IQ ya Nyerere ilikuwa kubwa sana: Debate kati ya Nyerere na mke wa Rais Roosevelt

Nae alikuwa Tanganyika akidai Uhuru?


Huyu ni Mkenya mashuhuri alikuwa ni miongoni mwa wanasiasa na wanaharakati wa kudai uhuru si Kenya tu bali Afrika mashariki na Afrika yote, alikuwa (kwa maoni yangu) mzuri katika Lugha (Kimombo) na mtaalamu mkubwa wa kujibu maswali ya mtego alipohojiwa na wazungu.

Nenda youtube cheki, Tom Mboya.
 
Kwa hiyo katika nchi hii tangu tupate uhuru hakuna cha maana chochote kilichotekelezwa na Rais (mwalimu) J.K Nyerere? Hata kutekeleza harakati za kupata uhuru ambao ndiyo msingi wa sisi kujitegemea kama nchi pia huoni kwamba ni jambo kubwa la kumpongeza Mwalimu Nyerere pamoja na wenzake? Be a critical thinker siyo unaleta chuki binafsi kuhusu Nyerere. Sasa ni Rais yupi ambaye ametekeleza hayo unayoyataka kuliko Nyerere? Mbona mpaka leo mnalalamika tu. Haya unayoyaona leo ni Muunganiko wa utekelezaji wa toka awamu ya Kwanza hadi sasa. Infact hakuna awamu ambayo imeshawahi kutekeleza mambo mengi katika kila sector kama ilivyokuwa awamu ya kwanza ya uongozi wa nchi yetu.

GO BACK TO HISTORY MY BROTHER/SISTER
mbona una hasira!!?..huwezi fikiri ukiwa katika hali hiyo,nchi changa haiwezi kuwa na war fronts nyingi,unatangaza vita na ujinga,maradhi na umasikini...halafu hujengi sekondari kwa miaka 44,kisha unadai kupambana na ujinga,mashamba na viwanda vinakufa,miundombinu duni(barabara) vyama vya ushirika vinakufia ilhali una nguvu kubwa kimamlaka,lakini wakati huohuo uko frontline kukomboa nchi za kiafrika..hakuna utacho achieve hapo na sio smart move
 
Baada ya utumwa wote na ukoloni wote, bado wazungu walikuwa wako tayari kukaa mezani na ku-negotiate juu ya uhuru wa mtu mweusi! Wangeweza kukataa au kupuuza na hakuna lolote tungefanya.

Kutoka hapo, kuanzia miaka ya 1940's mpaka 1948 , wakatengeneza makubaliano ya makaratasi ramsi ya kisheria ya kuzuia ukoloni, utumwa na ubaguzi wa aina zote! UDHR, ICCPR, CERD, ICESCR na mengine mengi!

Kwenye negotiations za uhuru, Nyerere alikataa hizo bill of rights kwa kuwa alitamani madaraka yasiyohojiwa, hatimaye akajitungia autocratic constitution! Mpaka anang'atuka miaka ya 1980's ndio akaiingiza bill of rights kwenye katiba baada ya kutawala kwa uhuru sana! Tume ya Nyalali ilifanya kazi kubwa sana ya kuchambua sheria nyingi zilizokinzana na mabadiliko hayo ya kikatiba kisha mahakama kuu kuzifutilia mbali baada ya hapo! Mojawapo ni sheria pendwa ya "Preventive Detention Act".

Huyu "beberu" anauliza, mko tayari kujitawala!?? Do you have the necessary sophistications!??? the essentials? the economy? Ninaamini hilo lilikuwa ni swali lenye mantiki kubwa lakini lilijibiwa kisanii sana! Kutoka kwenye maisha ya uporipori kwenda kwenye mifumo mipya ya kisiasa, YOU ARE NOT GIVEN BACK "YOUR" JACKET. YOU ARE GIVEN A "NEW" JACKET.

Alifanya mambo mazuri, alikuwa na akili nyingi, lakini alikuwa na mapungufu yake!
 
Nimesoma capitalism ya kizungu nimeiva, ujamaa ni mzuri mno ila unapingana na human nature of individualism , egoism and selfishness! Kiasili kila mtu ni mlafi na lazima ashibe yeye kwanza na wanawe halafu ndo ataangalia jirani na nchi ! ni kinyume na asili ya binadamu kukabidhi kwa hiari kodi au mali ya umma bila shuruti, kunyongwa,kupigwa virungu, mabuti , kulala jela na sheria kali isiyochagua jina wala cheo cha mtu! Hivi ndivyo wazungu wanafundisha capitalism! Nyerere ni kiongozi mzuri mno hakuna muafrika anaemfikia kwa akili ila kitu kimoja tu hakujua Ujamaa ni ideology isiyofanya kazi kama hutawafunga kuwapiga na kuwanyonga wazembe wavivu wezi na mafisadi wa mali ya umma!! Maneno yangu haya yatasimama daima!
Hili ni tatizo la watu wenye akili nyingi, wao hufikiri wengine pia wanaweza kufikiri angalau nusu ya uwezo wao, kiuhalisia watu wengi hawatawaliwi na fikra bali mihemeko.
 
Kinachonisikitisha ni kuwa thats is only 50 years ago, na hao wote hapo wameshalala mavumbini, yaani miili yao imegeuka mavumbi, ni mafuvu tu.

Kweli ni ubatili na kujilisha upepo
Hata mimi niliwaza hivyo hivyo nilipoiona hii video siku za nyuma.
 
Mrangi,
Nadhani umekusudia nichangie katika uwezo wa Mwalimu Nyerere.

Viongozi wa TAA katika miaka ile mwishoni 1940 kuelekea 1950
hakuna aliyekuwa anamjua Nyerere kwa undani kupita Hamza
Mwapachu
.

Kati ya Hamza Mwapachu na Julius Nyerere mimi binafsi siwezi
kusema nani alimzidi mwenzake kwa akili.

Mwapachu ndiye alikuwa ''mentor,'' wao na ndiye aliyewakutanisha
Abdul na Nyerere.

Hamza ndiye aliyefanya juhudi Nyerere aingizwe kwenye uongozi
wa TAA 1953 na 1954 waunde TANU wadai uhuru wa Tanganyika.

Lakini hili lisingeliwezekana bila ya msaada wa Abdul Sykes aliyekuwa
Acting President na Secretary.

Hamza alikuwa anaamini kuwa mtu aliyefaa kuongoza kudai uhuru wa
Tanganyika ni Julius Nyerere ingawa kwanza Abdul yeye alimtaka Chief
Kidaha Makwaia
lakini wakati ule alikuwa bado hajafahamiana na Nyerere.

View attachment 1128440

Chief David Kidaha Makwaia wa Siha

Historia hii nimeileza mara nyingi inafahamika.

Mimi nimefaidi sana kusoma barua za Nyerere katika Nyaraka za
Sykes.

K
wanza lugha ya Kiingereza Mwalimu akiijua vizuri sana.
Nasikitika kuwa wenye nyaraka zao hawajataka kuzifungua kwa umma.

Nyerere alipopanda kwenye jukwaa Mnazi Mmoja na kusema kuwa sasa
Watanganyika wanadai uhuru wao mambo yalikwenda kwa haraka mno.

Ujumbe wa Mwalimu kwa Watanganyika ulikuwa, ''Kutawaliwa ni fedheha.''

Mwalimu alikuwa na uwezo mkubwa sana na kipaji cha kuzungumza na
kujenga hoja kila mtu akaielewa.

Yako mengi sana ninayoyafamu kuhusu Mwalimu Nyerere katika harakati
za kudai uhuru wa Tanganyika.

View attachment 1128420

Mwalimu Nyerere akihutubia mkutano wa TANU Mnazi Mmoja na huo mnazi mmoja wenyewe unaonekana.
Hiyo barabara ambako hizo nyumba zipo ni New Street ambayo ilikuwa inaanza Arab Street hadi Morogoro
Road. Kushoto kwa hizo nyumba ni Kidongo Chekundu. Hiyo ndiyo Gerezani ilivyokuwa katika miaka ya 1950.
Mmh...hii account imehakiwa au?
 
Wakati huo Nyerere alikuwa Yanki tu wa miaka 37 au 38 lakini alikuwa akitema madini ya hatari.

Huyu mzee alikuwa kichwa siyo mchezo!

Mkuu Missile,
Asante sana kwa madini haya.
Hii ndio interview yangu ya kwanza ya Nyerere wakati wa pre independence, nadhani ilifanywa alipokwenda UNO, 1958.
Thanks.
P
P
 
Kizazi cha Nyerere kilikuwa komesha sana,
Watu walikuwa weredi sana kwa kila walichokuwa wakifanya.
Kuna wapuuzi wanawalinganisha baadhi ya viongozi na Baba WA Taifa.
Nyerere kwa elimu yake alikuwa anauwezo mkubwa wa kuchambua mambo na siasa za ulimwengu kuliko wenye PhD zao wa sasa hv.
Nyerere, Salim Ahmed Salim, Hashim Mbita, Hassan Ngwilizi,
Kwa sasa hivi, Ambapo tunavilaza walioenda shule kama Kabudi, Mpango, watu pekee ambao naona wana ka unyerere ndani yao ni, January Makamba, Suleiman Jafo, na Halima Mdee
OMG!! Halima? U can't be serious aisee!!!
 
