Iran inakaribia kuwa mzalishaji na muuzaji wa chanjo nje hivi karibuni

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Namaki: Iran inakaribia kuwa kitovu kikuu cha uzalishaji na uuzaji nje chanjo

Waziri wa Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu wa Iran ametangaza kuwa: Hadi kufikia msimu ujao wa machipuo Iran itakuwa moja ya kambi kubwa za kuzalisha na kuunza nje chanjo duniani.

Saeed Namaki amesema pambizoni mwa mazungumzo yake na viongozi wa juu wa kidini katika mji mtakatifu wa Qum kwamba: maendeleo ya wasomi wa nchi hii katika kutengeneza wa chanjo ya Kiirani ni makubwa na ya kujivunia na kwamba siku chache zijazo si tu Iran itajitosheleza katika kutengeneza wa chanjo, bali pia itakuwa moja ya nchi wazalishaji wa chanjo za aina mbalimbali.

Namaki ameongeza kuwa, licha ya vikwazo vyote vilivyopo na mazingira ya sasa ya corona lakini Iran imekuwa na mafanikio makubwa katika kutengeneza dawa na suhula za tiba kwa kadiri kwamba, mwaka huu pekee tumeokoa dola bilioni moja. Amesema Iran imeuza barakoa nyingi na mashine za kusaidia kupumua (ventilators) katika nchi mbalimbali.

Mashine za kusaidia kupumua (Ventilators) zinazotengenezwa hapa nchini Iran

Wakati huo huo Waziri wa Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu wa Iran amesema maambukizi ya corona yamedhibitiwa hapa nchini na kwamba: Licha ya kuenea kirusi cha corona ya Uingereza lakini wafanyakazi wa sekta ya afya wameanzisha ufuatiliaji wa nyumba kwa nyumba kote nchini na leo hii idadi ya sampuli za vipimo zinafika zaidi ya laki moja kwa siku kutoka elfu kumi.

Ventilators made in Iran

My take:Hawa viumbe sio aisee wairan ni noma, sijui tunakwama wapi kwanini tusiagize chanjo kutoka kwao?​

4bxyb1dc54c7991ttk5_800C450.jpeg
 
Nani atainunua hiyo chanjo kwenye ulimwengu wa mabeberu? Wao ndio wanapanga nani auze nini Nani auze nini
Hapo kwenye chanjo ni matakwa tu ya nchi husika..........labda kwa wale wanaosubiri chanjo za msaada ndo watapangiwa
 
Back
Top Bottom