Ipo Siku mtaelewa Umuhimu wa hizi Tozo

Matumizi ya TOZO yameshaonekana, kulipa mikopo ya chanjo, uhamasishaji chanjo, usambazaji chanjo, uanzishwaji wa vituo vya chanjo, kulipia matangazo ya chanjo, kulipa watumishi wa chanjo, chanjo , chanjo .........x1000
Hapo hela za wahisani kwaajili ya covid zinakua zinanunua mafuta ya viete sio maana zingine mwendazake alishakula 🤣🤣 Tanzania ngumu hii
 
Kulalamika ni hali ya asili, mbali ya kuwa nin haki yetu, kama unaumia utakaa kimya kwa sababu wajua maana? Kama yey ajua tunapokweda muache atupeleke,
 
Usifikiri hii nchi imejaa wajinga km bado mnafikiria
Pesa ya kununua ndege, ipo tena cash ila ya kujenga vituo vya afya inatoka kwenye Tozo.
Ipo wapi gesi ya Mtwara? Leo gesi bei juu.
Kwahiyo hii nchi inapata maendeleo kwasababu ya tozo?
Aiseee
Vipi kuhusu hela za utalii, madini, kodi na hela ya ATCL zinafanya nini?
Mtadanganya wajinga ila wenye akili wanawaona ni weupe tu vichwani.
Ukituma pesa tozo, ukitoa tozo, umeme tozo bado maji ila kuajiri na kuongeza mishahara hamtaki.
Mama ni Kazi tuu,maneno achia Chadema na mataga wa legacy 👇

View attachment 1942324
 
Tozo sikatai ila tozo ziangalie na vipato vya wananchi.
Huyu mwananchi anambembesha mzigo mzito wa tozo zisizo na maana.
Leo ukituma elfu 70,000 unakatwa km 3000 hivi halafu ukitoa unakatwa tena utafikiri watu wanachimba pesa au wananchi wanapesa nyingi sana.
Ajira hawatoi hata Paypal wanabana.
Tozo zina umuhimu ila nafikiri ingependeza wangesema kuwa tunahitaji kukusanya kiasi kadhaa mf: shs trilioni tatu, kwa ajili a kufanya abcd hivyo mtuvulie kwa miaka ...hivi
 
Bajeti iliyotengwa 2020/2021 ni zaidi ya shillings 33t ambapo pesa ya matumizi ya kawaida ni zaidi ya shillings 20t na pesa ya maendeleo ni zaidi ya shillings 13t na bado haiendi yote, maana yake 70% ya bajeti ni kwaajili ya posho, mishahara,mafuta etc na 30% ndio barabara,zahanati,shule, maji etc ambazo hazifiki zote kwenye miradi. Kazi iendelee miaka 60 ya uhuru
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Tatizo la nchi hii sio MAPATO ila tatizo ni MATUMIZI, Kuna mianya mingi ya mapato lakini bado haijatumika sawa sawa kabla hatujafika kwenye double taxation na tozo kandamizi pia kwenye matumizi huko ndio shida kabisa maana matumizi makubwa sio yale yanayogusa maendeleo ya mwananchi kulingana na vipaumbele vya kijinga ie unaenda kuongeza ndege kwa cash kwenye shirika linaloendeshwa kwa hasara badala ya kuongeza uwezo kwenye miradi inayogusa wananchi mojakwamoja kama maji,umeme,barabara etc
 
Ndio ukweli huo kwa sababu shughuli za utawala ni muhimu na za lazima kuweka stability ya Nchi,bila usalama hakuna maendeleo..

Pia unapo analyse hiyo bajeti usikariri ,kwa mfano kulipia elimu bure,mikopo ya wanafunzi,madawa hospital,watumishi let say wa Afya na Usalama vyote vinaingia kwenye utawala lakini ni uwekezaji ambao haukupi tija kwa mda mfupi.

Hata hivyo hiyo 13% ni hatua kubwa Sana.
 
Ipo siku mtaelewa umuhimu wa hizi Tozo Kwa Mambo yatakayo fanyika mbeleni
Mkuu ni Mtanzania gani mgeni wa kulipa Kodi ?, Mbona ma-VAT, Income Tax, Duty, Witholding n.k. watu tumekuwa tukitoa kila siku ? Hakuna mtanzania mlaji ambaye hajawahi au halipi Kodi
Mama Samia ana nia nzuri sana na hii Nchi Mda ndo utatoa majibu pekee
Tutapata shida kwa kipindi hiki ila Miaka Ijayo hayo yote yatabaki story
Miaka ijayo ipi ?, Watu walikuwa wanakula mlo mmoja kwa siku huenda sasa hivi ni mmoja kwa siku mbili, unadhani hiyo miaka ijayo wataenjoy au watakuwa wanatibu magonjwa ya vidonda vya tumbo?
Tuwe na Subra tusiwe watu wa Lawama Mda wote Serikali inajua nini inafanya na ina Malengo gani,
Serikali inajua wananchi hawajui ? Ni wajibu wa walipa Kodi kulalamika kama wanaona mambo hayaendi sawa, pia wanaruhusiwa kuchangia ukizingatia waliopo madarakani ni watumishi wa waliopo mtaani
Sisi watanzania tumekuwa Wepesi sana Kulalamika without Reasoning ila Tozo zitafanya Mambo makubwa huko mbeleni ndo mtaelewa umuhimu wake
Kama wanashindwa kutueleza tukaelewa basi hawajui / hawawezi kazi yao...
Tusipende kuwa Negative kwenye kila kitu tusubiri Matokeo yake ndipo tuanze kulalama

.Tuendelee kula Dagaa ipo Siku hizo Dagaa Zitabaki Historia Wakati Tukila Kuku na Maisha Yakienda Fresh
Usubiri matokeo alafu ndio ulalamike ?, unapimaje hayo matokeo miaka 100 au elfu moja? Hivi unajua bei ya dagaa mkuu ?, Watu hata dagaa wanazitavuta hawazioni kwao hata uhakika wa matibabu, mkono kwenda kinywani na kulala kama binadamu na sio nguruwe itakuwa tosha... By the way Wananchi wote wangebana mkanda hakuna ambaye angelalamika ila inaonekana mkanda huu ni wa wachache watoa tozo na sio watoza tozo
 
Tatizo la nchi hii sio MAPATO ila tatizo ni MATUMIZI, Kuna mianya mingi ya mapato lakini bado haijatumika sawa sawa kabla hatujafika kwenye double taxation na tozo kandamizi pia kwenye matumizi huko ndio shida kabisa maana matumizi makubwa sio yale yanayogusa maendeleo ya mwananchi kulingana na vipaumbele vya kijinga ie unaenda kuongeza ndege kwa cash kwenye shirika linaloendeshwa kwa hasara badala ya kuongeza uwezo kwenye miradi inayogusa wananchi mojakwamoja kama maji,umeme,barabara etc
Hapo waulizwe wenye serikali
 
Tozo sikatai ila tozo ziangalie na vipato vya wananchi.
Huyu mwananchi anambembesha mzigo mzito wa tozo zisizo na maana.
Leo ukituma elfu 70,000 unakatwa km 3000 hivi halafu ukitoa unakatwa tena utafikiri watu wanachimba pesa au wananchi wanapesa nyingi sana.
Ajira hawatoi hata Paypal wanabana.
Nyie walalamishi nadhani ni vijana wa miaka ya karibuni hamjui kodi za kichwa wala ada za shule..

Tozo unazolia Lia hapa hulazimishwi kulipa,hutumii mitandao kila siku Sasa hizi kelele sijui ni za nini hasaa.
 
Ndio ukweli huo kwa sababu shughuli za utawala ni muhimu na za lazima kuweka stability ya Nchi,bila usalama hakuna maendeleo..

Pia unapo analyse hiyo bajeti usikariri ,kwa mfano kulipia elimu bure,mikopo ya wanafunzi,madawa hospital,watumishi let say wa Afya na Usalama vyote vinaingia kwenye utawala lakini ni uwekezaji ambao haukupi tija kwa mda mfupi.

