Iramba-Singida;Minada yaendelea kama kawaida licha ya tishio la Corona

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,634
26,369
Wakuu,

Baada ya kuwepo kwa ugonjwa wa covid-19 maarufu kama Corona nchini Tanzania,serikali kupitia Waziri mkuu ilipiga marufuku mikusanyiko mbalimbali ikiwemo,semina,mikutano,vikao,warsha nk,na ikaenda mbali zaidi kwa kufunga shule kuanzia chekechea hadi vyuo vikuu.

Lakini katika hali ya Kushangaza serikali imeendelea kuacha Minada ifanyike kama kawaida.

Kuna mnada umefanyika leo tarehe 20/3/2020 katika kijiji cha Malendi tarafa ya Shelui wilayani Iramba na chanzo cha taarifa ni wakazi wa eneo husika.

Ni Minada hii hii ambayo hukusanya watu wengi kutoka maeneo tofauti tofauti ambapo watu hubanana,bidhaa hushikwa na watu wengi kwa wakati mmoja,ulaji na unywaji wa vinywaji baridi na vileo.

Je kuachwa Minada iendelee kuna nia njema na afya za watanzania? Au mapato ni muhimu kuliko afya za watu?
images%20(1).jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, Acha watu watafutie watoto ugali, corona ni mafua ya kawaida mno sema ninyi mnayatukuza mpaka yanaonekana kuwa tishio wakati sivyo
 
Back
Top Bottom