Ipo siku Spika ataahirisha bunge kwa Mahudhurio hafifu ya wabunge! CCM wabunge wake si makini

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Kwa hakika yale maneno yasemwayo sana mitaani kua "Upinzani ndio bunge, na bunge ni upinzani" hii ina maana ya kwamba hakuna bunge bila upinzani. Mwenendo wa bunge la sasa kimahudhurio si mzuri!


Ni wazi kabisa baada ya wabunge wa upinzani kuamua kutoka na kutohudhuria vikao vyote vya bunge endapo anayeongiza ni Naibu spika Tulia Acksoni kwa sababu ya kutokutumia mizania sawa kutoka pande zote wakati wa mijadala, bunge zima limebaki na wabunge wa chama kimoja cha CCM! sasa nao wengi wanaonekana kutohudhuria vikao kwa sababu zao binafsi na wengine kwa majukumu ya kazi za kiserikali hasa mawaziri.

Japo kwenye suala la posho linawahusu wale wa upinzani lakini hawa wa CCM hata kama hawapo lakini posho wanalipwa tu. Maana "mkuki mtamu kwa nguruwe ila kwa binadamu mchungu"


Imethibitika kua sasa mahudhurio ya wabunge wa CCM ni hafifu sana, wengi hawapo bungeni na imeonesha wazi wazi kabisa pasina shaka kua wabunge wa upinzani pekee ndio waliokua wakihudhuria vikao vyote vya bunge pamoja na uchache wao ili kuhakikisha kua wanaisimamia serikali ipasavyo. Hali ya kutokuwepo bungeni kwa wabunge wa upinzani imeoekana ni pengo na pigo kubwa sana kwa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ambapo kwa sasa taswira yake halisi kwa sasa inafifia. Sijui ni kwanini huyu Naibu Spika hashtuki na halionei taifa uchungu.

Kuna uwezekano kabisa siku moja Naibu Spika akaahirisha kikao kwa sababu ya uchache wa wabunge waliopo ndani ya ukumbi, kuna uwezekano akatoa sababu nyingine kabisa ya kuahirisha kikao kwa kuogopa kuwaumbua wabunge wa CCM lakini tatizo likawa wazi kabisa.


Bunge bila ya LISSU,Zitto, Mnyika,Mdee,Maiko,Bulaya,Heche, Kubenea,Pareso, Gekulu sio bunge kabisa hata dunia nzima inatambua.
 
Hivi huyo spika hakuna siku ya kuwaachia wenyeviti ili wapinzani waingie. Naona karibu siku zote anaongoza yeye ili watoke. Mama siku moja ikiwezekana mpe mwenyekiti wa bunge aongoze ili tupate ladha ya upinzani.
 
Wabunge wa CCM na Serikali yao wameamua kuikimbia nuru iletayo uzima na kukimbilia giza la mwovu shetani ambalo kwalo limeja fadhaa na machukizo yote ya dunia. Walifikiri kwa kuamua kwao kujifungia na kuwanyima wananchi uhuru wa kuona na kuchambua kile kinachofanywa na wabunge ndani ya vikao vyao ndiyo itawapa fursa ya kupitisha madudu yao na kuilinda Serikali lakini mwisho wa siku hiyo dhambi na dhuluma wanayolifanyia taifa hakika itawageuka na kuwatafuna maisha yao yote.

SERIKALI INAYOOGOPA KUKOSOLEWA NA KUFANYA MAMBO YAKE KWA KIFICHO INADHULUMU HAKI YA WANANCHI WANAOKAMULIWA KILA UCHAO KWA KODI AMBAZO HUTUMIKA KUGHARAMIA UDHALIMU HUO.
 
Hata zile siku hatari anakomaa tuu......njaa mbaya! Ana fadhila huyo bi kiroboto Jr mbona inajulikana!!!

Hivi huyo spika hakuna siku ya kuwaachia wenyeviti ili wapinzani waingie. Naona karibu siku zote anaongoza yeye ili watoke. Mama siku moja ikiwezekana mpe mwenyekiti wa bunge aongoze ili tupate ladha ya upinzani.
 
Bunge ladoda, wabunge 85 wajadili bajeti



Na Arodia Peter, Dodoma

BUNGE la bajeti linaloendelea mjini Dodoma, jana limehudhuriwa na wabunge 85 badala ya 277 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya wenzao wa Kambi ya Upinzani kususa vikao vinavyoendeshwa na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson kwa madai kuwa hawana imani naye.

Kwa wiki ya pili sasa wabunge hao wanaotokana na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) huingia bungeni asubuhi na kutoka baada ya dua ya kuliombea Bunge hivyo kuwaacha wale wa CCM wakiendelea na mjadala wa bajeti peke yao.

Bunge la Jamhuri ya Muungano lina jumla wa wabunge 395, kati yao 118 ni kutoka vyama vya upinzani na 277 ni wa CCM wakiwamo wateule wa rais.

Katika mkutano huo wa tatu, kikao cha 43 cha Bunge la bajeti kilichoendelea jana, karibu robo tatu ya wabunge wa CCM hawakuwamo ukumbini huku wachangiaji walio wengi wakirudia michango ya wenzao waliotangulia.

Baadhi ya wabunge wa CCM waliozungumza na MTANZANIA kwa masharti ya kutotajwa majina gazetini, walisema kutokuwapo kwa wabunge wa upinzani katika mjadala wa bajeti kumesababisha Bunge hilo kupooza na kukosa msisimko wa hoja.

“Sitaki unitaje kwenye chombo chako, lakini wale wenzetu tumewa-miss, michango yao mara nyingi inalifanya Bunge kuwa hai zaidi, sifurahii hawa jamaa kukaa nje ya Bunge,” alisema.

Mbunge mwingine wa CCM kutoka mkoani Singida, alisema kabla hajaingia bungeni alikuwa anatamani kujenga hoja kama za Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), hivyo kukosekana kwake kunamkosesha fursa ya kujifunza kutoka kwake.

Wakati hali ikiwa hivyo, juzi Mbunge wa Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwanko alimshauri Naibu Spika, Dk. Tulia pamoja na wabunge wa Ukawa kukaa chini na kumaliza tofauti zao ili kuweka taswira nzuri ya Bunge.

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa alipoulizwa wanajisikiaje kuwa nje ya Bunge wakati wa kipindi hiki muhimu cha bajeti ya taifa, alisema ngoja CCM waendelee peke yao kwani hawaoni umuhimu wao.
 
Ni ukweli kabisa,na hata ndani ya hao wabunge wa CCM hawapendi mwenendo wa Tulia ila kwa uwoga wao wanshindwa kusema.

Nsazugwanko alijitahidi kuongea kwa kutumia hekima ya utu uzima lakini binti majivuni kwa kutokuwa na hekima hakumuelewa,anadhani anawakomoa wapinzani kumbe anajikomoa mwenyewe na Taifa.Hajui kwamba hamsaidii Rais na usikute hata Rais anajutia uteuzi wake.

Na kwa kawaida muda ni dawa.
 
nimecheka sana pale niliposoma kwamba hata zile siku za hatari NS anakomaa tu,kuendesha bunge kana kwamba hakuna wasaidizi wake
 
Muda wa kudekezana umepita, nchi haiwezi kusimama kusubiria wasiotaka watake. Kule zanzibar baraza litakuwa halina upinzani kwa miaka 5 na bado mambo yataenda sembuse hawa wanaogomea baadhi ya vikao.

Mgomo ambao hauwezi kuleta madhara kwenye utendaji wa bunge, Mgomo huo hauna maana.

Dr Slaa aliposusa Mbowe alisema chama haiwezi kukaa kusubiria mtu mmoja. Acha ajitafakari akirudi atatukuta mbele ya safari. The same bungeni acha ukawa watafakari wakiamua kurudi watalikuta bunge mbele ya safari.
 
kiujumla ukawa walijitaidi sana kuchangamsha bunge. wabunge wa ccm wengi huingia bungeni kwa ajili ya posho. lakini hakuna siku ambayo hili bunge litahairishwa kwa uchache wa wabunge kamwe. hili ni bunge la posho....
 
Naibu spika alikua na fulsa pana ya kujijenga kisiasa kwa Kwakua yeye ametokea kwenye uteuzi badala yake kaamua kuwa one sided. She was supposed to play smart and earn credit both sides from her perfomance but ndo hivyo kashindwa kuwa mediator.
 
Chata vikao vya chama vinaweza fanyika humo humo maana wamebakia wenyewe
 
Wabunge wa CCM na Serikali yao wameamua kuikimbia nuru iletayo uzima na kukimbilia giza la mwovu shetani ambalo kwalo limeja fadhaa na machukizo yote ya dunia. Walifikiri kwa kuamua kwao kujifungia na kuwanyima wananchi uhuru wa kuona na kuchambua kile kinachofanywa na wabunge ndani ya vikao vyao ndiyo itawapa fursa ya kupitisha madudu yao na kuilinda Serikali lakini mwisho wa siku hiyo dhambi na dhuluma wanayolifanyia taifa hakika itawageuka na kuwatafuna maisha yao yote.

SERIKALI INAYOOGOPA KUKOSOLEWA NA KUFANYA MAMBO YAKE KWA KIFICHO INADHULUMU HAKI YA WANANCHI WANAOKAMULIWA KILA UCHAO KWA KODI AMBAZO HUTUMIKA KUGHARAMIA UDHALIMU HUO.
Absolutely
 
Back
Top Bottom