Ipo siku yako, endelea kupambana, mwisho wa kupambana ni pumzi yako inapoishia!!

kindikinyer leborosier

JF-Expert Member
Jan 6, 2018
430
780
Salam! hapa jamvini tumekuwa tunapeana matukio yetu ya kila siku, mapenzi mahusiano, matatizo nk.
.
.
leo nimeamka na hilinla kuwapa moyo wapambanaji wanaoelekea kukata tamaa na maisha haya, kuwa ipo siku yao, wanayoyapitia pengine ni funzo wanatakiwa walipate kwenye maisha!!
.
.
ni sahihi umemaliza chuo, huna kazi uliyotarajia, unawatazama wenzako wamefanikiwa, wanapost picha zao wakiwa na maisha tofauti kabisa na wewe, USIKATE TAMAA KUNA FUNZO UNAPEWA ENDELEA KUPAMBANA IPO SIKU.
.
.
upo single kijana wa kiume hujawahi kukaa na mahusiano hata mwaka mmoja, unaumia unahisi upo dunia ya kivyako vyako, ukiachana na mwanamke hamalizi miezi miwili, anatangaza uchumba, unaona wewe ndo ulikua na nuksi, kibaya anakujumuisha watsap group la michango, unajitutumua unamchangia asikuone unamwonea wivu bado, BADO USIKATE TAMAA IPO SIKU YAKO!!
.
.
Unatazama nyuma wadogo zako kiumri wanazidi kuovertake gari lako linalojikongoja na moshi mkali, unajiuliza umemkosea nini Mungu, usikate tamaa bado,, IPO SIKU YAKO, ENDELEA KUPAMBANA NA KUMHESHIMU MUNGU.
.
.
Unaanza kutengwa na marafiki zako, wanakuona huna chochote cha kuwasaidia, zaidi utakuwa wewe ndo mwenye kutaka msaada, HAYA YOTE NI YA KAWAIDA IPO SIKU YAKO!!
.
.
kila siku ukiwatazama wazazi ndita na nyuso zinazidi kujikunja kwa uzee, wakiwa na matumaini wewe ndie Musa wao, wewe mwenyewe ugali wako tu wa shida, ya leo bora ya jana, USIKATE TAMAA IPO SIKU YAKO, ENDELEA KUBISHA HODI ENDELEA KUKAZA IPO SIKU!!
.
.
Weekend njema!!
 
Hakika ipo siku yetu isiyokuwa na jina. Tuzidi kupambana
 
Back
Top Bottom