IPTL / Richmond

cremoo

Member
Nov 2, 2014
41
2
Nimetumia muda wangu mwingi kufuatilia maswala ya IPTL na Richmond/Symbion. Kutoka kwa jamaa wa usalama wa taifa ambae anafanya kazi ikulu amenipa ukweli kuhusu mmiliki wa IPTL, Dowans, Richmond/Symbion. Ukweli ni kwamba IPTL na Richmond ambayo kwa sasa ni Symbion zinamilikiwa na viongozi wa ngazi ya juu wa serikali.

Viongozi wa juu akiwemo kiongozi wa juu kabisa (jina limehifadhiwa) ndiyo wanaomiliki haya makampuni. Seth na mmiliki wa VIP ndugu Rugemalila ni kama mawakala tu lakini wala si wamiliki halali wa makampuni haya. Mtoa habari ameniambia mashine hizo zilinunuliwa kwa kodi za wananchi, kwa kupitia miradi hii viongozi wa juu wa serikali wamejivunia mabilioni ya pesa tangu miaka 90.

Ameniambia kuwa mashine hizi unufaisha takribani viongozi 72 moja kwa moja akiwemo waziri mmoja aliejiuzuru. Kuna viongozi wa ngazi za chini wenye influence au wenye kujua habari hizi wakiwemo usalama wa taifa upewa mgao kidogo ili kuwanyamazisha, pia utumiwa kwenye kampein za uchaguzi.

Aidha wale wasiopewa mgao ndio vinara wa kutoa nyaraka za siri na kuwapa wapinzani. Jamaa anasema, baada ya kugundulika kuwa Richmond haina mmiliki pale ambapo Mwakyembe alipokuta Marekani hakuna Kampuni inayoitwa Richmond , viongozi wa juu walimfuata mwanaume mwenye asili ya Asia wakampa milioni 800 ili ajifanye kuwa yeye ndie mmiliki wa Richmond, lakini huyo mmiliki alikataa kabisa kupigwa picha alipokuja nchini, alihofia sura yake ingeonekana ingekuwa ni hatari sana nchini kwake.

Aliefanya mchakato mzima wa kutafuta mmiliki fake wa Richmond ambayo kwa sasa ni Symbion ni Rostam aziz. Mpaka sasa Symbion inadai deni lenye utata la zaidi ya dola milioni 100, wakati ukifika zitalipwa Mtonyaji anasema, ili kupata njia rahisi ya kukwapua pesa za IPTL, viongozi walizua kesi fake ili kupitia wakili fake waweze kulipana hizo pesa. Wakili aliechaguliwa ni Mkono.

Mkono amepewa jumla ya bilioni 60 na kitu kwa ajili ya kesi, fedha hii ni nyingi sana, lakini kutoka kwenye fedha hizo yeye alikuwa anachukua kiasi na baadhi anawapa wakubwa serikalini. Inasemekana mgao wa fedha za makampuni haya ni mkubwa sana kiasi kwamba wengi wamehamua kufungua account nje ya nchi hasa kwa kutumia majina ya watoto wao, majina yanatumika ni yale ya kikabila/ kinyumbani kiasi kwamba uwezi kuwatambua kirahisi.

Kwa hiyo wadau; IPTL na Symbion, Dowans ni changa la macho, zinamilikiwa na viongozi serikalini. Kuna document nazisubiri,
 
Mosi Karibu JF ambako tunaruhusiwa kuongea bila woga kama nafasi hii uliyopata,

Pili unapochangia JF tulia andika kitu kinachoeleweka, sio kila msomaji anaweza kusoma mpangilio unaochosha, wengine watapita bila kusoma kutokana na maandishi yako,

Tatu tafuta ushahidi kabla haujaandika, inawezekana unapoint lakini ukishachanganya vitu ambavyo haujafanyia uchunguzi kiasi cha kutosha watu hawataendelea kusoma hata kama thread yako inaonyesha kuwa na vitu vyenye interest kwa jamii

Karibu sana
 
Jawabu la Tanzania kuwa huru ni JWTZ kuchukua nchi vinginevyo nchi kishauzwa baada ya baba wa taifa kuaga dunia
 
Kwa taarifa yako hata hao unaowaota JWTZ nao ni watiifu kwa chama, hasa wakubwa na wale walio na umri mkubwa. Wakistaafu wanateuliwa kuwa wakuu wa wilaya na mikoa. The country is corrupt in every sector
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom