Ipo siku tutamkumbuka Rais Dkt. Magufuli tunayemdhihaki kila siku katika mitandao ya kijamii

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,383
4,317
Kazi anazozifanya Rais Dr Magufuli kwa sasa ipo siku tutakuja kumkumbuka kwenye maisha yetu pamoja na dhihaka za kila siku ambazo inaandikwa katika mitandao ya kijamii.

Rais Dr John Magufuli ameikuta nchi ina nyufa kubwa sana sasa Rais ameanza kujenga msingi wa nyumba hapo lazima wanaoishi ktk hiyo nyumba watalalamika tu watapigwa na mvua, jua, watalala njaa, nk lakini ipo siku watamkumbuka tu kwa anayoyafanya leo.
 
Hiyo misingi ya nyumba inayojengwa sasa haikuwahi kuwepo? Kama ilikuwepo ni nani aliibomoa na kama haikuwepo ni nani alipaswa kuijenga na ni kwa nini haikujengwa?

Yaani miaka zaidi ya 56 ya Uhuru wa Tangayika na miaka zaidi ya 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ndiyo sasa misingi ya nchi hii inajengwa!?
 
Rais Dr John Magufuli ameikuta nchi ina nyufa kubwa sana sasa Rais ameanza kujenga msingi wa nyumba..
Nyie watu wa Lumumba jifunzeni kuandika kimantiki. Unaweza kuziba nyufa bila ya kubomoa nyumba, lakini huwezi kujenga upya msingi bila ya kubomoa nyumba ya awali kwanza. Kwa ivo ni wakati gani Magufuli aliibomoa hiyo nyumba?

hapo lazima wanaoishi ktk hiyo nyumba wanalalamika tu atapigwa na mvua, jua, watawala njaa, nk lakini ipo siku watamkumbuka tu kwa anayoyafanya leo.
Ulitaka kuandika nini kwenye hayo maelezo? Pamoja na makosa ya kisarufi lakini pia unataka kuonesha kwamba ni Magufuli peke yake ndiyo anaijenga Tanzania, na sisi wengine wote na wewe ukiwemo tumekaa tu hakuna tulifanyalo?
 
Kazi anazozifanya Rais Dr Magufuli kwa sasa ipo siku tutakuja kumkumbuka kwenye maisha yetu pamoja na dhihaka za kila siku ambazo inaandikwa ktk mitandao ya kijamii.

Rais Dr John Magufuli ameikuta nchi ina nyufa kubwa sana sasa Rais ameanza kujenga msingi wa nyumba hapo lazima wanaoishi ktk hiyo nyumba wanalalamika tu atapigwa na mvua, jua, watawala njaa, nk lakini ipo siku watamkumbuka tu kwa anayoyafanya leo.
Namuomba aachane na huu upinzani njaa.
Kumbe walizoea wakikohoa wanaitwa Ikulu kunywa chain, wasikanyage kabisa, na huku mtaani wajaribu kupanda jukwaani kumsema vibaya ndio watatujua sisi raia tunamchukuliaje president.

Wasituletee ukaskazini hapa
 
Uache kumkumbuka mama yako aliyepewa jukumu la kukuleta duniani, unaanza kumkumbuka Magufuli, kama sio ukichaa huo ni nini ?
wote wanakumbukwa tu kwanini Dr Magufuli asikumbukwe...
 
Hiyo misingi ya nyumba inayojengwa sasa haikuwahi kuwepo? Kama ilikuwepo ni nani aliibomoa na kama haikuwepo ni nani alipaswa kuijenga na ni kwa nini haikujengwa?

Yaani miaka zaidi ya 56 ya Uhuru wa Tangayika na miaka zaidi ya 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ndiyo sasa misingi ya nchi hii inajengwa!?
Nyufa kibao katika msingi wa nyumba ndugu.... Lazima msingi uimarishwe
 
kweli mimi nitamkumbuka maana kaharibu maisha ya watu wengi...
kuna familia wazazi wao wamelala mahabusu kisa chuki zake kwao...
kuna familia zimepoteza wapendwa wao kutokana na upuuzi wake....(kabwe)
kuna watu wameachishwa kazi kwa sababu ya ujinga wake
 
Sukar 5000/-?
IMG_20171102_194251.jpg
 
Kagera walipata tetemeko la ardhi zaidi ya raia 30 walipoteza maisha na wahanga wengine wakawa hawana mahala pa kuishi, akawambia kwamba yeye hakuleta tetemeko, ajabu nyumba za askali arusha ziliungua kwa moto faster akatoa pesa za kujenga nyumba nyingine za askali, kweli hatuwezi kusahau kiongozi mbaguzi.
Au kavunjia nyumba wakazi wa kimara hadi kibaha lkn mwanza akasema wasibomolewe kwakuwa ndio walimpa urais unadhani huyo tunaweza kumsahau?
 
Acha kusakama kabila la watu Wewe, kumbuka hao hao ndio mnategemea wawapatie kura. Wasipowapa hata wale nyumbu wakiwapiga kura hamuwafikii.

Sijataja kabila la mtu. Please no offence muhimu tambua hii ni nchi yetu sote

Ngosha ndie anaetegemea wasukuma wenzake, haukumsikia juzi akisema wao ndio waliompa urais?
 
Back
Top Bottom