Iramba: DC Mwenda ataka mpango mkakati wa kutekeleza majukumu, akaza kamba kero za Wananchi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,858
930


MHE MWENDA ATAKA MPANGO MKAKATI WA KUTEKELEZA MAJUKUMU, AKAZA KAMBA KERO ZA WANANCHI.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe Suleiman Yusuph Mwenda ameendelea na ziara yake ya kupita kata kwa kata kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea maelezo na ufumbuzi wake. Akiwa kata ya Kiomboi leo Ijumaa Julai 30, 2021 akapata kero ya viongozi wa ngazi ya kata kukaa ofisini na kutoenda kutatua kero za wananchi ambapo Mhe Mwenda amewataka watumishi kuandaa mpango kazi wa kuonyesha namna watakavyotekeleza majukumu na kila mtu kwenye mtaa wake aonyeshe namna atakavyotekeleza majukumu yake na kila ijumaa Mtendaji wa kata apeleke daftari lenye kuonyesha majukumu hayo ofisini kwa Mkuu wa Wilaya.

Kuhusu matukio ya wizi na udokozi, Mhe Mkuu wa wilaya akamwagiza Kamanda wa polisi wilaya kuandaa mpango kazi na kuanzishwa operesheni ya kuwasaka wahalifu na wachukuliwe hatua za kinidhamu. Mkuu wa kituo cha Kiomboi OCS akamuhakikishia Mhe Mkuu wa wilaya kuwa atafanya operesheni na Jumapili majibu yatapatikana na kuwaomba wananchi wote wampe ushirikiano kwa kuwafichua wahalifu kwa kuwa wanaishi nao katika maeneo yao na wanawajua.

Suala la wananchi kupatiwa hati za kimila katika mji wa Kiomboi, Afisa mipango miji alimtaarifu Mhe Mwenda kwamba kuna vijiji 12 ambavyo vina sifa ya kutoa hati za kimila na wako mbioni kulikamilisha. Pia Afisa mipango miji aliwaambia wananchi wa Mji mdogo wa Kiomboi kuwa maeneo ya Ndago, Shelui, Misigiri na Kiomboi yana hadhi ya miji hivyo wamiliki wa ardhi wa maeneo hayo wanasifa ya kupata hati za kawaida. Pia Mhe Mwenda aliwaagiza watu wa idara ya ardhi kuhakikisha wanapanga ratiba ya kwenda kwa wananchi kuwapa elimu ya namna ya kupata na kumiliki ardhi ambazo zitawasaidia katika kupata amana mbalimbali mfano mikopo.

Pia Mhe Mwenda aliwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Corona kwa kuhakikisha wananawa maji tirirka na kutumia vitakasa mikono na kuvaa barakoa.

#KaziinaendeleaIramba

IMG-20210731-WA0001.jpg


IMG-20210731-WA0002.jpg


IMG-20210731-WA0003.jpg


IMG-20210731-WA0004.jpg


IMG-20210731-WA0005.jpg
 
Back
Top Bottom