Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,013
- 144,371
Hili wazo nimekuwa nalo kwa muda mrefu na limekuwa likinijia na kupotea na leo tena limenijia hivyo nimeona bora nililete hapa ku-share na wengine.
Ni hivi,hisia zangu zinanionyesha kwamba, ipo siku Tundu Lissu huyu wanaemnyima haki yake ya matibabu,atakuwa kwenye ofisi kubwa ambapo watesi wake watalazimika kusubiri idhini yake wakatibiwe nje ya nchi kama sehemu ya formalities.
Hata kama sahihi yake itakuwa sio takwa la kilazma kisheria,lakini kwa nafasi atakayokuwa nayo wakati huo,anaweza kutumia madaraka kufanya hiki anachofanyiwa leo ila naamini yeye hatalipiza bali itakuwa ni somo tosha kwa watesi wake kuwa maisha yanabadilika na madaraka ni ya kupita tu.
Tundu Lissu anaweza kufika hapo kwa wakati tusioujua na kupitia chama chake cha sasa,chama tofautI au hata kupitia muungano wa vyama vya siasa utakaoundwa wakati huo.
Vile vile sio lazima awe mkulu wakati haya yanatimia, bali anaweza pia kuwa ndio waziri mwenye dhamana na matibabu ya watu wakiwemo watesi wake wa leo.
Kupona kwa Lissu katika mazingira yale si kwa hivi hivi tu, balI nina amini Mungu ana makusudio yake juu ya mtu huyu na kupitia kwa Lissu, atatoa somo kubwa kwa wanadamu hawa waliopewa madaraka na wanayatumia vivyo sivyo
Hifadhi hii thread.