Ipo siku familia za viongozi zitahamia bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ipo siku familia za viongozi zitahamia bungeni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kmp, Aug 10, 2010.

 1. kmp

  kmp Member

  #1
  Aug 10, 2010
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kinyang’anyiro cha kuwania ubunge kinachoendelea ndani ya CCM kimeibua mengi yakiwapo rushwa iliyokithiri pamoja na watoto wa vigogo kuamua kuwafuata wazazi wao ndani ya uongozi.

  Kuna idadi kubwa safari hii ya watoto wa viongozi wa juu wa serikali na chama hicho ambao wameamua kugombea ubunge kupitia majimbo na viti maalmu.Mbali ya hilo wapo pia watoto wa vigogo hao ambao wameamua kugombea uongozi ndani ya chama hicho ili kijiwekea mazingira ya baadae kuwa viongozi wa juu wa chama hicho au kuwania ubunge.
  Baadhi ya watoto hao walioamua kuwania nafasi ya uongozi ni mototo wa tatu wa waziri mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda, Fortunata (26) ambaye ameibuka kidedea katika kura za kuteuliwa kuwakilisha UVCCM katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitokea mkoa mpya wa Katavi.

  Fortunata Pinda ambaye ni mtumishi wa Serikali akiwa ofisa katika ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma amechaguliwa katika mkutano wa Makamanda wa UVCCM uliofanyika Dodoma.

  Mwingine ni mototo wa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, anaitwa January ambaye ameshinda kura za maoni katika jimbo la Bumbuli.
  Waliopo katika nyadhifa za kisiasa mpaka sasa ni mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhwan ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Uchumi ya UVCCM. Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete ni Mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCMTaifa kutokea mkoa wa Lindi.
  Wakati mama akiwa mjumbe wa mkutano mkuu, mtoto wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM ), Rais Jakaya Kiwete, Khalfani Kikwete (11) ni Mjumbe wa baraza Kuu la Chipukizi Taifa Tanzania Bara.

  Mtoto wa mweka hazina wa CCM, Amos Makala hivi karinuni alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chipukizi taifa, huku mkoani Morogoro, mtoto wa aliyekuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Lucy Nkya, Jonas Nkya, akishikilia wadhifa wa Mwenyekiti wa Mkoa UVCCM.

  Labda nieleweke mapema kwamba hakuna mtu anayepinga watoto wa vigogo na familia zao wasigombee nyadhifa za juu za uongozi wa nchi au hawana haki.
  Ila ukweli ni kwamba wanapogombea wakati wazazi bado wapo kwenye nafasi zao kunakuwa na ziada ya kupata usaidiziu kutokana na majina ya wazazi wao.

  Sio siri kwa mwendo huu wa kasi wa watoto wa vigogokuingia katika nyadhifa za chama na serikali kuna siku familia nzima kuanzia mtoto wa kwanza mpaka wa mwisho wakawa bungeni siku zijazo.Sio ajabu kabisa baba akawa waziri na naibu wake kama mkewe au mwanae. Hapa uwajibikaji utakuwepo?
  Nitachotaka kueleza ni kwamba haki ya watoto hawa kugombea nafasi hizo wanayo na hilo wala halina mjadala, lakini nafasi za baba zao na mama zao zinawabeba.

  Nadhani sasa watanzania tunatakiwa kufuata mfano wa Baba wa Taaifa, Mwl. Julius Nyerere ambaye pamoja na kuishi ikulu kwa miaka 25, hakuwasaidia kuwabeba watoto wake kuwapeleka juu hata kidogo.
  Mwalimu Nyerere hakugeuza siasa kuwa ni mtaji wake wa kutajirikia kwamba familia yake yote iingie serikalini au bungeni kwa manufaa yake.

