Ipo wapi Sheria inayosimamia utoaji wa hati ya kusafiria ya kielektroniki Tanzania?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Nimetafuta maeneo mbalimbali sheria inayosimamia pasipoti za kielekroniki Tanzania ila sijaiona, nimetafuta kanuni hakuna, nimetafuta mwongozo hakuna popote.

Lengo la kutafuta nyaraka hizi ni kutaka kujua kama kigezo cha kuwa na National ID unapoomba pasipoti kipo kisheria au kimetungwa tu na Idara ya Uhamiaji. Nilitaka kujua kama watu waliochini ya miaka 18 nao wanatakiwa kuwa na kitambulisho hicho?

Nilitaka pia kujua kama kigezo cha mwombaji mjasiriamali au mwanafunzi aliyehitimu chuo au shule au mama wa nyumbani kuambiwa akalete barua ya mdhamini anayefanya kazi serikalini kipo kisheria?

Kwanini kuna aina flani ya ubaguzi kati ya ngozi nyeusi na nyeupe kwenye kupewa pasipoti? Watu wenye asili ya Asia na wale walio na ngozi flani hivi ya shombeshombe hawakataliwii pasipoti kwa kigezo cha kukosa barua ya udhamini wa mwajiriwa wa serikali ila sisi wa ukerewe na kyela lazima tuwe na barua hizi.

Lakini pia nimepitia sheria ya zamani ya pasipoti na kanuni zake nimeona inamatobo mengi sana ikiwemo kutotambua kitambulisho cha nida na wadhamini waajiriwa wa serikali.

Natambua kazi nzuri ya udhibiti inayofanya na Uhamiaji ila niwaombe watengeneze sheria na kanunu na wazisimamie siyo kutoa huduma kwa kuzingatia afisa anavyojisikia.

Naamini kwa umakini wa kamishna wa Uhamiaji lazima atafanya mapitio ya sheria anazofanyia kazi kwa haraka na kuzifanyia marekebisho.

Juzi nimekutana na afisa mmoja mkubwa ofisi za uhamiaji mkoa flani nikamuuliza haya maswali na kumwomba anipe sheria inayosimamia kutoa huduma alichonijibu ni kwamba hoja hizi zinqfanyiwa kazi huku akinipongeza kwa kuona huo mwanya wa mapungufu ya sheria.

Katika marekebisho hayo nadhani ni muda muafaka sasa kuweka kipengele cha adhabu kali kwa raia wa kigeni kujipatia pasipoti ya Tanzania kinyume cha sheria. Kukutwa na pasipoti ya Tanzania huku ukiwa ni mgeni iwe serious offence na isiwe na faini, kipengele kama hiki kitawafanya wageni wanaodanganya na kupata pasipoti zetu kuzikimbia.

Wapo jamaa karikoo wanafundisha watu mbinu za kupata pasipoti na wanatengeneza manyaraka na watu wanapata hivyo sheria iwe kali.

Nipongeze sana serikali kwa kuja pasipoti nzuri na yenye adhi za kimataifa, kila nikiishika nafarijika kwamba waafrika tunaweza kuishi maisha ya ulimwengu wa kwanza. Tusikubali wageni wakachafua jina zuri la Tanzania kwa kujipatia pasipoti zetuuuuuuuu na kwenda kuzifanyia mambo yasiyofaa.
 
Back
Top Bottom