Haaaa mfano mama janet au mama jk wanakuaje wakiwa pale
Ifike Mahali ofisi za first Ladies wetu ziandae vipindi redioni na kwenye TV kwa ajili ya mijadala madhubuti ya kuhimiza maendeleo ya wananchi. Ma'first ladies' wetu wahusike moja kwa moja kuendesha vipindi.
===
Mwalimu was a best listener and a best discussant.
 
pumbaf ulitaka akulinde wewe na mbugaruu, wako wa kishamba huo, kwanza kwa nini uvae mbuga wewe si jinga?

uliwakoga wanakijiji wakakupiga unamlaumu Nyerere ndo maana hamkusoma kwenu. hela yenu ya pamba mkakimbilia mabuga ili ujionyeshe kwenye mastore ya kijijini kwenu, na kushindania wanawake.

wakati elimu ilikuwa ya bure. na alisema kabisa jifunze kusoma wakati ni huu.View attachment 1128423

Wewe na huyu Mzee ndio mliotoka vijijini tukawapokea Dar. Enzi hizo bilashaka ulikuwa bado hujazaliwa ndio maana unayadharau mabuga, wajanja ndo yalikuwa mapigo yao, Raisi unaacha kuweka sheria za maana unatunga sheria ya kupiga marufuku mabuga! Kataifisha mali za wengi na kuuwa wengi, hizi nyimbo mnazofundishwa shule kuhusu huyu mzee ndizo zinazowatia ujinga, huyu mzee na jiwe lao moja.
 
Wewe na huyu Mzee ndio mliotoka vijijini tukawapokea Dar. Enzi hizo bilashaka ulikuwa bado hujazaliwa ndio maana unayadharau mabuga, wajanja ndo yalikuwa mapigo yao, Raisi unaacha kuweka sheria za maana unatunga sheria ya kupiga marufuku mabuga! Kataifisha mali za wengi na kuuwa wengi, hizi nyimbo mnazofundishwa shule kuhusu huyu mzee ndizo zinazowatia ujinga, huyu mzee na jiwe lao moja.
Aaaahhh baba mtoro wewe noma! nimezaliwa ocean road mie wewe, yaani mimi na baba nyerere letu moja. ILA

Niombe samahani kuniweka kundi moja na huyo rafiki yako JIWE
 
Hata kwenye shule ya mataahira kuna namba moja na wakifuatiwa na wengine na wale wa mwisho wanawaona wale wa mwanzo ni ma genius sanaaa na kuwasifu sifu sanaaa hasa yule namba moja anaonekana ana IQ kubwa au yale maahindano ya para Olympic
Wakati huo Nyerere alikuwa Yanki tu wa miaka 37 au 38 lakini alikuwa akitema madini ya hatari.

Wanasiasa vijana wa leo mna la kujifunza namna ya kufanya midahalo, solution ni kujisomea sana, kuwa na maarifa mengi.

Ukimsikiliza Mwalimu hapa yaani anatambaa smoothly kabisa na panel ya kwenye huo mjadala bila wasiwasi wowote

Kwanza ana command nzuri ya English, lakini pia ana substance, yaani kichwani yuko vizuri.

No wonder profesa Mazrui wa Kenya aliwahi kusema kuwa kwa Marais wote wa Afrika wa kizazi cha Uhuru, hakuna aliyekuwa Intellectual wa kumfikia Nyerere.

Huyu mzee alikuwa kichwa siyo mchezo!

 
Zakaria...
Ikiwa unanijua utakuwa unasoma mara nyingi nikimwambia mtu kuwa sina tatizo na ufikiriavyo.

Ikiwa wewe unaona hivyo hakuna neno.

Mimi nimemsoma Hamza Mwapachu zaidi yako toka yuko Uingereza na "connections," zake na Fabians sasa hii huenda imeniweka katika fikra tofauti na wengine.

Zaidi nimemsoma Hamza katika TAA Political Subcommittee na mchango wake katika Constitutional Development Committee.

Katika hali kama hii lazima tutatofautiana katika kuyajua mambo.
Kwa maana hiyo, Maalim Said, Mama Givens, Msaidizi wa Mwalimu akiwa Rais alikuwa ni matunda ya connections za Mzee Hamza na 'the Fabian Society!!?'
 
Kweli kabisa mkuu!

Wewe isome tuu Tanzania vision 2025....maneno mazuuuri...Utekelezaji sasa....bhabhabhaaaaaa
Eti every 5 years iwe reviewed...tagets na milestones ziwe set....halafu tunajiuliza sijui tunakwama wapi.
Nilikuwa naisoma tena Leo hii vision nikaishia kusema wacha nijifanyie tathmini binafsi kabla sijakosoa sana hii ya taifa....kiufupi iko vizuri sana ila utekelazaji ndio janga
 
Back
Top Bottom