  Watoto wa Mwalimu waliingia katika siasa baada ya baba yao kuondoka ikulu. Sio kwamba hakuwa na watoto ambao walistahili kuwa wenyeviti wa chipukizi taifa, UVCCM taifa au kuwa mawaziri. Alijua kwamba kuingiza familia nzima katika uongozi kunaweza kumfanya ashindwe kuwatendea haki wananchi wengine.Ni kutokana na hali hiyo ndio maana hata mwanawe, Charles Makongoro mwaka 1995 aliibuka na kujiunga na chama cha NCCR Mageuzi akagombea ubunge jimbo la Arusha mjini akashinda.

  Makongoro aliamua kukiacha chama cha baba yake alichokiasisi huku akipanda jikwaani kupambana kwa hoja na Mwalimu Nyerere wakati akimpigia debe mgombea urais wa CCM, Benjamin Mkapa.

  Ingekuwa viongozi hawa wa leo kwanza hawangekubali mtoto wake aondoke CCM na kuingia upinzani na wangejitahidi kuwaingiza katika chama na pendine kustaafu akiwaacha wakiwa makatibu au makamu mwenyekiti. Kinachotutia hofu hapa ni kwamba kasi ya viongozi wetu kuwaingiza watoto waokatika mkondo wa siasa kwa kutumia majina yao unaweza siku moja kuifanya nchi hii kutawaliwa na familia moja tu huku wengine ambao hawako kwenye mkondo huo wataishia kuwa watazamaji tu.

  Hivi leo ikitokea familia yote ya rais ikawa bungeni, waziri mkuu anakuwa na watoto wake wane bungeni, mawaziri nao na watoto wao litakuwa bunge kweli ambalo lina meno ya kuibana serikali itekeleze majukumu yake?
  Tanzania ya leo inaweza ni ya amani, lakini hiyo isiwe sababu ya viongozi kudhani kuwa wakati wote watanzania watakuwa zuzu kuwakubalia kila jambo.

  Mwandishi wa makala hii ni Julius Samwel Magodi
  Source Mwananchi
   
 2. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  sijui tunakoelekea
   
 3. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda hii, na mawazo yangu ya kwanza ambayo naona siyo mazuri ni kwa wanaJF nao kutuma wawakilishi wao kila jimbo kuhakikisha tunatoa nasisi makamanda wetu ambao kazi yao ni kuhakikisha hawayumbwi na hawa jamaa wanaotaka kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kifaume.

  Watanzania wengi wamenyimwa elimu, wamekuwa waoga kila sehemu, leo hii mtu akija mtaani anatema utumbo wanashangilia badala ya kumtoa uvivu wanamkaribisha kisha kaja na hela. "This is crazy" Inasikitisha lakini yanamwisho wake.Ndivyo viongozi wetu walitaka wanancho wao wawe hivyo. Cha msingi ni kuwatoa ambapo nako si kazi ndogo, maana inahitaji resources nyingi.
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Sisi ambao wazazi wetu walikuwa ni wakulima hatuna nafasi katika uongozi wa nchi hii.
  Hata katika taasisi nyeti za serikali wengi ni watoto wa wakubwa.
  Nchi imekuwa ni ya Kifalme zaidi.
  Bora ujifanye huna makuu kwani mabo mengine ukiyafikiria sana utakonda bure!
   
 5. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Nashauri suala la 'Conflict of interests' liingizwe kisheria katika chaguzi mbalimbali ili kuepuka hali hii.
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  mwisho wa haya yanayosimikwa leo huwa ni umwagikaji mkubwa wa damu. Everything has its end. And it's end will come. It mighty not be leo, kesho au keshokutwa, but it will come. hata Idd amin, Charles taylor, Mobutu etc walitenda vivi hivi but they are no more!!
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Aug 10, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Huko ndiko tunakoelekea ingawa watu wengi hawataki kukubaliana na ukweli huu!
   
 8. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Siwaelewi sana wanachama wa hiki chama wanapokuwa wanapiga kura...
  Wanaangalia uwezo,fweza au surname..?...
   
Loading...