Iran haitaki ugomvi waendelea na ujenzi wa malaki ya nyumba

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Rouhani: Iran haitaki ugomvi na nchi za dunia
Aug 27, 2019 11:58 UTC
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran haitaki ugomvi bali inachopigania ni usalama wa kieneo na kimataifa na vile vile kushirikiana vizuri na nchi rafiki.
Rais Rouhani amesema hayo leo kwenye sherehe za kuanza ujenzi wa nyumba laki moja na elfu 10 za raia hapa Tehran na kusisitiza kuwa hakuna nchi yoyote inayoweza kuitweza nguvu Iran. Ameongeza kuwa, wale walioliwekea vikwazo na kulifanyia taifa la Iran ugaidi wa kiuchumi, wanapaswa kujirekebisha na kuachana na njia batili wanayoifuata na badala yake watekeleze ahadi zao na kutambua rasmi haki za taifa la Iran kwa heshima.
Amesisitiza kuwa, kamwe hakuna mabadiliko yoyote yatakayotokea katika uhusiano wa Iran na Marekani hadi pale Washington itakapoondoa vikwazo na kuachana na chuki zake dhidi ya taifa la Iran.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vile vile amegusia madai yasiyo na mashiko ya Marekani ya kwamba eti Iran inataka kumiliki silaha za nyuklia na kusisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haina nia yoyote ya kumiliki silaha za nyuklia kwani fikra na mfumo wa kiulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu hautegemei kabisa silaha zisizokubalika.
Amesema, siasa za Iran hazikusimama juu ya msingi wa kuwaogopa maadui, bali zinategemea itikadi, maadili na fatwa ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Rais Rouhani amezungumzia pia mchakato wa mazungumzo baina ya Iran na pande zilizobakia katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kusisitiza kuwa, kama pande hizo hazitotekeleza ahadi zao, Iran nayo haitoheshimu ahadi zake.
Tags
ROUHANI
 
Back
Top Bottom