Ipo siku tutainuka na kushangaza ulimwengu; Amka, acha visingizio, kwepa umasikini.

iMachange7

Member
Jun 19, 2016
58
32
*Mark Elliot Zuckerberg* ndiye mgunduzi wa Facebook na mmiliki wa Whatsapp. Mwezi huu wa May, 2017 jarida la Forbes lilimtaja kuwa tajiri namba 5 duniani, akiwa na utajiri unaofikia US$ 63.3 billion (Dola bilioni 63.3) sawa na Trillioni 139.26 za kitanzania.

Unafikiria nini? Zuckerberg ni mkubwa sana? Hapana, amezaliwa May 14, 1984 kwahiyo May mwaka huu wakati anatangazwa tajiri namba 5 ulimwenguni ana miaka 33 tu. Bado unashangaa??!!

Ngoja nikujuze, wakati anataka kuanzisha Facebook, akiwa bado na wazo kichwani (wakati huo yuko chuo Harvad mwaka 2004), aliwafuata wanachuo wenzake wengi sana kuwaeleza anachotaka kufanya. Wengi sana walichomoa. Hawakumuunga mkono. Zuckerberg hakukata tamaa akawashirikisha watu wengi zaidi, mwishoni akaungwa mkono na roommate wake wanne ambao ni:
*1. Eduardo Saverin* ambaye ana utajiri wa US$ 7.2 billion sawa na trillioni 15.84. Eduardo alifanya kazi facebook miaka mitatu tu 2004-2007 akaenda kufanya mambo yake mengine.

*2. Andrew McCollum* ambaye pia hakufanya kazi sana facebook akarudi zake Harvad kusoma degree ya Computer Science na baadae akasoma Masters ya ualimu.
Ni mmoja kati ya wanataaluma wa Harvad na mwalimu tajiri zaidi pale Harvad.

*3. Dustin Moskovitz*
Kijana anayemiliki utajiri wa US$ 10.4 billioni, sawa na trillioni 22.88 za kitanzania.
March 2011, alitajwa kuwa ndiye billionea mdogo zaidi katika historia katika kipengele cha “utajiri aliojitengenezea mwenyewe” (youngest self-made billionaire in history). Na bado hii Facebook analipwa share ya 2.34% katika mapato yote.

*4. Chris Hughes*
Kijana mdogo ambaye mwaka 2015 utajiri wake ulitajwa kuwa US$ 450 millioni, sawa na billioni 990 za kitanzania. Huyu ndiye aliyetoa wazo kuwa facebook isitumike tu Harvad itoke na shule zingine na vyuo vingine. Na hii ndo ikawa sababu ya facebook kuenea dunia nzima.

Umewaona hao watu wanne waliokubaliana na Zuckerberg kuhusu wazo lake la facebook?? Umewaona watu wanaochangamkia fursa walipofikia?
Wewe uko wapi?
Hebu wafikirie wale wanachuo kibao ambao walifuatwa na Zuckerberg kuhusu wazo lake wakachomoa!, Kwa sasa wanajisikiaje? Ni kweli hawajuti!?

Wewe pia umekua ukishirikishwa fursa kibao, na bado unatoa visingizio tele bila kuifahamu vizuri fursa yenyewe.

Amka, acha visingizio, kwepa umasikini.


Yamkini hata sasa unasoma ujumbe huu na bado unajiambia kuwa hauwezi kufanya chochote na hauwezi kufanikiwa. Hio si sawa...!!
 
Hizo fursa zingine hazina maana zitatutengenezea uadui na ndugu na jamaa zetu. Hasa hayo mafursa yenu ambayo yanaonesha wazi ni ya Pyramid schemes. Hizo ni Scam za kutosha. Nishirikishe fursa ambayo hata mtoto wa la saba itamwingia akilini. Vitu kuweka hela rahisi afu kutoa ni ishu unanambia ni fursa. Damn it!
 
Acha kukaa unatoa mifano ya waliofanikiwa wakati wewe unaganga, na mwisho wa siku unawashirikisha watu "fursa" ya kuuza bidhaa za trevo...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom