Iramba wanunua kifaa cha kisasa cha upimaji ardhi na urasimishaji makazi

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
320
412
Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida Mhe Suleiman Yusuph Mwenda siku ya Septemba 23, 2021 amezindua kifaa cha kisasa cha upimaji wa ardhi kiitwacho DGPS S86 RTK chenye uwezo wa kutembea Km 30. Akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa kifaa hicho, Mhe Mwenda aliwapongeza kwa pamoja Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iramba Mhe Innocent Msengi na Mkurugenzi Mtendaji wake Mhandisi Michael Matomora kwa kufanikisha kununua mitambo hiyo ya kisasa ya upimaji ardhi aina ya DPGS S86 RTK inayotumia teknolojia ya Real Time Kinematics.

Mhe Mwenda alisema Wilaya ya Iramba imekuwa ya kwanza katika mikoa ya Kanda ya Kati kununua kifaa hicho ambacho kilikuwa kinahitajika sana Iramba ili kutambua ardhi, kupanga, kupima na kurasimisha ardhi kwa matumizi bora wilayani Iramba na kwamba wametekeleza vyema maagizo ya Ilani ya CCM kununua kifaa hicho tena kwa fedha za wananchi wenyewe.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Iramba alisema kifaa hicho ambacho kimenunuliwa kwa fedha za wananchi wenyewe kitasaidia suala la kupima ardhi kama inavyoagiza sera ya CCM na kwamba wakati anateuliwa jukumu mojawapo aliloagiza Mhe Rais Samia ni kuhakikisha ardhi ya Iramba inapimwa na wamenunua kifaa hicho ili kutekeleza agizo hilo la Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.

#IrambaKaziInaendelea.

IMG-20210925-WA0022.jpg

IMG-20210925-WA0023.jpg

IMG-20210925-WA0024.jpg

IMG-20210925-WA0021.jpg

IMG-20210925-WA0017.jpg

IMG-20210925-WA0018.jpg

IMG-20210925-WA0019.jpg

IMG-20210925-WA0014.jpg

IMG-20210925-WA0015.jpg

IMG-20210925-WA0012.jpg

IMG-20210925-WA0011.jpg

IMG-20210925-WA0013.jpg

IMG-20210925-WA0016.jpg

IMG-20210925-WA0020.jpg
 

Attachments

  • VID-20210925-WA0010.mp4
    13.2 MB
hivi vyombo/vifaa huku maeneo ya kwetu vinamilikiwa na vijana wadogo wanaotafuta shughuli za upimaji viwanjaa na hawapatii?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom