Ipo haja ya kuangalia educational background ya wanaotoa maoni juu ya COVID 19 Tanzania

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
32,626
2,000
Watanzania wawe macho na waropokaji wote wanaongelea COVID 19 katika media mbalimbali.

Muda huu ni muhimu kuwasikiliza wataalamu wa afya Tanzania na wote waliotajwa kutoa taarifa rasmi.

Hata kama kuna muigizaji ,mwanasiasa au mtu maarufu sana anatoa maoni yake basi ni vyema kujua ana background gani ya kielimu au hata kwenye udhibiti wa magonjwa.

Mtu anaweza kuwa ni mwizi wa mitihani hapo awali au ni division sifuri au ni ngwini aliyekimbia sayansi sasa hivi ana followers wengi na yeye anajidai ni msemaji kwenye eneo la covid 19.

Waandishi mtusaidie kuiunganisha jamii na ma expart wa magonjwa ya milipuko tuacgane na vilaza.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
1,777
2,000
Mkuu unaweza kuwa na hoja kwenye andiko lako, ila au umepondtea sana kwa kuandika yafuatayo, ninakunukuu;

"ama ni ngwini aliyekimbia sayansi sasa hivi ana followers wengi na yeye anajidai ni msemaji kwenye eneo la covid 19"

Hivi unaona watu walio "opt" kwenye mkondo wa sayansi ndio tu vipanga pekee wenye kutambulika kitaaluma siyo! Acha hizo bro, sayansi ya bongo ingekuwa ni kama dhahabu, sidhani kama tenda za maana za miundombimu ya barabara, madaraja na hata ujenzi wa majengo mbalimbali wangalipewa Wachina, Wahindi na watu wa mataifa mengine.

Mkuu, with "due respect" hao unaowaita mangwini yupo wataalaamu tuliobobea katika fani mbalimbali, mf. sheria, uhasibu, fedha, uchumi, mipango, rasilimali watu, biashara, ujasiriamali nk. Ambapo bila sisi sayansi zako zitabaki kuwa hazina maana ktk ulimwengu wa sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
3,267
2,000
Misingi ya public knowledge ni consistency ya information jamii inayopewa; iwapo huku kuna Gwajima anakwenda 5G, Mama Lwakatare na masheikh wanaenda na mungu, hapo hapo kuna watu kama hakina Makonda; huku serikari kupitia timu zake rasmi inaenda na message zake.

Tegemea public confusion tu; we kama una akili zako timamu weka akiba ya paracetamol za kutosha nyumbani kwako come thank me in 1 or to 2 month.
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
32,626
2,000
pole kama umekwazika lakini ujumbe huu uliwalenga mangwini wote waliozoea kupiga domo nyakati za utulivu wa magonjwa ya milipuko...eti nao sasa wanataka kujidai wasemaji na watoa maoni kwenye jambo linalotumia ubongo kulitatua.

ujumbe ni kuwa ngwini wote watulie kwa sasa na wasubiri vipanga wawape nini cha kusema.
COVID 19 is for intellects to solve not some mburululas
 
King Ngwaba

JF-Expert Member
May 15, 2016
15,955
2,000
Hoja yako ni Ya Msingi lakini umekosea mbinu za kuiwasilisha kiasi ya kwamba inajionesha umewalenga Directly watu wa Kundi Fulani badala ya Watu wote.

Ni kweli sasahivi kila Mtu ni msemaji wa Corona (Covid-19) na anataka aaminiwe hata kama hana knowledge yoyote kwenye hili jambo la Kitaalamu bali anaishia kuchota habari mitandaoni na kujifanya ni taaluma yake na kutaka Watanzania waziamini.

Tanzania tunao!
1) Hygienists
2) Doctors
3) Other Health Personnel

Kwanini tusiwasikilize hao ambao ndiyo wataalamu wetu?

Wanasiasa (Vyama Vyote), Wanaharakati na Watu Maarufu na Wasiokuwa Maarufu wanyamaze na kuwaacha Wataalamu watoe Ushauri wa Kitaalamu na sio Wao kuingilia Kazi za Watu.

Nashairi tuwasikilize zaidi hawa Hygienists kwenye hili la Corona kwani wao ndiyo wataalamu wa Kinga
 
Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
5,651
2,000
Kuna ambao Prof. Kabudi alisema kemia hawakufikia hata kwenye "periodic table" ya kidato cha pili ila sasa hivi ni wachambuzi wa "concentration" ya madini yaliyomo kwenye makinikia!"
 
sblandes

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
5,372
2,000
Kuwa kiongozi au mtawala sio leseni ya kuwa bingwa wa kila jambo,ndio maana wanapewa washauri ambao ni mabigwa wa fani husika.

Lakini wapo watu wanatumia common sense kama huyo Mama japo sio medical specialist,tusiwapuuze.
 
Attachments

  • File size
    9.7 MB
    Views
    0

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
9,218
2,000
Kuna ambao Prof. Kabudi alisema kemia hawakufikia hata kwenye "periodic table" ya kidato cha pili ila sasa hivi ni wachambuzi wa "concentration" ya madini yaliyomo kwenye makinikia!"
Atakuwa alikuwa anajisema mwenyewe.
 
Ngunichile

Senior Member
Nov 27, 2019
128
250
Kuwa kiongozi au mtawala sio leseni ya kuwa bingwa wa kila jambo,ndio maana wanapewa washauri ambao ni mabigwa wa fani husika.
Lakini wapo watu wanatumia common sense kama huyo Mama japo sio medical specialist,tusiwapuuze.

Hapa ndo unaona umuhimu wa shule, amederive kwa dk 5 tu unapata new hope, new directions, contingency plan, New Thought, guidance

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mwanamena

JF-Expert Member
Feb 4, 2020
552
1,000
jingalao, Huuu Uzi naona Ni jiwe ambalo limerushwa nuruni, limemlenga jamaa mmoja hivi. Maana japo upotoshwaji upo, kiuhalisia Shule alikimbia, kwa usanii ana followers wengi sana, nchi hii.

Msemaji wa Covid-19.

Kama alipotosha iweje asamehewe, Sheria inasamehe jinai,? Ulengwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanamena

JF-Expert Member
Feb 4, 2020
552
1,000
Kuwa kiongozi au mtawala sio leseni ya kuwa bingwa wa kila jambo,ndio maana wanapewa washauri ambao ni mabigwa wa fani husika.
Lakini wapo watu wanatumia common sense kama huyo Mama japo sio medical specialist,tusiwapuuze.
Mkuu ,nimemsikiliza huyu mama, amezungumza truth and only the very truth. Imetouch my five senses. Mungu aijaze roho ya kuelewa, hili alilolisema huyu mama, kwa viongozi wetu.

Nature for real heals than these Oxford education.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
37,404
2,000
pole kama umekwazika lakini ujumbe huu uliwalenga mangwini wote waliozoea kupiga domo nyakati za utulivu wa magonjwa ya milipuko...eti nao sasa wanataka kujidai wasemaji na watoa maoni kwenye jambo linalotumia ubongo kulitatua.

ujumbe ni kuwa ngwini wote watulie kwa sasa na wasubiri vipanga wawape nini cha kusema.
COVID 19 is for intellects to solve not some mburululas

Updates za viwanda zimekushinda, saa hii unarukia mipasho ya mambo mepesi.
 
kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
5,969
2,000
Tatizo lako na la wale mnaodhani ni vipanga mlicho nacho ni karatasi tu za shahada.Hakuna hata mmoja wenu aliye maabara sasa hivi zaidi ya kusoma taarifa za mtandaoni tu ambazo kila mtu ataziona.

Mwisho wale unaowabeza kwa kukosa makaratasi ya shahada za uzamili ndio hatimaye watagundua dawa ya covid 19.
pole kama umekwazika lakini ujumbe huu uliwalenga mangwini wote waliozoea kupiga domo nyakati za utulivu wa magonjwa ya milipuko...eti nao sasa wanataka kujidai wasemaji na watoa maoni kwenye jambo linalotumia ubongo kulitatua.

ujumbe ni kuwa ngwini wote watulie kwa sasa na wasubiri vipanga wawape nini cha kusema.
COVID 19 is for intellects to solve not some mburululas

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom