Ipp mpaka leo hatujapokea mishahara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ipp mpaka leo hatujapokea mishahara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by TreasureFred, Sep 3, 2009.

 1. TreasureFred

  TreasureFred Member

  #1
  Sep 3, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana Jf

  Nimesukumwa kuandika post hii baada ya kupata tetesi kuwa mwenyekiti anaenda Tabora kutowa msaada wakati mpaka leo hii hatuja pokea mishahara yetu.

  Mwezi ulopita tumepokea tar 8,juzi imetumwa email na idara ya uhasibu kuwa ttusitegemee mishahara soon hili ni jambo la kuikitisha.

  Najua pos hii itaondolewa lakini umefika wakati kujiuliza hii ni haki?

  amekuwa mstari wa mbele kututaka kuwa wavumilivu,umeanzishwa mtindo kuwa pesa za Matangazo mwenyekiti anazichukua zote kufanyia siasa sisi anataka kampuni ijiendeshe kwa pesa za kuuza magazeti wakati kurasa moja ya NIPASHE ama GUARDIAN thamani yake ni magazeti 3000,tunatafuta matangazo pesa anazichukua matokeo yake tunalipwa tarehe 8 or 15 ya mwezi mwingine hii inavunja moyo na kuumiza.


  naomba kuwasilisha
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Sep 3, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,876
  Trophy Points: 280
  Tanzania tambarare, ukiona nyingine kuzimu!
   
 3. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mbona unajistukia mkuu?
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  I thought charity begins at home!but unaweza kuta yeye alishasign cheque kitambo wahasibu wanajibaraguza.
  Huwa nakerwa sana na wahasibu si wanasikia raha kukaa na mihera ya watu eti muutambue umuhimu wake kwenye company.
  TUACHE ULIMBIKENI KWA WENYE IYO TABIA
   
 5. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #5
  Sep 3, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  hayo ni majungu tu, soko la ajira liko wazi kwanini usiache kazi kama IPP hailipi, nenda New Habari au kule channel ten ukale kuku kama wenzio.
  IPP ina policy zao, na IPP NI TAASISI KUBWA mENGI KUTOA MISAADA UJUE WAKATI MWINGINE SI PESA ZA IPP, yeye anaubia na makampuni mengi kama jina lake.....
  wito wangu kwako kimbia hapo.....nenda hata dailyNews ukalipwe TGS D. Kama hutaki vumilia .
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,272
  Likes Received: 5,635
  Trophy Points: 280
  pole sana nahisi ni vizuri ungekuwa mwalimu haya yote usingeeumia sie mpaka tar 35
   
 7. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mmeanza kumpakazia mzee wa watu... Huyo ana mihela yake kibao kutoka sources mbalimbali hawezi kutegemea vijisenti hivyo vya Nipashe. Nyie mna matatizo yenu wenyewe huko.
   
  Last edited: Sep 3, 2009
 8. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Nadhani tuache kuchanganya mambo hapa! Hela za mwenyekiti na mishahara wapi kwa wapi?

  Je kama payroll software ina kwikwi... hatuwezi jadili vitu nusu nusu.

  Kwa vyovyote ufanisi wenu sio mzuri, na kawaida inachangiwa na wafanyakazi pia. mauzo kama yameshuka...
  matokeo yake ndio hayo... dinner za mzee Mengi za maskini haziwezi kukosesha mshahara.
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Duh yaani mpaka leo bado hamjapata salary ohoo lakini si mbaya sana kwasababu sisi tuliopata mshahara tarehe 25 tayari tumeshamaliza tunaomba mungu mwezi ukimbie haraka.

  Msaada anaotoa Mzee Mengi wakati mwengine hauna uhusianao wa moja kwa moja na fedha za IPP Media.Mzee Mengi ana makampuni nyngi kama lilivyo jina lake kwa kuanzia tu ana kampuni ya Bonite Bottles ya mjini Moshi,ana kampuni ya body care na nk.Mleta hoja ana uhakika gani Mzee Mengi kachota fedha za matangazo IPP.

  Napata mashaka kidogo juu ya nia na madhumuni ya mleta hoja kwamba pengine ni miongoni mwa lile kundi kubwa la wanaopiga vita makamanda wetu wanaopinga ufisadi.Hawa jamaa wako kila kona yaani mpaka NEC na CC wameshaiteka mahali wanaposhindwa kidogo ni pale mjengoni na hapa Jamii forums.
   
 10. M

  Magezi JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Leo ni tarehe 3 sept. nadhani hawaja chelewa kiasi cha kuanza kumsema vibaya Mzee Mengi. Mbona serikali yenyewe huwa wakati mwingine inashindwa kulipa on time? haya ni matatizo ya kawaida hasa ktk sekta binafsi inayotegemea soko na si kodi kama serikali.

  Kama walivyo shauri wenzangu, ukiona hujaridhishwa na mwenendo wa IPP MEDIA ki maslahi basi mlango uko wazi katafute kampuni nyingine. Mimi huwa sipendi mijitu ya kulia lia huku kuchukua uamuzi inaogopa. Niliwahi kufanya kazi ktk kampuni ya AIR conditioners ya wahindi (inaitwa DAIKIN) pale nyerere road, pale nilikuta wabongo wanaolialia huku shule hawana. Mimi nilikaa pale miezi 5, lakini kumbe wale wabongo ndo waliokuwa wanapeleka umbea wa yote tuliyokuwa tunaongea tukiwa site.

  Siku moja muhindi alikuja site akasema muda wa kazi ukiisha tukiwa site lazima turipoti ofisini alafu ndo kila mtu aende kutafuta daladala, mimi nikamwambia pale muda wa kutoka kazini utakapofika nikiwa site, basi ntaondokea huko huko, kiongozi wetu ndo anawajibika kuja hadi ofisini. Muhindi akasema wewe jeuri ntakufukuza, nikasema mbona mwezi huu naacha kazi!! Akasema wewe jinga masikini uache kazi? anaglia wenzio hawa wanamiaka mingi hapa na hawana jeuri ya kuacha kazi.

  Siku iliyofuata yaani kesho yake nilienda ofisini kama kawaida, nikapangia kazi, nilipofikishwa site nikamwambia dereva arudishe vifaa mimi ndo nimeacha kazi rasmi. Yule muhindi alinitafuta miezi 3 nirudi nikamwambia kwa simu kwamba aliowazoea siyo mimi sitaki kazi tena. Wakati huo ananipigia simu mimi nasoma UDSM.

  Kwa hiyo huyo wa ippmedia naona anajaribu kueleza umbea usiokuwa na manufaa.
   
 11. a

  adobe JF-Expert Member

  #11
  Sep 4, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 1,666
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  we hujasoma ndo maana hujapata mshahara.kazi haiko ipp peke yake ziko sehemu nyingi kama una qualification zako nzuri achia ngazi.au umetumwa na mafisadi papa?
   
 12. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #12
  Sep 4, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,968
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Duu Kali hiyo Dictatorship ya manyangumi ni kali
   
 13. J

  Jahom JF-Expert Member

  #13
  Sep 4, 2009
  Joined: Aug 26, 2008
  Messages: 349
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  nilidhani mtu akiomba msaada si lazima asaidiwe. Nawashauri wale ambao hamna point za kumsaidia huyu asiseme kitu. Amepoost hii kuufahamisha umma kuwa kunafuka moshi. Ni ukweli kwamba ktk kipindi kifupi wengi wameacha kazi IPP. Ni vema habari hizi ziwe wazi
   
 14. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #14
  Sep 4, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kama mnaona hampati mishahara kwa wakati ondokeni mkatafute kazi sehemu nyingine. Sioni kwa nini utoe siri za kazini kwenu kwa watu ambao hatuwezi kuwasaidia kupata huo mshahara.
   
 15. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #15
  Sep 4, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  SIO TU KIPINDI HIKI, HII NI TAASISI HURU....mmoja anatoka kumi wanaingia, IPP ILIKUA NA KINA Misanya Bingi, Charles Hilary, Mikidadi mahamudu, suzan Mungi, Flora Nducha.....wote hao walikua nyota na wakaondoka, hakuna chaajabu , ni majungu tu.
  wanapaswa kuongeza tija nasikulalama tu, sasa mzee Mengi ndio afisa uajili wao.
  Mengi ni mwenyekiti na anamajukumu mazito.
  Hakuna Moshi unaofuka IPP-media........ushauri wangu ni kua Aacj=hae kazi aende mahali ambako hakuna matatizo, mbona Amina Mollel yuko TBC TAYARI, KAMA huridhiki kimbia ,usigeuke nyuma.
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Sep 4, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mtajili wengi wa Kibongo wanapenda sana kujionyesha kwa watu kuwa wanasaidia maskini lakini sie tuliopo kwenye kazi zao hatuthaminiwi, mishahala kiduchu na tunacheleweshewa ndo hivyo Miafrika ndivyo tulivyo.
   
 17. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #17
  Sep 4, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mhhhhh!! payroll ipo mzigoni kha!
   
 18. OFFORO

  OFFORO Member

  #18
  Sep 4, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kama wenzangu walivyoshauri ukiona ipp haikupi kile unachokitaka acha kazi, waache wengine nao waje wafanye hapo maana nafasi hiyo wengine wanaitaka
   
 19. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #19
  Sep 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Laiti mngejua maisha ya IPP...
   
 20. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #20
  Sep 4, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  kwahiyo mmegundua zile mlizokuwa mlipwe ndio zinaenda nzega?
  malalamiko yenu mmeyapeleka mahala husika au ndio mnaazia hapa jf?
  kama huwa inatokea mara kwa mara mmeshakaa na mwajiri wenu kupitia chama cha wafanya kazi tawi la hapo kwenu mkaelezea matatizo yenu mkaona hasikilizi?
  vinginevyo inawezekana madai yako ni ya kweli lakini watu wakaona ni uzushi kisa yamepelekwa sehemu isiyo ya kwake, siunajua hata mahindi yakiota kwenye shamba la ufuta ni magugu?
   
Loading...