Ipo tofauti gani kati ya Ubaguzi Afrika Kusini na ubaguzi na unyanyasaji, dhuluma dhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ipo tofauti gani kati ya Ubaguzi Afrika Kusini na ubaguzi na unyanyasaji, dhuluma dhi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by akili, Mar 18, 2010.

 1. a

  akili Member

  #1
  Mar 18, 2010
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nina hakika nchi za Kiafrika na Kiarabu kwa pamoja zikikataa kufanya biashara au kuwa na ushirikiano wowote na Wayahudi haitochukua muda suluhisho la serikali mbili, yaani, ile ya Kiyahudi na ile ya Kipalestina kuwa jambo linalowezekana.
  Afrika tusiamini kuwa ni Marekani itakayoleta mabadiliko huko Mashariki ya mbali. Tuamini kwamba ni Afrika kwa ushirikiano wake na nchi kama China, Brazili, Iran, India na Marekani ya Kusini na kati ndiyo dawa ya tatizo la Wapalestina. Hili linawezekana. Vijana wa Kiafrika waoneeni huruma Wapalestina wanaoishi kama watumwa na wahamiaji katika nchi yao wakati mvamizi kawa bwana na mmiliki na mwizi wa mchana wa ardhi na haki nyingine za Wapalestina.
  NINAZISHANGAA nchi nyingi za Kiafrika zilizokuwa mstari wa mbele kupinga ubaguzi wa rangi lakini leo nchi hizo hizo zimekaa kimya dhidi ya uuaji, unyanyasaji na dhuluma za Wayahudi dhidi ya Wapalestina.
  Hivi Umoja wa Afrika unaona kuna tofauti kati ya ubaguzi wa rangi na dhuluma dhidi ya Wapalestina zinazofanywa na Israili ikisaidiwa na mabwana kama sio mabibi zao Wamarekani?
   
Loading...