IQ Test: Kwanini Mzee Mkali alifurahia sana siku Mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 27 alipo muuliza "Baba hivi ulimpataje mama?"

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,067
26,997
Mzee Mkali ( 67) ana kijana wake wa kiume aitwae Mashoto ( 27 )

Siku moja Mashoto alimuuliza baba ake " BABA HIVI ULIMPATAJE MAMA?"

Mzee Mkali aliposikia swali hili kutoka Kwa kijana wake WA kiume alifurahi Sana Na haraka haraka akamuita Mama Mashoto akisema " MKE WANGU NJOO UMSIKIE MTOTO WAKO ANACHO KISEMA"

Baada ya Mama Mashoto kufika sebuleni , Mzee Mkali akasema " WEWE MASHOTO HEBU RUDIA TENA KUNIULIZA KILE ULICHO NIULIZA NA MAMA AKO ASIKIE"

Mashoto akapaaza Sauti yake na kusema " BABA HIVI ULIMPATAJE MAMA"?

Mama Mashoto alivyo sikia hivyo Kwa aibu kubwa aka ondoka sebuleni haraka haraka Na kwenda kujifungia chumbani kwake..

Mzee Mkali akamwambia " WEWE MAMA MASHOTO UNAKWENDA WAPI? HEBU NJOO HAPA "

Baada ya kaka dakika ishirini za kujifikiria mama Mashoto alirejea sebuleni huku akiwa kajifunika USO wake kwa aibu Na fedheha.

Kwa mshangao wa mama Mashoto ,Mzee Mashoto akasema "NIMEFURAHI SANA KIJANA WANGU MASHOTO KUNIULIZA SWALI ZURI KAMA HILI". Kisha akaendelea kusema Sababu iliyo mfanya afurahie kuulizwa swali kama Hilo Na Mtoto wake.

IQ test: JE KWANINI MZEE MKALI ALIFURAHIA KUULIZWA SWALI KAMA HILO NA MTOTO WAKE?

Una dakika arobaini za kujibu swali hili. Zikipita dakika arobaini bila kupata majibu nitatoa majibu.

Haya Sasa twenzetu
 
Oya bado dk 3 utupe jibu tusichoshane maisha yenyewe yameahatupiga.
 
Nimechelewa kuja ila hii ngumu!!

Jibu.
Mzee Mkali ni hasira na Kushoto ni busara. Hivyo ukipatwa na hasira sauti ya busara hukujia na kuuliza hasara na faida za kufanya tukio la hasira, hivyo ukilegezwa na busara ukagundua madhara ya kufanya maamzi ya hasira lazima ufurahi kufunguliwa na busara mapema. Ila mama mashoto ni akili yani kiunganishi cha busara ya hasira.

Zero kitu gan bwana☝️☝️☝️☝️
 
Nimechelewa kuja ila hii ngumu!!

Jibu.
Mzee Mkali ni hasira na Kushoto ni busara. Hivyo ukipatwa na hasira sauti ya busara hukujia na kuuliza hasara na faida za kufanya tukio la hasira, hivyo ukilegezwa na busara ukagundua madhara ya kufanya maamzi ya hasira lazima ufurahi kufunguliwa na busara mapema. Ila mama mashoto ni akili yani kiunganishi cha busara ya hasira.

Zero kitu gan bwana☝️☝️☝️☝️
Zero
 
Kawaulize wanafunzi wako sie tuna mambo mengi,ila jamani kwani unatuonaje kutuletea chemsha bongo
 
JIBU NI RAHISI TU,
MZEE ANAJUA KABISA KIJANA WAKE NI SHABABI NA KWA UMRI WAKE MTOTO HUYU ANATAKA MWENZA HIVYO ANATAKA KUJIFUNZA JAMBO KUTOKA KWA BABA YAKE ILI AJUE ANA ANZIA WAPI NA YEYE KUSAKA JIKO LAKE LA MAISHA.
 
Mtoto anataka kujua ilikuaje baba amepata mke bora na chombo?
Baba anaonekana wa kawaida sana

Mama kaona aibu
Kwa sababu ya majibu yatakayo tolewa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom