IPP kujenga kiwanda cha kubanguakorosho

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
korosho.jpg


KAMPUNI ya IPP Limited inakusudia kujenga kiwanda cha kubangua korosho mkoani Mtwara, ikiwa moja ya kampuni tano zilizoonyesha nia katika uwekezaji huo.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, alisema hayo jana ofisini kwake mjini hapa alipozungumza na waandishi wa habari huku akibainisha kuwa IPP ni kampuni pekee ya kizawa inayomilikiwa na mfanyabiashara maarufu, Dk. Reginald Mengi, huku zingine nne zikiwa za kigeni.

Alisema Dk. Mengi, ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kundi la Kampuni za IPP, alitembelea mkoani Mtwara wiki iliyopita kukagua eneo analotarajia kujenga kiwanda hicho katika kijiji cha Hiyari, wilayani Mtwara. “Mwekezaji mzalendo Reginald Mengi alifika ofisini kwangu na kuwasilisha nia yake ya kujenga kiwanda cha kubangua korosho katika mkoa wangu.

Nilimpeleka katika kijiji cha Hiyari eneo ambalo tumelitenga kwa ajili ya viwanda na tayari amechangua eneo alilopendezwa nalo,” alisema Byakanwa

“Tunachosubiri ni mwendelezo wa utekelezaji wa nia ya wawekezaji hao ila kwa namna ya kipekee nimpongeze na kumshukuru Mzee Mengi kwa moyo wake wa kizalendo wa kuwekeza nchini kwake kwa ajili ya ustawi wa Watanzania wenzake kwani viwanda hivyo vitatoa ajira kwa

Byakanwa alizitaja kampuni zingine zilizoonyesha nia ya kuwekeza katika viwanda vya ubanguaji wa korosho kuwa ni ni MBR International Trading Company, Safi Group Company, Shafa Investment na Food Source Company Ltd.

Alisema uwekezaji huo ni mwitikio wa serikali wa kuzuia usafirishaji wa korosho ghafi nje ya nchi na kuagiza korosho zote kubanguliwa nchini lakini akasema kwa sasa ni mapema kuelezea uwezo wa viwanda hivyo. “Kwa sasa tunajitahidi kuhakikisha miundombinu yote muhimu kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda inafika katika eneo la Hiyari.

Tumeazimia huduma za uhakika za maji na umeme zisogezwe karibu ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi,” alisisitiza. Mkuu wa Mkoa alibainisha kuwa hadi sasa serikali imekusanya na kuhifadhi katika maghala tani 209,398 za korosho ambazo zinasumbiriwa kubanguliwa na kwamba kujitokeza kwa wawekezaji hao kutafungua njia ya ukuaji wa sekta ya korosho katika kuliongezea thamani zao hilo. Ujenzi wa kiwanda cha kubangua korosho Mtwara ni mwendelezo wa IPP katika kutekeleza sera ya taifa ya maendeleo ya viwanda nchini kuelekea uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Dk. Mengi kwa kushirikiana na mbia wake, Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka India, Nagesh Bhandari, wameamua kujenga kiwanda cha dawa kitakachojulikana kama M-Pharmaceuticals. Kiwanda hiki ambacho kitajengwa eneo la Kerege, Bagamoyo, kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kuzalisha kwa siku chupa 100,000 za dripu kwa mwaka kitazalisha chupa milioni 30.

Kiwanda kingine cha kutengeza simu za mkononi za kisasa na za bei nafuu, kinatarajia kuanzishwa na Kampuni ya IPP Touchmate Ltd, ambayo pia itatengeneza vifaa mbalimbali vya kielektroniki, vikiwamo vya nyumbani. Kiwanda hicho ambacho kitakuwa cha kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki kitajengwa eneo la Mikocheni, Dar es Salaam na uwekezaji huo unakadiriwa kuwa Sh. bilioni 11.5 na kitakuwa na uwezo wa kuzalisha simu za mkononi 1,200 kwa siku, kuajiri watu 2,000 na watu wenye ulemavu kupewa kipaumbele. Kiwanda kingine ni cha kuunda magari Tanzania na tayari Kampuni ya IPP Automobile Ltd imeshaingia mkataba wa makubaliano na kampuni ya Youngsan Glonet Corporation kutoka Korea Kusini.

Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha zaidi ya ajira 1,500 kwa Watanzania. Kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kuuza mabasi ya abiria na magari ya mizigo kuanzia tani 2.5 mpaka tani 28 Oktoba, mwaka huu na baadaye mwaka 2022 kitaanza kuzalisha magari madogo.

CChanzo: Nipashe
 
Back
Top Bottom