IRAN: Kitendo chochote cha kishetani cha Israel kitapewa jibu kali na muafaka

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Kamanda Salami: Kitendo chochote cha kishetani cha Israel kitapewa jibu kali na muafaka.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (Sepah) amesema kuwa, harakati za utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo la Magharibi mwa Asia zitakuwa na matokeo kinyume na ilivyokusudiwa na Iran itajibu kitendo chochote cha kishetani cha Israel katika daraja hiyo hiyo lakini kwa nguvu kubwa zaidi.

Brigedia Jenerali Hossein Salami amesema kuwa vitendo viovu vya Wazayuni katika kanda ya Magharibi mwa Asia vitakuwa na matokeo kinyume na malengo yao na vitawafanya wakabiliwe na hatari halisi katika siku za usoni.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, iwapo Wazayuni wa Israel wataendelea kufanya jinai watakaribia zaidi katika mproroko na kusambaratika, hasa ikitiliwa maanani kwamba, mazingira yote ya kusambaratika utawala huo yako tayari.

Brigedia Jenerali Hossein Salami amesema kuwa, tumeona jinsi vitendo vyao viovu vya siku kadhaa zilizopita vilivyopata jibu mwafaka na matokeo mengine yaliyojiri katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel); na tunaamini kwamba, matukio hayo yanaweza kukaririwa au kushadidi zaidi katika siku zijazo.

4bn2c1682cc6bdws9j_800C450.jpeg
 
Hii geresha bwege sijui itaisha lini?

Iran na Israel, Lao ni moja, kuwachafua Waarabu kwa namna yoyote ile.
 
Mbona unateseka sana? Wapigane wao, damu utoke wewe. Inashangaza sana. Hao hawakuongezei kitu chochote kwenye maisha yako
 
Kamanda Salami: Kitendo chochote cha kishetani cha Israel kitapewa jibu kali na muafaka.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (Sepah) amesema kuwa, harakati za utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo la Magharibi mwa Asia zitakuwa na matokeo kinyume na ilivyokusudiwa na Iran itajibu kitendo chochote cha kishetani cha Israel katika daraja hiyo hiyo lakini kwa nguvu kubwa zaidi.

Brigedia Jenerali Hossein Salami amesema kuwa vitendo viovu vya Wazayuni katika kanda ya Magharibi mwa Asia vitakuwa na matokeo kinyume na malengo yao na vitawafanya wakabiliwe na hatari halisi katika siku za usoni.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, iwapo Wazayuni wa Israel wataendelea kufanya jinai watakaribia zaidi katika mproroko na kusambaratika, hasa ikitiliwa maanani kwamba, mazingira yote ya kusambaratika utawala huo yako tayari.

Brigedia Jenerali Hossein Salami amesema kuwa, tumeona jinsi vitendo vyao viovu vya siku kadhaa zilizopita vilivyopata jibu mwafaka na matokeo mengine yaliyojiri katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel); na tunaamini kwamba, matukio hayo yanaweza kukaririwa au kushadidi zaidi katika siku zijazo.

View attachment 1766771
Umejichagulia kuishi kwa stress
 
Iran Maneno maneno afu utasikia washapigwa pwaaa wakiuguza maumivu wanapiga tena Mikwara... ndio mwendo huo huo daily
 
Wazichape tu tuone mbabe ni nani. Hii mikwara ya miaka na miaka haina maana.

Tena wazipige "kavu kavu", wasitumie silaha za "nyuklia"!

Nakumbuka tambo za Saddam, Muamar Gaddaf na wengine....kumbe "hamna" kitu!
 
Back
Top Bottom