Hata hivyo hiyo 13% ni hatua kubwa Sana.
Sawasawa buraza ndio maana wanaopenda kuzindua miradi zinaenda viete zaidi ya ishirini zenye watu wanaolipwa posho na per diem, yaani wanaenda kuzindua mradi wa shillings 400m gharama ya uzinduzi shillings 200m 🤣🤣 hizi nguruwe bwana akili zao hazina akili
Screenshot_20210917-205614_1.jpg

Kwaiyo ndio wamewajaza mje kutetea ushubwada watanzania sio wajinga
 
Ipo siku mtaelewa umuhimu wa hizi Tozo Kwa Mambo yatakayo fanyika mbeleni
Mama Samia ana nia nzuri sana na hii Nchi Mda ndo utatoa majibu pekee
Tutapata shida kwa kipindi hiki ila Miaka Ijayo hayo yote yatabaki story

Tuwe na Subra tusiwe watu wa Lawama Mda wote Serikali inajua nini inafanya na ina Malengo gani,

Sisi watanzania tumekuwa Wepesi sana Kulalamika without Reasoning ila Tozo zitafanya Mambo makubwa huko mbeleni ndo mtaelewa umuhimu wake
Tusipende kuwa Negative kwenye kila kitu tusubiri Matokeo yake ndipo tuanze kulalama

.Tuendelee kula Dagaa ipo Siku hizo Dagaa Zitabaki Historia Wakati Tukila Kuku na Maisha Yakienda Fresh
Hizi story tushazizoea. Nchi wameshindwa kuijenga kwa rasilimali kama.dhahabu, ruby, tanzanite, diamond, chuma, coal, bandari, bahari ndo waje waijenge kwa tozo?????
 
Sawasawa buraza ndio maana wanaopenda kuzindua miradi zinaenda viete zaidi ya ishirini zenye watu wanaolipwa posho na per diem, yaani wanaenda kuzindua mradi wa shillings 400m gharama ya uzinduzi shillings 200m 🤣🤣 hizi nguruwe bwana akili zao hazina akili View attachment 1942344
Kwaiyo ndio wamewajaza mje kutetea ushubwada watanzania sio wajinga
Unajikuta una akili kumbe mburula tuu usiyejitambua..
 
Mtoa uzi either hajielewi au ana ujinga kichwani. Hivi unawezaje kuweka matozo yote haya ingali mtumishi wako wa umma hujamuongezea chochote ndani ya miaka mitano huu wa sita? Yan hata kile kidogo ambacho anakipata serikali inakinyakua. HII SIO SAWA.
 
Wameshaelewa mbona,bado machadema na mke wao wa kambo wazee wa legacy almaarufu sukuma gang..

Kama kuna mtu anategemea eti tozo zitakuja kuondolewa uchaguzi ukikaribia akaote vizuri,hicho ni chanzo endelevu cha mapato na kinaonesha tija tayari..

Mfano tumeshaacha kuchangishwa michango ya kujenga shule,kuagizwa madawati na upuuzi kama huo..

Ndani ya miaka 5 ya Tozo zaidi ya vituo vya afya 700 vitajengwa,haya ni mapinduzi makubwa kwenye sekta ya Afya Tzn..

Na Ili kukabiliana na upungue wa watoa huduma ndio maana serikali imekuja na muongozo wa kuajiri watu kwa mkataba/ kujitolea
You must be dreaming. Stop living in a PIMPERS PARADISE.
 
Hapo hela za wahisani kwaajili ya covid zinakua zinanunua mafuta ya viete sio maana zingine mwendazake alishakula 🤣🤣 Tanzania ngumu hii
Zile pesa si hisani, ni mikopo ya ‘masharti nafuu’, tutalipa yote na riba juu kupitia hizi tozo
 
Zile pesa si hisani, ni mikopo ya ‘masharti nafuu’, tutalipa yote na riba juu kupitia hizi tozo
Mbona Kama Kuna dalili ya ufisadi hapo ie wakati wanasema ni tozo za mshikamano kwaajili ya kujenga barabara na zahanati kule bungeni hao IMF walikua hawajaridhia kutoa huo mkopo wa kupambana na covid,hela ya IMF imetoka tena mnasema hizi tozo ndio zitakazo tumika kulipia mkopo. Ndio maana Tanzania tatizo sio mapato ila Kuna mianya mingi pesa zinavuja na kuliwa na watu wachache kwa visingizia Kama hivi
 
Back
Top Bottom