Ipo siku walioshinikiza Sheria ya Habari watatamani ifutwe

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,304
6,509
Nafasi za uongozi husahaulisha. Hutokea mwenye cheo kudhani anaweza kudumu nacho hata kutunga au kushawishi utungwaji wa sheria kandamizi zenye kumlinda.

Rais wa kwanza wa Zambia, Kenneth Kaunda ‘KK’, aliposaini sheria zenye kumpa mamlaka ya kumweka kizuizini mtu yeyote, hakujua kuwa sheria hiyo inaweza kumgeuka, naye kuwekwa mahabusu.

Mwaka 1981, alipomweka mahabusu Fredrick Chiluba kwa mamlaka yake kama Rais wa Zambia, hakuwaza kama nyakati zijazo Chiluba huyo atakuwa Rais kisha naye atamfunga. Unahitaji hekima za kiuongozi kutambua kuwa dunia ni duara.

Baada ya Chiluba kushinda urais wa Zambia mwaka 1991, alitumia sheria zilezile zilizosainiwa na Kaunda kumsulubu kiongozi huyo wa kwanza mzalendo wa nchi hiyo. Hupaswi kutunga sheria kana kwamba wewe utafia madarakani.

Utunzi wa sheria hupaswa kuangalia maslahi mapana ya taifa. Wakati inapopitishwa, watunzi na anayesaini ni lazima wajiweke upande wa raia wa kawaida. Unajiuliza; kama nikiwa raia wa kawaida sheria hii itakuwa nzuri kwangu?

Kaunda hakuwaza hivyo, kwamba ipo siku atakuwa raia wa kawaida wa Zambia, mwenye heshima ya cheo cha Rais mstaafu peke yake. Angejiweka nafasi ya raia wa kawaida kisha kumfikiria Rais tofauti na yeye akijiamulia tu kumuweka mtu mahabusu kwa amri yake, bila shaka asingesaini sheria hiyo.

Hili ni tatizo ambalo huzitokea tawala nyingi duniani. Cheo ukishakuwa nacho kinaweza kukufanya usijione raia wa kawaida, unajiona ni tabaka maalum, kwa hiyo unakubaliana na sheria ambazo nyakati zikifika unazijutia.

Lowassa, Sumaye ni mfano

Tangu Uchaguzi Mkuu 1995, vyama vya upinzani vimekuwa vikilalamikia kuwepo kwa tume huru za uchaguzi. Kwamba zilizopo, Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hazikidhi viwango vya haki na demokrasia.

Fredrick Sumaye alikuwa Waziri Mkuu kuanzia mwaka 1995 mpaka 2005, kisha Edward Lowassa akawa Waziri Mkuu kuanzia mwaka 2006 mpaka 2008. Pitia vipindi vyote hivyo, Sumaye na Lowassa hawakujishughulisha na malalamiko hayo ya wapinzani.

Kimsingi Sumaye na Lowassa hawakuona kasoro za tume za uchaguzi kama ambavyo wapinzani walilalamikia. Ni kwa sababu matarajio yao waliyaelekeza kuamini kuwa ndoto zao za kisiasa zingetimia ndani ya CCM.

Kimbunga cha Uchaguzi Mkuu 2015, kiliwafanya Sumaye na Lowassa wajikute wapo upinzani kwenye Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Lowassa akawa mgombea urais wa Chadema, Sumaye akasimama kama meneja kampeni.

Matokeo yalipotoka na kuonesha Lowassa ameshindwa na Rais John Magufuli, ndipo hapo malalamiko kuhusu tume yakaibuka. Lowassa alimuunga mkono aliyekuwa mgombea urais wa Cuf Zanzibar, Seif Sharif Hamad kulalamikia matokeo ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka jana kufutwa.

Kimsingi mazingira ya tume ambayo Lowassa aliyakumbatia akiwa Waziri Mkuu ndiyo hayo ambayo alibadilika na kuyalalamikia. Kipindi akiwa kimya wapinzani wakilalamika, kama angewaza ipo siku atakuwa mpinzani, bila shaka angeshauri wapinzani wasikilizwe kuhusu madai yao ya tume huru.

Ukiweka pembeni hilo la tume, mwaka 2014 wakati wa mchakato wa Katiba Mpya ambayo tamati yake haifahamiki, Lowassa alikuwa mwana CCM aliyeshiriki umeng’enywaji wa rasimu ya Tume ya Jaji Joseph Warioba kisha kupatikana Katiba Inayopendekezwa kupitia Bunge Maalum la Katiba.

Baada ya kuenguliwa CCM, Lowassa hakuwa rafiki tena wa matokeo ya Bunge la Katiba lililoongozwa na hayati Samuel Sitta. Pengine Lowassa baada ya kuhamia Chadema alitamani muda urudi nyuma ili aitetee rasimu ya Katiba kama ilivyopendekezwa na tume ya Warioba lakini muda huo angeupata wapi? Ukiwa na nafasi tambua kuhusu leo na kesho.

Sheria ya Habari itawageuka

Ukiwa mtawala unaweza usione umuhimu vyombo vya habari kuwa huru. Inaweza kutokea ukaviona ni kiherehere, kwa hiyo ukatamani kuvidhibiti ili kurahisisha matakwa yako au maono yako ya kiuongozi.

Hata hivyo, ukiwa pembeni ndipo utaona umuhimu wa vyombo vya habari kuwa huru. Utaona mantiki ya waandishi wa habari kufanya kazi zao bila kuingiliwa na watawala. Ni eneo hilo ndilo ambalo linanifanya nibashiri kilio cha mashabiki wa Sheria ya Huduma za Habari 2016 siku za usoni.

Wenye taaluma yao walipaza sauti kuhusu uliokuwa muswada wa Huduma za Habari. Wenye kuifanya kazi hiyo, waliomba waongezewe muda japo miezi mitatu ili wajadili na kuondoa kasoro zilizobaki, lengo likiwa kuifanya Sheria ya Huduma za Habari 2016 iwe bora, yenye kuendana na wakati.

Sauti za wadau wa tasnia ya habari hazikusikilizwa. Wabunge wakajadili na kuupitisha muswada wa Huduma za Habari kisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Magufuli akaweka saini kuuthibitisha muswada huo kwamba sasa ni sheria kamili.

Ushauri kwa wadau ambao wameshika tama wakiwa na bumbuwazi kwa namna muswada ulivyopelekwa mpaka umekuwa sheria, wanapaswa kutabasamu huku wakivuta subira. Muda una kawaida wa kuwafanya walioanza na tabasamu wamalize kwa kilio, waliolia mwanzoni wakaishia kwenye kicheko.

Wapo watu ambao walishabikia upatikanaji wa Sheria ya Huduma za Habari inayolalamikiwa, miongoni mwao ni vijana tena wanaota ndoto kubwa. Nyakati zijazo yanaweza kutokea wakatamani kutimiza matarajio yao nje ya mazingira waliyonayo sasa.

Muda huo ukifika na kukutana na mtawala ambaye anatilia mkazo Sheria ya Huduma za Habari 2016, ndipo vilio vyao vitaanza kusikika. Mungu akinipa uhai na akanijalia uwezo wa kuendelea kuandika, nitaandika kuwakumbusha shangwe zao za 2016 kama ambavyo nawakumbusha Lowassa na Sumaye. Haitakuwa masimango bali kukumbushana.

Kama sitakuwepo au kama sitakuwa na uwezo wa kuandika kulingana na matakwa ya Mungu Mfalme, naamini watapatikana wengine wenye kumbukumbu na watakumbusha.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nnauye, siku akikutana na mgeuko wa kisiasa na kuwa nje ya mfumo, atatamani vyombo vya habari viwe huru bila kuingiliwa na Serikali. Akipiga kelele atakumbushwa: “Wewe ndiye ulikuwa jikoni na ulipika mwenyewe hiki chakula unacholalama kuwa kimeungwa mafuta ya taa.”

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba, ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii. Siku akiona nafasi yake ya kutimiza matarajio yake ya kisiasa ni nje ya mfumo, atageuka mtetezi wa uhuru wa vyombo vya habari. Muda huo ukifika atakumbushwa.

Inaweza kutokea hivyo maana ndivyo siasa huwa. Serukamba alikuwa mtu wa mstari wa mbele akimpigania Lowassa CCM, huku akiwa na matumaini makubwa kwamba watafuzu tiketi ya kuwa mgombea urais wa CCM kisha kushinda uchaguzi mwaka jana na kuchukua dola. Hata hivyo haikuwa. Leo Serukamba ni CCM, Lowassa yupo Chadema.

Nape na Serukamba ni mifano tu lakini ukweli ni kuwa watakaoililia Sheria ya Habari 2016 watakuwa wengi, hata wale wa chinichini. Waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari watazoea na kuitii sheria iliyopo, wanasiasa wenye kusaka madaraka ndiyo wataumia zaidi na watajuta ila watakumbushwa.

Mataifa mengine tasnia ya habari inapewa thamani kama mhimili wa nne wa dola baada ya Serikali, Bunge na Mahakama. Sheria ya Huduma za Habari 2016 Tanzania inazika ndoto hizo kwa Tanzania. Kivuli cha Serikali sasa kitaonekana hata kwenye vyombo vya habari vya watu binafsi. Hatukupaswa kabisa kufika huku.

Walikumbushwa waliotetea Ukuta wa Berlin

Wabunge wanapaswa kutunga sheria kwa kumtazama mwananchi wa kawaida. Rais pia awe na jicho hilo wakati anasaini muswada kuwa sheria. Wasiwe kama aliyekuwa Kiongozi wa Ujerumani Mashariki, Erich Honecker na watu wake.

Kutokana na maslahi ya kisiasa, Honecker akiwa Mkuu wa Usalama wa Chama cha Kikomunisti, Ujerumani, alisimamia ujengwaji wa Ukuta wa Berlin, lengo likiwa kuwatenganisha watu wa Ujerumani Mashariki na ndugu zao wa Ujerumani Magharibi.

Mwaka 1971, akawa Kiongozi wa Ujerumani Mashariki, hivyo kuendeleza maono yake ya kuwagawa Wajerumani pande mbili. Watu zaidi ya 200 waliuawa baada ya kubainika kutaka kuruka ukuta kwenda Ujerumani Magharibi.

Honecker alikuwa na mwisho mbaya baada ya kupinduliwa mwaka 1989. Alianza kuugua mfululizo hadi kifo chake mwaka 1994. Watu wake wa karibu kama Egon Krenz walijikuta wakisota jela na kuishi maisha ya hovyo baada ya Ukuta wa Berlin kubomolewa. Wapo waliojitokeza kuuponda Ukuta wa Berlin ila walikumbushwa: “Ninyi ndiyo mlikuwa vibaraka wa Honecker na sheria zake.”

CHANZO: Maandishi Genius
 
Haya ma ccm sijui yakoje yakishindwa kuni kura za maoni ya chama chao yanakimbilia huku ukawa na yanaanza kulaumu mfumo mfumo yakishindwa huko yakija kwetu tuyakatae
 
Nikiwaza yale maswali ya wanahabari kwa rais naona ni afadhali maana walitia aibu xana
 
umenena mkuu, wao wanajifkiria wao tuu baada ya uma time wil tel the truth
 
Kuna watu watakuja kupanda kizimbani wakiwa na umri wa miaka 80 au 90 kujibu tuhuma za Kivuko vibovu, EPA, KAGODA, RICHMOND,MEREMETA,LUGUMI,n.k

Ni swala la muda tu na Tanzania sio kisiwa na zaidi Mungu ni yule yule.

Tena yaweza tokeo Lema ndio akawa waziri wa mambo ya ndani wakati huo au Lissu ndio akawa Raisi wa nchi.
 
Historia huwa ni kurunzi pevu.hukupa mwanga wa kumbukumbu na dira ya kesho.Muda nao ni mwalimu mzuri asiye na upendeleo kwani kila mtu atapewa stahiki zake.
 
what a word,hongera kwa uzi wenye maono na unao fikirisha
Magufuli atalipa kila tendo analotenda leo, yeye na kizazi chake watalipa, yuko wapi Saddam na wanawe? Yupo wapi Mobutu na wanawe? Acheni atutese atutesavyo, lenye mwanzo lina mwisho.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom