IPP Media yaisusia Simba Sports Club | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IPP Media yaisusia Simba Sports Club

Discussion in 'Sports' started by Mayolela, Jan 23, 2010.

 1. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2010
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli wenye visa watu,Kampuni ya IPP Media amepiga stop habari zozote zinazohusu klabu ambayo kwa sasa ni gumzo hapa Afrika mashariki na kati kwa ushindi mfululizo.

  Kwa mfano ushindi wa simba dhidi ya Prison haujatangazwa kabisa, zaidi ya kurukia mechi ya kesho kati ya Yanga na Manyema Fc, nadhani sio haki kwani mnawanyima haki wasikilizaji na watazamaji wenu. Suala la kuonyesha live ni kweli lazima kuwe na makubaliano kati ya pande husika.

  Kweli tutafika hivyo?
   
 2. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wakaonyeshe Mechi ya kandambili na Manyema Kesho kama Kandambili atakubali! Tatizo la wabongo ukionyesha Mpira live hawaendi Uwanjani sasa kama timu zinategemea mapato ya Mlangoni huoni zinaathirika! Simba endeleeni Uzi huo huo unless kama wanawalipa some money for compensation
   
 3. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2010
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Inajulikana Mengi na watangazaji/wanahabari wao wengi ni supporters wa Yanga. Lakini, hawajui wanajiharibia biashara? Nakumbuka walishawahi kufanya hivyo miaka ya nyuma na wasikilizaji na watazamaji wanapenda michezo wengi waligeukia vyombo vingine vya habari.
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,842
  Trophy Points: 280
  vyombo si vipo vingi mazee
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hii inadhihirisha ule upuzi wa baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vinaongozwa na hisia na mapenzi kuliko professionalism
   
 6. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #6
  Jan 26, 2010
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,280
  Likes Received: 4,283
  Trophy Points: 280
  Hii si mara ya kwanza imewahi kutokea huko nyuma
   
 7. M

  Magehema JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hii hoja haina ukweli na haihusiani na mzozo uliopo kati ya Simba na vyombo vya IPP. Unataka kuniambia Mengi ameanza kuishabikia Yanga juzi wakati mechi na Lyon/Manyema, mbona kabla ya hapo habari za Simba zilikuwa zinaandikwa na kutangazwa katika vyombo vya IPP? Tuache unafiki, swala lipo wazi ni kweli Simba walikuwa na haki ya kuja haki yao ipo wapi mechi yao ikirushwa live, lakini approach yao ni ya kimtaani mtaani zaidi, ilikuwa ni suala la wao kuwasiliana na TFF na sio kutishia kuvunja vifaa ya kurushia matangazo. Huo ni UHUNI!
   
 8. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,063
  Trophy Points: 280
  Jamani acheni unazi.
  Mara ngapi kwenye siku ambayo yanga imecheza na kwenye taarifa ya habari-michezo tunatangaziwa habari ya basket ball nk na wakati mwingine hata matokeo ya mechi wasitangaze-ndiyo maana tunakimbilia Star TV/TBC/Channel 10.
  IPP hawaishabikii yanga tangu miaka ile ambapo mzee mengi alipojitolea kuleta umoja yanga na wahuni wakamtolea lugha isiyo ya kistaarabu.
  Lakini kwa hili la simba naamini hawakutumia busara kwani prime time ya TV za tanzania ni saa2 Usiku ambapo audiance kubwa ya waTZ huwa glued on TV na hasa michezo kwa wakati huu kampuni za TV hutoza bei ghali sana matangazo sasa wakisusa anayekula hasara ni nani???? nadhani wangeacha kuwa emotional kwenye biashara. Suala hili wangeliachia TFF wamalizane na wadau wao kwa sababu wao ni wateja wa TFF
   
 9. B

  Bongo Lala Member

  #9
  Jan 26, 2010
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kampuni za IPP zinaendeshwa kwa visasi, yaani thinking yao ni kama watoto wadogo. hata kama ni kweli some few Simba people walileta mzozo na crew ya Itv is it fair kuwanyima habari wanaSimba waliojaa nchi nzima?? sijawahi kuwaona watu wanafiki kama IPP Media, to hell with them....
   
 10. N

  Nanu JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Siyo mambo ya visasi, watangazaji na waandishi wa habari na wapiga picha wa ITV walizuiliwa na uongozi na mashabiki wa simba kuingia uwanjani kuonyesha mechi yao na kutangaza. Si wameona kuwa Dar ndiyo kuna mashabiki tu? Viongozi wetu wa vilabu hawajumlishi na kutoa kabla hawajafanya maamuzi hasa hawa akina Kaduguda..
  Lazima wajue yafuatayo:
  1. Simba au Yanga washabiki wake si wa Dar tu
  2. Watu wengi wa nje wanapata muda wa kuangalia performance ya wachezaji
  3. Wadhamini (TBL) wao wanapata coverage kubwa (hivyo wataongeza dau)
  4. Inasaidia kuweka records sahihi na zitatumika kusahihisha makosa ya wachezaji na waamuzi
  5. inawapa wale watu ambao kwa maumbile yao hawawezi kufika uwanjani nao kuburudika na kushangilia timu yao
  6. itaisaidia timu kuendelea kupata mashabiki wengi na kuongeza mapenzi kwa timu hivyo baadaye wanaweza kupata michango mingi kupitia mitandao n.k.
  7. Kwa soka la kwetu linahitaji kutangazwa zaidi ili likuwe na timu ziweze kuwa na wafadhili wengi ambao wataifanya iwe na mapato mengi zaidi.
  8. Hii inataka kiongozi ambaye si "short sighted"
  9. timu inapoonekana kwenye luninga ikiwa Dar ikienda mikoani watu watataka kuona timu live na hiyo itaongeza mapato.
  10. kuna faida lukuki za kuonyesha hii michezo kwa sasa lakini kama viongozi hawaoni hayo basi waachiwe timu zao,
  11. after all timu si simba tu tanzania na wala siyo bora na ndiyo maana hata tusker ilitolewa nishai na mabingwa ni yanga.
   
 11. alsaidy

  alsaidy JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 334
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu uko sahihi kabisa,approach ya simba ilkuwa ya kimtaani zaidi na IPP walijitetea kuwa walishapata baraka za TFF.

  Walichotakiwa kufanya ni kwenda TFF kujua haki yao wanaipata vipi lakini si kutishia kuvunja vifaa vya kurushia matangazi live.

  Hatoendelee ngo mpaka dunia inakwisha tutabaki na uswahili wetu!!
   
 12. M

  Magehema JF-Expert Member

  #12
  Jan 26, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ila mkuu usishangae, Simba na Yanga bado zinaendeshwa kimtaani zaidi hata kauli za viongozi wao ni vituko! Nakumbuka kuna kauli aliitoa Kaduguda siku moja, lilikuwa zogo kati ya uongozi wa Simba na Friends of Simba, alisema kama wao (FoS) wamemwaga ugali basi yeye atamwaga mboga na kuzima jiko! Haya ni maneno ya wachuuzi na wapakua mizigo wa bandarini, sio maneno ya kusemwa na katibu mkuu wa klabu iliyokongwe zaidi ya Enyimba!
   
 13. B

  Bumbwini Member

  #13
  Jan 26, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  magehema umenena ukweli mtupu,kama wanazi wa simba waliona wanakosa haki yao wangefata taratibu kupitia tff wakajua watapataje haki yao,sio kuleta mambo ya kihuni nakuanza fujo nakutaka kuvunja vifaa vya kazi wanajua thamani yake,ni mapesa mengi mno kuvinunua,mm binafsi nawaunga mkono waandishi wa ipp kuwasusia simba wako sawa kabisa.
   
 14. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #14
  Jan 26, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Shida ni kwamba IPP Media inongozwa na kwa mkono wa chuma! Mengi ni ka dikteta kadogo, yaani jamaa hajambo kwa visasi! Uki-mess naye utakuandama, tabia za kitoto sana hizo! Wanafanya migogoro kuwa personal na sijui hata hana mshauri! Hivi ukikataa kutangaza habari za simba nani ana-loose! Kama nilitaka kuona matokeo si Nitaenda Channel 10, au Star TV. Simba hawana cha kupoteza ila wao ndio itawa-cost!

  Pili IPP sio ya Mengi ni ya Watanzania wanao invest na wewe unapata faida unapowanyima haki yao ya kupata news kwa sababu ya ugonmv wako na Simba, that is too person!

  Na inaonyesha hata upeo wako wa kuona mbali ni mdogo kwa sababu wewe unawaona Simba tu lakini Big picture umemnyima haki kila mtanzania ambaye hata hajui unachogombania!
   
 15. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #15
  Jan 26, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Ni kweli ITV/Mengi inawezekana wanayo matatizo. Lakini, kama umemzuia mwandishi kuingia uwanjani au kufanya kazi yake, unataka akatangaze nini? Hiyo habari/picha ataitoa wapi? Sanasana ataishia kutangaza jinsi ulivyomzuia kuingia uwajani!

  Tatizo hizi timu zetu za soka zinaendeshwa 'kiswahili' mno mapaka wengine tumeshapoteza interest kabisa!
   
 16. N

  Nanu JF-Expert Member

  #16
  Jan 26, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama mtu amekufukuza utafanyaje?
  Ukivunja chombo cha mamilioni ya fedha utamdai nani wakati viongozi wa simba na mashabiki wao ni waganga njaa (mimi ni shabiki wa simba). Hakuna ugomvi kati ya IPP na Simba bali walikataa mechi isiyonyeshwe na waandishi walizuliwa na ilikuwa mtafaruku hata vyombo vingi vya habari vilitangaza hiyo kimbwanga. Sasa kama TFF walitoa kibali na wanachama wake wanakataa au wanaleta fujo na TFF iliyotoa kibali haijachukua hatua yoyote, sasa chombo cha habari kingefanyeje?
  Hapo watakapoona umuhimu wa kutangazwa watakwenda mezani wenyewe kusema sasa hatutawapiga uwanjani na kuwekeana mikataba ya maelewano.
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  Jan 27, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa Mkuu...
   
 18. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #18
  Jan 27, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  IPP ilisha wahi kususia kutangaza habari za Yanga? kwani nini simba tu...acha wasi tangaze tutasikiliza TBC,Clouse FM, RFA na nk au nawao wamegoma maana dagaa alidundwa na FFU mpaka akalazwa vipi haandiki taarifa za michezo siku hizi!?...Siku hizi vyombo vya habari kibao wakisusa JF si ipo!?...teh teh
   
Loading...