Iran iliwakomesha mabeberu kwa kutaifisha sekta zote za mafuta. Je, kwanini tusitaifishe sekta zote za madini na sisi tuwatimuwe mabeberu?

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,839
17,437
Kutaifishwa Sekta ya Mafuta Iran
Mar 20, 2019 18:38 UTC

Tarehe 29 mwezi Esfand kwa kalenda ya Hijria Shamsia sawa na Machi 20 huadhimishwa kila mwaka kama siku kukumbuka kutaifishwa sekta ya mafuta ya petroli nchini Iran.

Siku hii ni muhimu sana katika historia ya kisiasa na kiuchumi ya Iran. Utaifishwaji wa sekta ya mafuta Iran ulifanikiwa baada ya mapambano magumu sana na ukawa mwanzo wa fikra ya "Uchumi bila Mafuta'. Karibuni kusikiliza makala maalumu kwa munasaba huu.

Ili kuweza kufahamu na kudiriki umuhimu wa siku ya kutaifishwa sekta ya mafuta Iran, tunapaswa kuangazia historia kwa kifupi ili tuweze kuona namna ambavyo madola makubwa ya kibeberu yalivyoanza kupora mafuta ya petroli ambayo ni utajiri mkubwa wa taifa la Iran.

Waliogundua mafuta kwa mara ya kwanza Iran walifahamu vyema kuwa, mafuta, yaani dhahabu nyeusi, itakuwa dhamana kwa maslahi na satwa yao ya kiuchumi na kiviwanda duniani kwa karne kadhaa.

Nchi za kiviwanda zilifahamu vyema kuwa, ili uchumi wao uweze kustawi ipasavyo zilikuwa zinahitajia mafuuta na iwapo hazingeweza kudhibiti vyanzo vya mafuta, basi zingelazimika kizinyenyekea nchi zenye utajiri huo.

Fikra hiyo iliweka msingi wa ubeberu wa mafuta na nyaraka kuhusu suala hizo zinapatikana katika majumba ya makumbusho ya historia ya mafuta ya nchi zinazozalisha mali ghafi hiyo muhimu ikiwemo Iran.

Nyaraka hizo zinaonyesha aina mbali mbali ya mikataba ya kibeberu ya uchimbaji, uzalishaji na uuzaji wa mafuta ghafi ya petroli.

Ni kwa msingi huo ndio tunaweza kubaini chanzo cha harakati ya kutaifishwa sekta ya mafuta ya Iran ambayo chimbuko lake ni mkataba wa mafuta ya petroli ya Iran ambao ulianza mwaka 1870.

Moja ya mikataba ya kushangaza zaidi ulikuwa mkataba baina ya serikali ya Iran na Baron Julius de Reuter. Kwa mujibu wa mkataba huo shirika moja la kigeni lilipata haki ya miaka 70 ya kumiliki na kutumia misitu, mito, madini ya mkaa wa mawe, chuma, shaba, madini ya risasi, mafuta ya petroli n.k. Haki ya Iran baada ya kuchimbwa madini au mafuta ilikuwa asilimia 15 tu.

Mkataba huu ulikuwa wa kushangaza sana kiasi kwamba hata Lord Curzon mmoja kati ya wanasiasa mashuhuri wa Uingereza na ambaye alikuwa kati ya waanzilishi wa sera za kibeberu za nchi hiyo alisema hivi kuhusu mkataba huo: "Kukabidhi vyanzo vyote vya kiviwanda vya nchi kwa dola la kigeni ni jambo la ajabu na urafiki wa karibu wa Uingereza na Iran haujawahi kufikia kiwango hiki."

Katika Mkataba baina ya serikali ya Iran na Baron Julius de Reuter, kipengee cha 11 kilisema hivi: "Petroli ambayo ina umuhimu mkubwa itakuwa sawa na mkaa wa mawe, shaba na madini ya risasi." Miaka 30 baadaye yaani mwaka 1902, watawala wa wakati huo wa Iran walilipatia shirika lingine la Uingereza haki ya muda wa miaka sitini kutafuta, kuchimba, kuzalisha na kuuza mafuta ya petroli katika maeneo yote ndani ya Iran isipokuwa maeneo ya kaskazini.

Mkataba huo ulitiwa saini kati ya Iran na Muingereza William Knox D'Arcy. Hisa ya Iran katika mkataba huu ilikuwa ni asilimia 16 tu. Cha kushangaza ni kuwa, pamoja na kuwa faida ya Iran ilikuwa ndogo sana lakini pia hawakuwa tayari kulipa kiasi hicho kidogo na hivyo shirika hilo la Uingereza lilipata faida kubwa sana katika shughuli zake za uchimbaji mafuata nchini.

Uporaji huu wa utajiri wa Iran ulipelekea kuibuka mwamko wa kisiasa na kijamii. Baada ya kukaliwa kwa mabavu Iran na Uingereza kisha Shirikisho la Sovieti na baadaye Marekani baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, mashindano ya madola ya kibeberu kuhusu maslahi yao nchini hasa mafuta yalishadidi.

Serikali ya Uingereza ilikuwa ikitaka kulinda satwa yake katika sekta ya mafuta kusini mwa Iran na kwa msingi huo ikatia saini mkataba mwingine na Iran mwaka 1933.

Mkataba huo ulilalamikiwa vikali na wananchi wa matabaka mbali mbali haswa Ayatullah Kashani ambaye alikuwa akihesabiwa kuwa mmoja kati ya wanazuoni wanamapambano katika bunge la Iran wakati huo na aliweza kufichua namna mabebeu waliovyokuwa wakipora mafuta ya Iran.

Fatima Amini, mtaalamu wa historia ya Mapinduzi ya Kiislamu anasema:
Nyaraka za kihistoria katika zama hizo zinaonyesha Ayatullah Kashani alikuwa na nafasi kubwa sana katika harakati ya kupigania kutaifishwa sekta ya mafuta ya Iran na aliweza kutetea haki za taifa hili na akaweza kuandaa mazingira ya taifa kudhibiti nishati hii ambayo ni neema kwa Iran kutoka kwa Mwneyezi Mungu."

Katika kuendeleza harakati yake, Ayatullah Kashani aliuandikia barua Umoja wa Mataifa akibainisha kutokuwa na itibari mkataba uliotiwa saini baina ya utawala na wakati huo wa kifalme na ubia wa mashirika ya Uingereza.

Aliutaja ubia huo kuwa wa kidhalimu na hapo serikali ya Uingereza ilianzisha njama za kubadilisha hali ya mambo kwa maslahi yake na kwa msingi huo, Ayatullah Kashani, alikamatwa na vibaraka wa mtawala Shah na kisha akapelekwa huko Kerman Shah na baadaye akabaidishiwa nchini Lebanon.

Harakati za kutaka sekta ya mafuta ya Iran itaifishwe ili nchi ifaidike na mali asili yake hiyo ziliendelea na Waziri Mkuu wa Wakati huo Dakta Mohammad Mossadeq alidumisha harakati hiyo.

Hatimaye tarehe 29 Isfand mwaka 1329 Hijria Shamsia sawa na Machi 20 1950, sekta ya mafuta Iran ilitaifishwa rasmi baada ya muswada kuidhinishwa katika Majlisi.

Kutaifishwa sekta ya mafuta ya Iran hakukumaanisha kumalizika njama za Uingereza dhidi ya taifa hili. Baada ya kupoteza satwa na ushawishi wao haramu katika sehemu kubwa ya mafuta ya Mashariki ya Kati (Asia Magharibi) mababeru walianzisha njama mpya dhidi ya Iran.

Ni kwa msingi huo ndio maana mwaka 1953 madola ya kibeberu ya Uingereza na Marekani yakashirikiana katika njama ya kuipindua serikali ya wakati huo ya waziri mkuu wa Iran Mohammad Mosaddegh. Baada ya mapinduzi hayo ya serikali, mashirika mengi ya Marekani na Uingereza yaliingia Iran kupora mafuta ya nchi hii chini ya ubia mpya.

Ubia huo uliundwa na mashirika kama vile Shell Petroleum, Gulf Oil, Mobile Oil, Standard Oil, Oil Company of California, Texas Oil n.k.

Ingawa sheria ya kutaifishwa sekta ya mafuta ilikuwa inatekelezwa lakini kivitendo serikali ya Iran ilikuwa na ushawishi mdogo sana katika Shirika la Kitaifa la Mafuta.

Hiyo ndiyo iliyokuwa hatima ya sekta ya mafuta ya Iran baada ya kutaifishwa. Kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979, sekta ya mafuta Iran ilikuwa mikononi mwa madola ajinabi.

Kutokana na kuwa nchi imekuwa tegemezi sana kwa mafuta, mali ghafi hiyo imeendelea kutumiwa kama chanzo cha kuishinikiza na kuiwekea vikwazo Iran na hiyo ni hasara kwa maslahi ya taifa la Iran.

Ni kwa msingi huo ndio kupunguzwa utegemezi wa sekta ya mafuta likawa jambo la lazima ambalo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameliashiria mara kadhaa katika kubainisha vigezo vya uchumi wa kimapambano ambapo amenasihi kwa kusema: "Utegemezi huu ni turathi chungu ya miaka 100."

Uchunguzi uliofanywa katika nchi ambazo mafuta ya petroli au mali ghafi mshabaha ni chanzo kikuu cha pato umeonyesha kuwa, pato la uuzaji wa bidhaa hiyo hutumiwa vibaya.

Uchunguzi unaonyesha kuwa, ongezeko la bei ya mafuta duniani hupelekea nchi ambazo zinategemea fedha za mali ghafi hiyo kuwa dhaifu katika uzalishaji wa bidhaa ndani ya nchi.

Aidha bei ya nyumba na ardhi nayo huongezeka na nchi hizo hudorora katika mfumo wa ukusanyaji ushuru. Hali kadhalika nchi hizo huwa hazina motisha wa kuwashirikisha wananchi katika masuala ya kiuchumi na hivyo utegemezi kwa pato la mafuta huongezeka.

Haya ni madhara ambayo yamezikumba nchi zenye utajiri wa mafuta ikiwemo Iran na ni kwa msingi huo ndio mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ukatangaza azma yake ya kuacha kutegemea uuzaji mafuta ya petroli kama chanzo kikuu cha pato la mafuta na badala yake pato liwe sehemu tu ya pato katika uchumi wa kimapambano.
Tags
IRAN MAFUTA

Jee sisi tunaweza kutaifisha sekta zote za madini na kuwatimua mabeberu???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana mku umetupa hiyo historia ya wenzetu, sisi Tz unatushauri nini?
 
Spika wa Bunge la Iran Na PM wao nao waige wenzao wa Tanzania kugombea kupiga Picha Na Piere wao!
 
Yanayotokea S.A ni fikra za kutaifisha.
Sisi wawekezaju tunashea nao mambo mengi sana na tunanufaika na zaidi kijamii.
Mfano wawekezaji wengi wa vituo vya mafuta ni ndugu zetu kiimani .
Wawekezaji wengi kwenye madini ni ndugu zetu kiimani.

Irani ikimfukuza mzungu ujue nyuma yake kuna suala la imani pia kwa hiyo wataungana mkono liwake jua inyeshe mvua.

Beberu aliyeko Afrika ni mwafrika mwenyewe.

Kuna waafrika wanaolalia madola majumbani kwa kuziibia nchi zao wanapokua nadarakani
Tuanze na hao mana wametumia madara tuliyowapa kutuibia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la Tz, mwekezaji analetwa na dalali ambaye anakuwa mtawala wa Serikalini.

Tatizo likitokea unapotoka kufanya maamuzi, unapata Upinzani kutoka hapa hapa kabla hata hujamfikia mabeberu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa kutupa historia lakini kwa dunia ya leo hatuna ujanja wa kuwafukuza wawekezaji,
Kumbuka kuwa wazungu walifanya amendments nyingi hapa karibuni ili kuepuka visa kama vya Iran.TANZANIA haina ujanja wa kuwafukuza wazungu.

Babu yako magufuli anawakaribisha mabeberu kila siku waje kuwekeza iweje wwe lofa wa lumumba uwakatae??
 
Yanayotokea S.A ni fikra za kutaifisha.
Sisi wawekezaju tunashea nao mambo mengi sana na tunanufaika na zaidi kijamii.
Mfano wawekezaji wengi wa vituo vya mafuta ni ndugu zetu kiimani .
Wawekezaji wengi kwenye madini ni ndugu zetu kiimani.

Irani ikimfukuza mzungu ujue nyuma yake kuna suala la imani pia kwa hiyo wataungana mkono liwake jua inyeshe mvua.

Beberu aliyeko Afrika ni mwafrika mwenyewe.

Kuna waafrika wanaolalia madola majumbani kwa kuziibia nchi zao wanapokua nadarakani
Tuanze na hao mana wametumia madara tuliyowapa kutuibia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli lakini kusema kweli kwa iran kumfukuza mwingereza eti kwasababu sio ndugu yao kiimani sio kweli kunyonywa kupo tu hata angekua ni mwarabu anamnyonya mwiran wangemtimua tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa kutupa historia lakini kwa dunia ya leo hatuna ujanja wa kuwafukuza wawekezaji,
Kumbuka kuwa wazungu walifanya amendments nyingi hapa karibuni ili kuepuka visa kama vya Iran.TANZANIA haina ujanja wa kuwafukuza wazungu.

Babu yako magufuli anawakaribisha mabeberu kila siku waje kuwekeza iweje wwe lofa wa lumumba uwakatae??
Mkuu lumumba watapinga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli lakini kusema kweli kwa iran kumfukuza mwingereza eti kwasababu sio ndugu yao kiimani sio kweli kunyonywa kupo tu hata angekua ni mwarabu anamnyonya mwiran wangemtimua tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kule hata angeamua kuwapiga risasi wote aliyefanya hivyo angepata sapoti kubwa ya ndani.

Kwetu mfano nani asiyeona misaada mikubwa tunayopata toka kwa nchi za kiislam (kiarabu ) Au Vatican.
Hivi unweza kwenda kuchukua maeneo ya Kanisa la Roma ambayo ni makubwa kabisa kwa sababu eti hawalipi kodi.
Unasahau misaada mikubwa ya kielimu na afya tunayopata.
Scholar ship nyingi wanazotoa kwa watanzania wenzetu n.k.
Mwingiliano huo unabalance kwetu.
Kwa taarifa yako hakuna MTU anayetoka nje na kuja kutuibia bila kushirikiana na watawala.
Na watawala wanapotaifisha Mara nyingi ni kwa faida yao.

Nchi Tajiri Duniani kama Quatar, Falme za Kiarabu,Saudi Arabia, Quwait, Brunei,Korea ya Kusini, Japani,China n.k.Zote zina wawekezaji na watu wanakula hata.
Maisha ni kuishi kwa raha. Sio hadithi za watu kuwatesa wengine huku wao wakila bata.
Mfano tu Hapa Afrika : Pesa zote zinazokusanywa kama kodi asilimia kubwa zinatumiwa kwenye shughuli za Utawala. Kundi la watawala linatumia Asilimia kubwa ya pato la nchi. Kidogo linaenda kwenye Miundo mbinu ambayo hata hivyo wao ndio watumiaji namba moja. Kidogo sana wanawaziba watu midomo kwa kuwapa baadhi ya huduma bure ili watu wasijue kinachoendelea.
Mtalipa kodi, na kila aina ya ushuru ili watawala wasipate shida. Muda wote wao wanatembea na mabegi ya pesa wakati wananchi hata mia mfukoni hawana ,halafu unasema eti Waingereza.
Kwenye Bajeti ya nchi zioni Mwingereza akilipwa mishahara 20 hewa, au cheti hewa cha Digrii.
Ni waafrika wenyewe.
Siku tutakapojua kuwa Wazungu na waarabu ni ndugu zetu tunaotakiwa kujifunza kwao na sio adui wa kufikirika ndio tutakapoanza kutatua matatizo yetu wenyewe.

Hivi Foleni ya Ubungo kwa mipaka nenda rudi ilikua inasababishwa na mabeberu au ni uroho wa watu kujitafutia manunuzi ua taa yasiyo na tija?

Miaka yote chuo cha Isafirishaji wanafundisha kuwa round abut inapunguza Foleni kwa zaidi ya 70% ukilinganisha na taa lakina hakuna mtu aliyechukua toka kwenye kitabu na kulifanya kazi mpaka alipokuja mchina ambaye amelitoa kitabuni pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: RTI

Nimesoma point yako nimesisimka mnoo kweli aisee asilimia kubwa ya bajeti zinalipa madeni na kulipa watumishi wa serikali ambao hata 1% ya nchi hawafiki

Tukija kwenye ufisadi ndo usiseme pesa mpaka imfikie mwananchi ishadonolewa wee daah africa tuna shida sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
baada ya azimio la Arusha tulisha jaribu hako kamchezo, matokeo yake sote tunayajua.
 
Basically the article lacks historical facts on commercialization of oil and gas sector, the evolution of the industry, Iran politics, middle east politics in general and the western role (philosophical approach in Oil and Gas)

In short wakati seven sisters (hayo makampuni tajwa yaki beberu yanaenda kusign mikataba) waarabu walikuwa clueless yanakazi gani huko na sehemu yenyewe ilikuwa jangwa tu. Faida walizokuwa wanapata wenzao walikuja kugundua kupitia thamani ya hizo kampuni via market share zao, na ndipo mzozo ulipoanza wa ku share faida.

Kilichopelekea Iran kutaifisha kabisa British Petroleum iligoma, kubadili mkataba wake wa kinyonyaji (well UK was broke after the II WW na wasingeweza poteza mapato kirahisi).

Its a long story but this article is short of facts, hakuna dini bali ni biashara (1950's) zilizoshape agenda ya kuangalia mikataba, siasa za Israel (Especially baada ya vita 1973 kati ya waarabu na Israel mafuta ndio kwa mara ya kwanza yalitumia kama silaha), sababu za kuanzisha IEA 1975, Maamuzi ya Ayatollah Komein ya 1979 yaliyochochea mgogoro wa Sunni na Shia in middle east, Tanker war 1980's.

Bila ya kurudi nyuma kwenye zama za 'standard oil', umuhimu wa Carl Benz kwenye sector, improvement ya refining na matumizi mengine ya oil by products (muda wote huo waarabu walikuwa sio wachezaji). Historia yao kwenye commercialization inaanzia 1930's ukielewa mapitio hayo utapata picha ya tabia ya Iran leo kisiasa.
 
Mabeberu wamehamia kufanya biashara za usafishaji wa mafuta ghafi na kuuza rejareja ambayo bado ni ya faida kubwa kwao, wanawaacha waarabu wachimbe wenyewe wao wanayanunua kwa bia rahisi,Total na Shell zimetapakaa dunia yote .Endeleeni na hadithi zenu za Abunuwasi na utaifishaji.
 
Basically the article lacks historical facts on commercialization of oil and gas sector, the evolution of the industry, Iran politics, middle east politics in general and the western role (philosophical approach in Oil and Gas)

In short wakati seven sisters (hayo makampuni tajwa yaki beberu yanaenda kusign mikataba) waarabu walikuwa clueless yanakazi gani huko na sehemu yenyewe ilikuwa jangwa tu. Faida walizokuwa wanapata wenzao walikuja kugundua kupitia thamani ya hizo kampuni via market share zao, na ndipo mzozo ulipoanza wa ku share faida.

Kilichopelekea Iran kutaifisha kabisa British Petroleum iligoma, kubadili mkataba wake wa kinyonyaji (well UK was broke after the II WW na wasingeweza poteza mapato kirahisi).

Its a long story but this article is short of facts, hakuna dini bali ni biashara (1950's) zilizoshape agenda ya kuangalia mikataba, siasa za Israel (Especially baada ya vita 1973 kati ya waarabu na Israel mafuta ndio kwa mara ya kwanza yalitumia kama silaha), sababu za kuanzisha IEA 1975, Maamuzi ya Ayatollah Komein ya 1979 yaliyochochea mgogoro wa Sunni na Shia in middle east, Tank wars 1980.

Bila ya kurudi nyuma kwenye zama za 'standard oil', umuhimu wa Carl Benza kwenye sector, improvement ya refining na matumizi mengine ya oil by products (muda wote huo waarabu walikuwa sio wachezaji). Historia yao kwenye commercialization inaanzia 1930's ukielewa mapitio hayo utapata picha ya tabia ya Iran leo kisiasa.
Fact

Sent using Jamii Forums mobile app
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom