'iramba magharibi ,jimbo la watanzania waliokosa matumaini ya kesho' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'iramba magharibi ,jimbo la watanzania waliokosa matumaini ya kesho'

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mwanakidagu, Jul 5, 2012.

 1. m

  mwanakidagu JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 208
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  1.maji
  2.elimu
  3.afya
  4.kilimo
  5.hali ya umaskini

  Kwa heshima nianze na salamu kwa wazee wangu wote ndani ya jimbo.pamoja na vijana wenzangu mnaoweza kujitokeza kupiga kura ya kuamua mustakabali wa maisha yenu ya usoni.
  Nimeainisha hayo mambo kifupi.

  *Nianze na elimu*
  ndio kwanza hamu ya vijana kujitahd kujipatia elimu imekoma.kuanzia ngazi ya awali hadi elimu ya sekondari,ukimsikia mwenye jimbo akijinadi maskini mbele ya wazee wetu ati ametoa madawati 50.wakati takriban jimbo lote watoto wana lazimika kuinama ama kusujudu wanapoandika.je hamu ya kwenda shule itatoka wapi!.vijana kwa wazee amkeni kukataa ujinga na kuchagua mabadiliko .

  *maji*

  ndio kwanza watoto wameanza kuzaliwa wana typhoid fever tangu tumboni mwa mama zao.yeye mwenye jimbo aliahd maji kila kona'enyi ndg zangu mtadanganywa kwa kupewa t.shirt na kofia na khanga mpaka lini.maji ni tatizo si kwa wanyama tu bl hata kwa binadamu kama sisi wa mbunge mahiri wa mipasho bungeni.tumedanganywa vya kutosha tumenyonywa vya kutosha'tumedhalilishwa vya kutosha.tumefika hapa tulipo ni kwa sababu ya wabunge dhaif wa ccm ndani ya jimbo letu.

  *Afya*
  hakuna hata exray ndani ya hospitali yet ya wilaya.dawa hakuna.tumerudia mita shamba. Wakubwa kule dodoma hawajali wamejipa jukumu la u semaji wa serikal.wana beza vyama vya upinzani vinavyo pigana kiume kuikumbusha ahadi zake kwani muda unaisha lini watatekeleza.

  *kilimo*

  uti wa mgongo ,uti wa familia nying. Waishio mijini na vijijin,
  kimetekekezwa jimboni kupitia migongo ya wazee we2.kimegeuka kuwa uti wa mgongo wa matajiri wanaowapunja wakulima katika mazao ya alizeti,vitunguu!.nk.hakuna soko la uhakika.mwenye jimbo yupo makini kukagua missing number kwenye ktk kusomwa kwa bajeti ya chama cha kwanza cha ushindani kinacho jiandaa kutwaa madaraka kwani kinaelekea kueleweka miongoni mwa wa tz wengi.waishio mjini na kijijini(mwigulu hatujakutuma hayo.).soko la mazao yetu li wapi tuondokane na kuishi kwenye nyumb za tembe tangu dunia kuumbwa! Ama wewe na nyinyiemu yako mnampango wa kuligeuza jimbo kuwa sehemu ya kitalii kuona nyumb za kale?

  *hali ya umaskini jimboni iramba magharibi!*

  umaskini unatisha.warudishieni wanyiramba maisha bora ,kwani kila sk serikali ya nyinyiem inawanyonya wanananch walio chini ya kipato cha nusu dola @750sh.michango isiyokuwa na tija..
  LAMECK. Tekeleza ahad zako kwa wanajimbo .

  Mods .msifute uzi huu ili wenzangu wa jimbo hl wa changie kwa muda wa kutosha.
   
 2. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Kijana wenu amelewa madaraka ambayo amepata bila kuandaliwa kwanza kuwa kiongozi! Hana tofauti na Lau Masha!
   
Loading...