Iramba tusidangayike tena, Mbunge wetu Dkt. Mwigulu hana uchungu na sisi kabisa

Lyambalyetu

JF-Expert Member
Apr 6, 2021
258
233
Ninatoa mfano wa Dr Mwigulu, mbunge wetu, akiwawakilisha Mawaziri na Viongozi wote wa Serikali, hasa wale wateule wa Rais.
Kila siku pakikucha Dr. Mwigulu anakuta nje gari la Ofisi limepaki anachukuliwa na dreva - gari limejazwa mafuta na Ofisi, so kwa kuwa hatumii gari lake basi tozo ya mafuta haipo tena. Hili linagusa watoto wake pia ambao ama wanabebwa na gari la ofisi au wapo Boarding. Gari hili pia hutuimka hata kwa safari za binafsi anapokuwa anaenda kijijijini kwao kule Makunda Iramba au pale kwenye nyumba yake Ulemo.

Mshahara wa Dr. Mwigulu na maruprupu mengine yanaingia moja kwa moja kwenye akaunti yake. Hivyo akienda Benki anaenda moja kwa moja kaunta ya bulk cash anahudumiwa hapo au mara chache anatoa fedha kwenye ATM. Ni nadra sana Dr. Mwigulu, mawaziri na hata wabunge kuwaona wanafanya transactions kwenye mobile money shops. Akitaka kuwatumia ndugu zake huku Iramb, ama ataingia moja kwa moja kwenye akaunti ya benki na kurusha huko huko au atamtuma dreva au msaidizi wake akawatumie. Ndugu zake waliopo kijijini labda ndiyo wataguswa na tozo hizo kwa sababu yeye alywas atakuwa ni mtu wa kuweka tu na wala sio wa kutoa. Hata anapolipwa posho zingine na Taasisi za chini yake hazitumwi kwenye simu - sana sana anapewa cash kupitia wasaidizi wake au anatumiwa kwenye akaunti yake.

Kuhusu kodi ya ardhi - ukweli hiyo wala sio kodi ya nyumba bali ni kodi ya mpangaji au "household tax". Ni ngumu Mwigulu kuishi nyumba ya kupanga - sana sana anaishi nyumba ya Serikali au amejenga yeye. Vyotevyote kumbuka kuwa Waziri na Viongozi wengine wote wanalipwa posho ya "utility" yaani umeme na maji kila mwezi. So wao wakinunua umeme wanatumia mihela ya Serikali ambazo ni kodi zetu. Wakubwa wengi ni nadra sana kushi nyumba za kupanga - wanaishi nyumba zao na zingine wanapangisha kwa walipa kodi ya pango.

Kwa cycle hiyo watu kama akina Dr Mwigulu, mbune wetu, hawawezi kamwe kuona machungu ya walalahoi kama sisi kwa kodi wanazotupangia. Kodi zote hizo zinalipwa na watu wa chini - wanunuzi wa mafuta ya magari ni wale watu wa kawaida tu may be na wafanyabiasahara, na sio viongozi. Ukija miamala ya kwenye simu inafanywa na watu wa chini amabao majority ni wafanyakazi wa chini na wakulima - viongozi wao mihela yao ni kwenye akaunti za benki na kulipwa cash kupitia kwa wasaidizi wao. Kodi ya ardhi - inalipwa na wapangaji ambao wengi ni wafanyakazi wa chini wasiliolipwa allowanace ya utility na wala hawana nyumba zao binafsi.

WaTanzania tumelela sana - ndiyo maana Mbunge mmoja katoa wazo la wao kukatwa kodi ameitwa kwenda kuadabishwa! Kazi kweli kweli!
 
They are fu*king you very hard now baada ya wagombea wa CCM kupora uchaguzi halafu ninyi wananchi mkawachekea na mimi nakuumiza zaidi kwa kukuambia ukweli ambao huwa unajidanganya kuwa hauujui.

Ukweli wenyewe ni kwamba Mwigulu au kiongozi yoyote yule wa CCM huwa hategemei kura ya mtu ili kuchukua madaraka.

7654311.png


Hii maana yake ni kwamba hata usipompigia kura Mwigulu bado atazidi kuwa mbunge wako na kuendelea kukutawala as long as he want.
 
They are fu*king you very hard now baada ya wagombea wa CCM kupora uchaguzi halafu ninyi wananchi mkawachekea na mimi nakuumiza zaidi kwa kukuambia ukweli ambao huwa unajidanganya kuwa hauujui.

Ukweli wenyewe ni kwamba Mwigulu au kiongozi yoyote yule wa CCM huwa hategemei kura ya mtu ili kuchukua madaraka.Hii maana yake ni kwamba hata usipompigia kura Mwigulu bado atazidi kuwa mbunge wako na kuendelea kukutawala as long as he want.View attachment 1909540
Leta vudeo tumsikie na sio kuunganisha maneno
 
Leta vudeo tumsikie na sio kuunganisha maneno
Hiyo habari ipo huku JF na hiyo ni screenshot kutoka JF,search kama ilivyo utaiona.

Halafu JF huwa hawakubali habari za uongo au za uzushi kuwa katika jukwaa lao in case ulikuwa hujui.JF ni credible source ya habari kwa maana ya kwamba kilichoandikwa hapo kwenye hiyo screenshot ndicho alichosema.
 
Hiyo habari ipo huku JF na hiyo ni screenshot kutoka JF,search kama ilivyo utaiona.

Halafu JF huwa hawakubali habari za uongo au za uzushi kuwa katika jukwaa lao in case ulikuwa hujui.JF ni credible source ya habari kwa maana ya kwamba kilichoandikwa hapo kwenye hiyo screenshot ndicho alichosema.
Ndio ila huoni maelezo hayo hakuna aliposema wataunda serikali ndio maana nikaomba video
 
This is real, ingawa umechukua thread yangu na kuiweka katika mazingira ya kwenu!
 
Ndio ila huoni maelezo hayo hakuna aliposema wataunda serikali ndio maana nikaomba video
Hivi nilichoandika hapo juu umekielewa?Unaelewa maana ya credible source?CNN au BBC wanaweza kuandika kitu kwenye page yao halafu upinge useme kuwa ni uzushi kwa hiyo unahitaji video?

Credible sources kama vile BBC,CNN,gazeti la mwananchi,JF na kadhalika wanapoandika kitu maana yake ni kwamba hicho kitu ni sahihi na kinapaswa kuaminika kwa sababu hawa ni credible source na wameconfirm walichoandika.

Labda ngoja nikuambie kitu ambacho hujui kuwa unapoandika habari fulani hapa JF mods huwa wanaenda kujiridhisha haraka sana kama hicho kitu ni sahihi na kama hiyo habari ni uzushi wanaifuta mara moja.

Hii screenshot yangu JF hawawezi kuifuta kwa sababu ni habari ambayo ipo humu na walijiridhisha kuwa ni ya ukweli na wakaiacha humu.

Huwezi kusoma habari kwenye gazeti la mwananchi au hapa JF halafu useme kuwa hiyo habari ni ya uongo kwa hiyo unahitaji video labda uwe na matatizo makubwa sana ya akili.
 
Mbona Mbunge wenu alisema,hizo tozo haziwahusu wananchi wa Jimbo lake ,
 
Wanyiramba mlivyo wasahaulifu uyo jamaa atachora chora tena mawe kisha mtamchagua tena
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom