Ipo siku wapinzani watakubali ukweli kuwa CCM haina mbadala wake

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,220
9,647
Ndugu zangu Watanzania,

Siku yaja na miaka yaja ambapo wapinzani watakubali kuwa CCM ndio chama pekee kinachopaswa kuungwa mkono na kupewa ushirikiano katika kuliongoza taifa letu, watakubali kuwa Sera ajenda Dira na muelekeo wa CCm ndio sahihi na unatosha kutuvusha Watanzania kuelekea nchi ya Kanaan.

Watakubali kuwa CCM ndio moyo wa watanzania linapokuja suala la Imani juu ya chama, watakubali kuwa, vyama vyao ni SHIKIZI tu kwa ajili ya kujipatia ruzuku, watakubali tu wapo upinzani kutolea mawazo yao lakini linapokuja suala la kuikabidhi nchi mikononi mwa chama basi CCM ndio chama pekee kinachopaswa kupewa jukumu Hilo.

Hii ni kutokana na historia yake CCM ambayo huwezi ukaitenganisha CCM na historia ya taifa hili. Huwezi ukaizungumzia Tanzania bila kuiambatanisha na CCM, Tanzania ni CCM, ni sawa na mtu na ngozi, huwezi ukamchuna au kumtenganisha mtu na ngozi akabaki hai, CCM ndio Tanzania na Tanzania ndio CCM.

CCM imejizatiti kisawasawa linapokuja jambo lenye maslahi kwa taifa, hakuna kuyumba katika maslahi ya taifa, CCM inaweza ikabadilisha mbinu, mikakati, sera, ajenda, uongozi wa juu na ilani kuendana na wakati lakini maslahi ya taifa ni ya kudumu na yanayolindwa kwa jasho na damu kuhakikisha kuwa taifa letu linabaki lenye amani na tulivu.

Kazi hii nyeti huwezi hata kwa bahati mbaya kuwapa upinzani huu usio na muelekeo wala ajenda wala uchungu na nchi hii, ndio maana ni kawaida kusikia kiongozi wa upinzani akisimama jukwaani na kusema nchi hii haitatawalika au nchi itawaka moto.

Hii ni kwa kuwa hawana uchungu na nchi hii zaidi ya kujali matumbo yao, hawaoni hasara kuvuruga amani yetu, ndio maana hata watoto wao wana uraia wa nchi za kigeni, ndio maana hata uzalendo wao ni hafifu sana juu ya taifa letu. Ndio maana huwa wanazungumza chochote kinachokuja katika midomo yao, ndio maana Watanzania kuamua kuwapuuza na kuwadharau wao na vyama vyao vilivyokosa dira na muelekeo.

Kauli za aina hiyo huwezi ukazisikia hata kwa bahati mbaya zikitoka kwa kiongozi yeyote na wa ngazi yoyote wa CCm, kwa kuwa wanajuwa na Wana uchungu na taifa letu na wanajuwa dhamana waliyo nayo katika kulipigania taifa letu ikibidi hata kuhatarisha maisha kwa ajili ya kulilinda Taifa.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
Ndugu zangu Watanzania,

Siku yaja na miaka yaja ambapo wapinzani watakubali kuwa CCM ndio chama pekee kinachopaswa kuungwa mkono na kupewa ushirikiano katika kuliongoza taifa letu, watakubali kuwa Sera ajenda Dira na muelekeo wa CCm ndio sahihi na unatosha kutuvusha Watanzania kuelekea nchi ya Kanaan.
Naunga mkono hoja, na hili sisi wengine tuliisha lieleza humu kuwa CCM itatawala nchi hii milele! Kwasababu Tanzania tuna chama kimoja tuu cha ukweli cha siasa kwa maana halisi ya chama cha siasa ambacho ni the one and only CCM!. Huu ndio ukweli wenyewe Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!.
P
 
Naunga mkono hoja, na hili sisi wengine tuliisha lieleza humu kuwa CCM itatawala nchi hii milele!. Huu ndio ukweli wenyewe Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!.
P
Nashukuru Sana mkuu wangu kwa mchango wako ,Nashukuru Sana kwa makala zako zote humu jukwaani ambazo nilianza kuzisoma kwa miaka mingi kabla hata ya kujiunga Rasmi humu, Nikiri kuwa makala zako wewe pamoja na mzee mwana Kijiji nilikuwa nazifuatilia Sanaa katika jukwaa hili la siasa, japo wapo wengine ambao sijawataja
 
Ndugu zangu Watanzania,

Siku yaja na miaka yaja ambapo wapinzani watakubali kuwa CCM ndio chama pekee kinachopaswa kuungwa mkono na kupewa ushirikiano katika kuliongoza taifa letu, watakubali kuwa Sera ajenda Dira na muelekeo wa CCm ndio sahihi na unatosha kutuvusha Watanzania kuelekea nchi ya Kanaan.
Mazingira Kwanza ya uwanja wa kuchezea uwe sawa ndio maoni haya yaje tutakuwa na la kusemea ndugu yetu japo umesema vzr sana Sana nami nakubaliana nawe kbs
 
Ndugu zangu Watanzania,

Siku yaja na miaka yaja ambapo wapinzani watakubali kuwa CCM ndio chama pekee kinachopaswa kuungwa mkono na kupewa ushirikiano katika kuliongoza taifa letu, watakubali kuwa Sera ajenda Dira na muelekeo wa CCm ndio sahihi na unatosha kutuvusha Watanzania kuelekea nchi ya Kanaan.
Tafuta kazi ya kufanya mkuu

Unapoteza muda wako bure

Hakuna anayekuona hapa JF

Walikuwepo wengi sasa hata hawapost

Hakuna ajira rahisi hivyo
 
Pokea simu wewe mataga pori umepangiwa kituo cha kazi huko visiwa vya saa nane
🤣🤣🤣🤣 Mmeshindwa miaka yoote kumpigia mh Mbowe kumuuliza habari za Ruzuku na hela anazokikopeshaga chama bila hata ushahidi halafu unajifanya kutaka kuwapigia wa CCm? Embu niambie pesa za join the chain zilikwenda wapi? Zilipatikana shillingi ngapi? Maana naona Hadi makomandoo walikuwa wanamlinda mwenye kigoda asiibiwe hata Mia kwenye pakacha lake la kukusanyia hela mitaani
 
🤣🤣🤣🤣 Mmeshindwa miaka yoote kumpigia mh Mbowe kukuuliza habari za Ruzuku na hela anazokikopeshaga chama bila hata ushahidi halafu unajifanya kutaka kuwapigia wa CCm? Embu niambie pesa za join the chain zilikwenda wapi? Zikipatikana shillingi ngapi? Maana naona Hadi makomandoo walikuwa wanamlinda mwenye kigoda asiibiwe hata Mia kwenye pakacha lake la kukusanyia hela mitaani
Mataga pori umepanic mnoo hadi unamuwaza Mbowe muda wote kuliko hata unavyomuwaza mume wako.
Ila pokea simu yangu acha kulia-lia.
 
Naunga mkono hoja, na hili sisi wengine tuliisha lieleza humu kuwa CCM itatawala nchi hii milele! Kwasababu Tanzania tuna chama kimoja tuu cha ukweli cha siasa kwa maana halisi ya chama cha siasa ambacho ni the one and only CCM!. Huu ndio ukweli wenyewe Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!.
P
Sasa Pascal umebakiza miaka mingapi hapa Duniani?

Chukua umri wako Halafu weka benchi Mark ya uwezo wa Mtu kufikiri yaani miaka 95

Kumbuka hawa wanaofika miaka 95 ni kizazi cha miaka ya 1920_1930

Wewe uliyezaliwa miaka ya 1960 au 1970 ndio afya zenu hazina tofauti na Hawa wa 2000

Watatawala milele utakuwepo?

Au ndio mitano tena

Nasema mitano tena

Au ndio wale Mataga JPM forever
 
Misingi imara ya CCM ,mfumo Thabiti na madhubuti wa CCm,mizizi imara ya CCM,mtandao wa kiuongozi wa CCM na demokrasia Iliyopo Ndani ya CCM unaihakikishia CCM kuongoza miaka na miaka
 
Ndugu zangu Watanzania,

Siku yaja na miaka yaja ambapo wapinzani watakubali kuwa CCM ndio chama pekee kinachopaswa kuungwa mkono na kupewa ushirikiano katika kuliongoza taifa letu, watakubali kuwa Sera ajenda Dira na muelekeo wa CCm ndio sahihi na unatosha kutuvusha Watanzania kuelekea nchi ya Kanaan.
Hili litakuwa zao la shule za kata ndio maana joined 2022
 
Back
Top Bottom