Ipo siku tutamkumbuka Rais Dkt. Magufuli tunayemdhihaki kila siku katika mitandao ya kijamii

Atakumbukwa kwa mengi sana;
1. Kuminya demokrasia na kuzuia mikutano ya vyama pinzani.
2. Kufukuza watumishi wa umma wenye vyeti huku akimuacha Bashite anapeta.
3. Kudororesha uchumi wa nchi.
4. Watu kauwawa/kupotea na wengine kupigwa risasi hovyo hovyo.
5. Bomoa bomoa ya nyumba za wanyonge ilhali wengine wakiachwa kwa sababu walimpigia kura.
6. Kushindwa kuongeza mishahara na kupandisha madaraja watumishi wa umma kwa muda usiojulikana.
7. Ya Angela Kairuki, Ummy Mwalimu, Mnyarwanda na mdogo wake first lady.
8. Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
9. Hotuba zilizojaa chuki, visasi, mikwara na ubabe wa kizamani.
10. Elimu ya PhD isiyoeleweka wala kutambulika.
11. Na mengine mengi ya ajabu ajabu.
 
Kama watu wamemkumbuka J.kikwete senbuse Magufuli...

Hiyo ni lazma, watamkumbuka tuu... enzi hizo Rais sijui atakuwa Kigwangala
 
Kazi anazozifanya Rais Dr Magufuli kwa sasa ipo siku tutakuja kumkumbuka kwenye maisha yetu pamoja na dhihaka za kila siku ambazo inaandikwa ktk mitandao ya kijamii.

Rais Dr John Magufuli ameikuta nchi ina nyufa kubwa sana sasa Rais ameanza kujenga msingi wa nyumba hapo lazima wanaoishi ktk hiyo nyumba wanalalamika tu atapigwa na mvua, jua, watawala njaa, nk lakini ipo siku watamkumbuka tu kwa anayoyafanya leo.
Tumkumbuke nani, huyu Mzee wa Msiwabomoleshee??? My foot
 
Kazi anazozifanya Rais Dr Magufuli kwa sasa ipo siku tutakuja kumkumbuka kwenye maisha yetu pamoja na dhihaka za kila siku ambazo inaandikwa ktk mitandao ya kijamii.

Rais Dr John Magufuli ameikuta nchi ina nyufa kubwa sana sasa Rais ameanza kujenga msingi wa nyumba hapo lazima wanaoishi ktk hiyo nyumba wanalalamika tu atapigwa na mvua, jua, watawala njaa, nk lakini ipo siku watamkumbuka tu kwa anayoyafanya leo.
mm nilikua naishi kimara

seriuz ntaendelea kumkumbuka
 
Chama kinakufa mikononi mwake jk kilimkosakosa akakili hapo mwisho wa safari atazuia kwa risasi ila ukomo wake ni sasa subiri muda utimu
 
Ni kawaida kila kiongozi kukumbukwa kwa aliofanya kama watu waliomponda jk lakini sasa wanamkumbuka na kumsifia kuwa bora kuliko aliepo sasa, hivyo hivyo na kwa jk walisema bora mkapa na kwa mkapa walisema bora mwinyi na kwa mwinyi walisema bora Nyerere na kwa Nyerere walisema bora mkoloni. Kwa hiyo watu kumkumbuka aliepita kuwa alikuwa bora na alileta maendeleo ni jambo la kawaida na itaendelea kuwa hivyo siku zote lisikutishe. Ila ukweli wa mazuri na mabaya utabaki pale pale kumbuka ukipenda kusifiwa kubali na kukosolewa.asante
 
Ni kweli
 
Back
Top Bottom