Na ni Kwa nini Russia, Japan, EU & Co, zote Kwa pamoja wanaonekana kupoteza msimamo Kwa hili suala la Iran? Siku 60 siyo nyingi, huenda lolote likatukia
 
Kuna wakati baada ya US kujiondoa, wengine waliokuwa wamesign hiyo JCPOA walisema wangetengeneza mechanism ya kuilinda Iran, na makampuni Yao dhidi ya US na vikwazo. Kama hilo lingewezekana, nadhani ndo ungeanza kuwa no mwishoni wa ushawishi wa US na nguvu ya dollar kwenye biashara za dunia. Kilichotokea no tofauti, mpaka sasa hakuna mechanism yoyote, uchumi wa Iran unaripotiwa kushuka na hata zile harakati za washirika kujikita katika kuisaidia Iran dhidi ya vikwazo zimepoa Sana. Swali langu ni kuwa, je kama Iran akijitoa kwenye mkataba, ni madhara gani atayapeleka Kwa US? Na ni faida gani ataipata? Na ni Kwa nini Russia, Japan, EU & Co, zote Kwa pamoja wanaonekana kupoteza msimamo Kwa hili suala la Iran? Siku 60 siyo nyingi, huenda lolote likatukia
Marekani atahathirika pakubwa sana iwapo Iran atafanikiwa kutengeneza Silaa za kinyukilia kwa sababu haitadhibitika tena.Nina Sema hivyo kwa sababu Iran ifanikiwa kumiliki salaa hizo kiburi atakacho kuwa nacho hata kiduku akasome,kwa hiyo ununapoiona Marekani ana haha kila kukicha kuibana Iran usidhani marekani anafanya kitu ambacho hakijui.Nina kuhakikishia Iran akifanikiwa kumiliki nyukilia maadui zake watapata tabu sana ikiwemo USA kwa sababu Iran itafanya inavyo taka na hakuna atakaye thubutu kukoroma.
 
Ni kweli mkuu, tena akishafanikiwa kuwa nayo hiyo Nuclear kiburi atakawa nacho ni kikubwa mno.

Na mwisho wa siku akija kukomalia kulifunga lile lango la Hormoz, sijui ka ma kuna mpuuzi atakae tia pua yake kibabe maeneo hayo.
Marekani atahathirika pakubwa sana iwapo Iran atafanikiwa kutengeneza Silaa za kinyukilia kwa sababu haitadhibitika tena.Nina Sema hivyo kwa sababu Iran ifanikiwa kumiliki salaa hizo kiburi atakacho kuwa nacho hata kiduku akasome,kwa hiyo ununapoiona Marekani ana haha kila kukicha kuibana Iran usidhani marekani anafanya kitu ambacho hakijui.Nina kuhakikishia Iran akifanikiwa kumiliki nyukilia maadui zake watapata tabu sana ikiwemo USA kwa sababu Iran itafanya inavyo taka na hakuna atakaye thubutu kukoroma.
 
And ninani hasa atamruhusu atengeneze hio nuclear???

Tatizo sio kumzuia ila tatizo lina kuja itumike njia gani kumzuia?njia pekee ya vikwazo haiwezi kulizuia taifa lolote kufanya inacho kitaka , na mfano mzuri tumeuona kwa kiduku licha ya vikwazo lakini Silaa walizitengeneza.
Mfano mwingine ni Urusi iliwekewa zikwazo na marekani na ulaya kwa kulichukua eneo la crimea,lakini licha ya vikwazo ambavyo viliiyumbisha Urusi kiuchumi bado mpaka sasa Cremea inashikiliwa na Urusi na hana mpango wa kulirudisha,na mifano mingi tu kama Cuba.
Nimetoa mfano hiyo kukuonesha ya kwamba njia ya kuizuia Iran isitengeneze hizo silaa ni kuishambulia kijeshi,chaguo ambalo ni ngumu muno kwa marekani na washilika wake.
Chaguo haliwi gumu kwa sababu labda eti marekani inaofia kushidwa vita hapana,bali ni madhara gani yataikumba mashariki ya kati na dunia kwa ujumla?
Tukubali tukatae Iran ina uwezo makubwa sana wa kijeshi ukilinganisha na nchi nyingi hapo mashariki kati,
shirika la BBC kama sikosei ilikuwa mwaka Jana walikuwa wana uchambua uwezo wa kijeshi wa Iran,wana kwambia Iran ndio taifa pekee pale mshariki ya kati lenye shehena kubwa sana ya makombora ya Masafa marefu yenye uwezo kupiga eneo lolote lile ndani ya mashariki ya kati na Ulaya.
Lakini tatizo lingine vita ikianza lango la kupitishia mafuta la uajemi litafungwa kwa kuhofia usalama wa meli za mafuta, na 35% ya mafuta inayo tumika duniani yana pita eneo hilo ,
wataalam wa masuala ya kiuchumi wanasema eneo hill likifungwa ndani ya Siku tatu mafuta yata panda kiasi kwamba pipa moja litauzwa kuazia $450 mpaka $500 sasa hebu tujiulize mimi na wewe kwa hapa tz Lita moja itanunuliwaje?
Kwa hiyo madhara ya hiyo vita hata mimi na wewe ni lazima yatukute,kwa sababu ya kila kitu kipanda sana kuanzia bidhaa za viwandani ,umeme,usafiri.
 
Back
Top Bottom