Iran imetangaza kutumia mashine za hali ya juu kurutubisha madini yake ya Urani

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,442
3,353
Iran imethibitisha itatumia mashine za kisasa zaidi kurutubisha madini yake ya urani katika awamu ya tatu ya kujiondoa kwenye mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 kati yake na mataifa yenye nguvu duniani.

Msemaji wa shirika la nguvu za atomiki la Iran Behrouz Kamalvandi, ameuambia mkutano wa waandishi habari hii leo kuwa licha ya kujiondoa polepole katika mkataba huo bado nchi yake itaruhusu Jamii ya Kimataifa kufuatilia kazi zake.

Kaimu mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomiki ( IAEA ) Cornel Feruta anatarajiwa kuwasili nchini Iran hii leo Jumamosi kukutana na viongozi wa ngazi ya juu kujadili suala hilo.

Tangazo la shirika la nguvu za atomiki la Iran litaipa nafasi nchi hiyo kuharakisha mchakato wa urutubishaji wa madini yake kwa kiwango cha asilimia 20.

Kwa upande wake, Marekani imesema haishangazwi kuwa Iran inaanzisha mashine mpya za nyuklia.
 
Watu ukiwaeleza yakwamba US Walichemka kwahawa wajamaa since 1979 ile hawaelewi

Yaani walitakiwa wamdhibiti pale pape asee ila wakachelewa

Samaki Mkunje Angali Mbichi Bana


IRAN TAIFA TEULE
Ile ID yako nyingine umeipotezea leo
 
Back
Top Bottom