Ipo haja ya Membe kuinuka na Kumchallenge Magufuli ndani ya CCM

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,495
51,089
Rais Magufuli anadhani kuwa bila yeye Tanzania haiwezi kupiga hatua ya maana ya maendeleo.

Haya ameyazungumza Juzi kuwa bila yeye miradi ya ndege, miradi ya Stieglers na SGR haiwezi kufanyika!

Magufuli anahoji kuwa kama ni uongo mbona basi haijawahi kufanyika huko nyuma?

Rais anaongea as if Kaikuta hii nchi ikiwa ni bush na yeye ndo kaja kuwa mkombozi.

Lakini cha kujiuliza, Hivi nchi hii haijawahi kujenga reli yake tangu uhuru? - TAZARA

Hivi nchi hii haijawahi kuwa na miradi ya umeme? - Kihansi, Nyumba ya Mungu, Kinyerezi 1 na mingineyo aliijenga yeye?

Anazungumzia kuhusu vituo 352 vya tiba, Hivi Hospitali za Wilaya alizozikuta, Vituo vya Tiba alivyovikuta, Hospitali za kata alizozikuta zilijijenga zenyewe?

Magufuli alikuwa Waziri mwenye dhamana ya ujenzi wa barabara kipindi cha JK, na kipindi cha JK zilijengwa kilometa maelfu ya barabara kwa kiwango cha lami ina maana kwake hicho ni kitu kisicho na maana?

Tatizo ninaloliona Rais amelishwa propaganda na wapambe wake, propaganda ambazo na yeye ameanza kuziamini kuwa kabla ya yeye nchi hii haikuwa na kitu, na kwamba yeye ni mkombozi na kwamba akiondoka yeye hakuna Tena Tanzania!. Kitu ambacho siyo kweli hata kidogo!

Lakini ukiacha kengele hii ya tahadhari ambayo imepigwa kutubeep kuona reaction zetu za mtu kutaka kung'ang'ania madarakani tumeona katika siku kadhaa zilizopita nchi ikiendeshwa totally kinyume cha sheria na katiba.

mfano, Kitendo cha kuingilia mamlaka za utaratibu wa uendeshaji wa shule, Mamlaka ya kuadhibu wanafunzi kwa makosa yao si ya rais na kama kuna kosa la jinai katika matendo ya wanafunzi zipo mamlaka za kisheria za kufanya hivyo.

pia tumeona mamlaka za DPP zikiingiliwa, DPP akipangiwa cha kufanya huku kupangiwa huko kukijificha katika mask ya ushauri

Lakini ukiachilia mbali hilo, unaweza kuona muendelezo wa kuminya haki za watu ikiwemo vyama vya siasa, wao CCM wanaendelea kufanya mikutano lakini wapinzani wanakuwa harrassed.

Teuzi za mtu wa kuendesha chombo neutral kama vile NEC anateuliwa kada

Kibaya zaidi, Utawala huu unajenga personality cult badala ya kujenga mifumo endelevu, Leo Rais anataka kutuaminisha kuwa bila yeye hakuna maendeleo, lakini asichotuambia ni kwamba Kajenga mifumo gani imara ambayo bila yeye nchi itaendelea kuwa imara?. Yeye ni mwanadamu, hana mkataba na Mungu wa kuishi milele, Je akitoweka duniani ina maana Tanzania ndo imeisha haitaendelea kamwe?

Kwani yeye rais Magufuli ni Messiah wa Tanzania?

Alikuwepo Mwalimu Nyerere, Wakati Mwalimu anajenga reli ya Tazara rais Magufuli alikuwa na umri wa miaka takriban saba, Wakati mwalimu anajenga Shirika la ndege Rais Magufuli alikuwa na umri usiofika miaka 20,Sasaeo kweli Magufuli ndo wa kutwambia sisi watanzanka kuwa bila yeye hatuwezi kufanya miradi mikubwa ya maendeleo?

Kwa hiyo ni dhahiri ili kuondoa personality cult, na kuipeleka nchi katika sintofahamu inayoweza kuipeleka nchi katika machafuko ni lazima rais Magufuli aheshimu katiba. Kapewa nchi hii kwa amani na wenzake waliojitahidi kadri ya uwezo wao kujenga walichojenga, na yeye ajitahidi kadri ya uwezo wake kuijenga atakavyoijenga lakini aheshimu katiba.

Pamoja na hayo ni wazi rais Magufuli anahitaji challenger, mtu wa kumchallenge na kushake ego yake ndani ya chama. Si vizuri kiongozi aina ya Magufuli akaachwa aamini kuwa yeye ni invincible na kwamba yeye ndo hatma ya nchi na hatma ya nchindo yeye

Hapo ndipo nauona umuhimu wa Bernard Membe kuchukua fomu ndani ya chama.

Membe ni mtu mwenye uzoefu mkubwa, ni mtu aliyepikwa katika vyungu vyote vya uongozi, Membe si calibre ya viongozi wanaoweza kudhani kuwa wao ndo maendeleo na maendeleo ni wao.

Membe ni aina ya watu wanaoamini katika utawala wa sheria, ujenzi wa mifumo, Kuheshimu katiba na sustainable development.

Membe anaamini katika Quality ya vitu badala ya Quantity peke yake na ni aina ya watu ambao wanaijua diplomasia vizuri.

Kwa hiyo kama kweli Membe anaipenda nchi hii, na kama anaamini tunahitaji uongozi mpya, basi afumbe masikio asisikie kauli za wanaojifanya kuwa na busara eti kumshauri asichuke fomu, Inabidi afumbe macho asitizame propaganda za "2020 ni Magufuli tu"

Tunamhitaji Membe akaendeleze mchakato wa Katiba Mpya, kutatua tatizo la ajira nchini, Kupambana na Ufisadi kiukweliukweli badala ya reactionary measures kama za Magufuli katika hili jambo ambazo zimekaa kisiasa zaidi kuliko kimfumo wa dhati kabisa .

Tunataka Membe aende akalinde demokrasia yetu na kujenga mifumo imara na endelevu ya maendeleo badala ya personality cult.

Membe Popote ulipo itikia wito huu, nchi inakuhitaji kuliko wakati wowote ule tangu uingie kwenye utumishi wa umma!

MUDA UKIFIKA CHUKUA FOMU MZEE
 
sema wewe unamuhitaji sisi hatumuhitaji

Na wewe una haki pia ya kuwa na maoni yako

Ila hapa nchi ilipofika, Vijana wanaumia kwa ukosefu wa ajira, Nchi imegeuka kuwa ya one man show, Biashara kufungwa, Kampuni za Kandarasi kufutwa, Kilio cha hali ngumu ya umasikini nchini ni dhahiri Magufuli siyo option sahihi tena kuelekea 2020-2025.

Ni vyema Akatokea mtu ndani ya CCM ya kumchallenge, na kwa maoni yangu sioni mwenye utayari, na uthubutu ndani ya CCM. kuliko Benard Membe
 
Magufuli anasahau jambo moja muhimu sana....

Kuwa, "kuondoka" kwa tafsiri yake ni kushindwa uchaguzi tu....

Hajui kuwa binadamu sisi ni kama maua? Tunachanua na kung'aa asubuhi lakini jioni ikifika tunanyauka na kukauka kabisa!!

Bwana John Pombe Magufuli, shika neno hili....

Kuwa, ni kweli inaweza asiwepo mtu wa kukutoa katika nafasi na cheyo hicho....

Lakini kipo KIFO ambacho mimi naamini kabisa huna mkataba nacho...

Unaweza kulala leo mzima, lakini kesho ukaamuka umenyauka na pengine umekauka kabisa...

Usiseme "SITA....." au "NITA......", nakushauri siku zote mwachie Mzee wa siku yeye ndiye aamue hatima yako....

After all, mtu mwenyewe umri ulishakukimbia mzee wangu....unakimbilia kwenye 70s yet unatamani uyaishi madaraka ya Urais kwa 30yrs to come....kweli? Itawezekana vipi??

Sema, " MUNGU AKIPENDA TUTAONANA....au TUTAFANYA HIKI AMA KILE....."
 
Magufuli ana mazuri mengi kuliko mapungufu. Kisiasa hatumuhitaji kwa kuwa anaminya demokrasia. Lakini kwa upande wa usimamizi wa rasilimali na matumizi yake no objection kwamba ameweza.

Pia ni kweli Kuna uwezekano wa baadhi ya Miradi kufa kama kiongozi ajae hatakuwa na uthubutu kama wa Magu. Hivyo tuwe rational observer ndio tuijadili hii Mada. Simpendi Magu Lkn napenda sana anayoyafanya, na tukubali kuwa hakuna mtu asiye na mbadala ila Kuna wakati ni vigumu kupata mbadala wa mtu.
 
Taratibu za CCM zipo wazi kwa kila mwana CCM. Rais aliye kwenye kipindi chake cha kwanza cha urais hupewa fursa ya kugombea "peke yake" pale anapotafuta ridhaa ya chama ili agombee kipindi cha pili.
unamaanisha nini unaposema taratibu!?..una maana ya katiba au mazowea au kawaida!?
 
Humtakii mema huyo ndugu yako? Maana awamu hii ukijifanya unamkosoa wazi wazi au unataka kumnyang'anya huyo mzee pande lake la keki, basi ujiandae kutunguliwa kwa risasi kama Tundu Lissu, upotee kusikojulikana kama Ben Saanane na Azory Gwanda, au upambane mahakamani kwa kesi zisizo na dhamana za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.

Kwa kweli tumeingia kwenye 18! Waliompitisha huyu jamaa walifanya kosa la karne ndani ya nchi yetu. Mtu gani unawaza muda wote kusifiwa, kusujudiwa na kutukuzwa tu! Nyimbo zote ni za kumsifia tu, mapambio yote ni sifa tu, wapambe wote ni kumsifia tu, na sisi wote tuliobakia tunalazimishwa kumsifia tu.
 
Na wewe una haki pia ya kuwa na maoni yako

Ila hapa nchi ilipofika, Vijana wanaumia kwa ukosefu wa ajira, Nchi imegeula kuwa ya one man show, Biashara kufungwa, Kampuni za Kandarasi kufutwa, Kilio cha hali ngumu ya umasikini nchini ni dhahiri Magufuli siyo option sahihi tena kuelekea 2020-2025.

Ni vyema Akatokea mtu ndani ya CCM ya kumchallenge, na kwa maoni yangu sioni mwenye utayari, na uthubutu ndani ya CCM. kuliko Benard Membe
Mkuu umeshauri jambo jema sana, kwa kupitia kauli za Mkulu mwenyewe za hivi karibuni na wapambe wake wa karibu, kuna kila haja ya kumdhibiti mapema kabla ya mambo hayajaharibika kabisa. Nakumbuka enzi za Komandoo akiwa Raia wa Zanzibar, mazingira yalikuwa kama haya, isipokuwa uwepo wa Baba wa Taifa ulisaidia sana.

Ila kwa mazingira ya sasa naona inaanza kuwa vigumu, kwa kuwa waliomtangulia anawananga kwa uwazi kabisa pasipo wao kufanya lolote lile, angalau wale waliojaribu hata kuandika ule waraka, ijapokuwa walengwa waliukwepa na kukaa mbali nao. Angalau kupitia waraka ule wangaliweza hata kujaribu kumfunga paka kengere, lkn walipoteza fursa na kete muhimu sana.
 
Back
Top Bottom